Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

HII THREAD SI YA KUSHINDANISHA URUSI NA UKRAINE BALI PICHA NA VIDEO ZA MAFANIKIO YA UKRAINE WALIO FRONTLINE VITANI.
Hoja kubwa hapa ni.
1. Tunafurahia mafanikio ya Ukraine sababu wameonewa, wanauawa bila hatia na wamevamiwa bila sababu ya msingi eti kwa sababu Rusia ana uwezo wa kijeshi. Kitendo cha kumtoa Russia kwenye ardhi ya Ukraine na kumpiga tunafurahia sana.

2. Tunafurahia ushindi wa Ukraine kwa sababu kamvua nguo aliyekuwa anafanya propaganda kuwa yeye ni super power, matokeo yake tumejua kumbe hana lolote.

3. Tunafurahia Ukraine kwa sababu amesimama imara kutetea nchi na watu wake. Haiwezekani jilani akuchagulie marafiki. Ukoloni mamboleo tunaupinga.

4. Tunafurahia ushindi wa Ukraine sababu, malengo na ndoto ya Putin kuiteka Ukraine yamepotea, badala yake yeye ndo kanasa. Wanaume wamemsubiri siku nyingi sasa kashanasa hawezi kutoboa. Atafurushwa kwa aibu kubwa. Muda utaongea.
 
Wameshaelewa. Sababu wanakuja kana kwamba tunashindana. Sisi tunaweka picha za Frontline. Kuliko kuja kutuharibia thread wapost hayo mambo kwenye thread yao ya Ubabe na ugaidi wa Urusi mwenye tamaa na mali za Jirani yake.
 
Kamanda wa Vikosi vya Urusi anayeitwa Gen Surovikin aka Amargadon, ametumbuliwa. Ni baada ya kuwa anatoa habari za Uongo. Anadai Urusi imeteka Sehemu fulani akijua ni uongo. Sasa kafurushwa. Wamemsaidia, angefia Ukraine
 
Good Analysis.

Analysis kama hizi zinaipa value mada na kupanua uelewa wa situation inavyokwenda katika uwanja wa mapambano.
 
Nani kakuambia hii mada ni ya Analysis? Anzisha mada yako ya Analysis.
Ndugu, with due respect. Wewe kuanzisha mada haimaanishi una own mada. From now on tutachangia tunavyotaka na hutotufanya lolote.

Nimekuheshimu sana ila inaonekana hujiheshimu.

Mimi ni pro Ukraine na nimesharusha mavideo na mapicha chungu nzima humu ya kuonyesha mafanikio ya Ukraine.

Ila kwa kuwa unaanza kubehave kama mjinga basi tutakwenda hivyohivyo from now on!

Na Hatoki mtu hapa!
 
Sihitaji heshima yako. Sababu sheria zinazoongoza mijadala zipo. Huwezi kupost kitu nje ya mada. Pambana na hali yako. Urusi tutawabutua hadi mtie adabu. Unakuja kwenye mada ya mjinga kufanya nini kama nawe si mjinga? Hii ni mada ya picha si vinginevyo. Mada yenu ya matusi msiikimbie nenda mtukane huko
 
Kiapo cha utii bila kutumia hata akili, kitawaponza sana hao makanali kwani utekelezaji wa Agizo hilo la Putin ni next to impossible. -Askari wa Urussi ni mdebwedo ila askari wa Wagner ndio waliopo kuweza kusimama kukabiliana na Ukraine. Lakini mtu wa mshahara (Wagner)ni tofauti na mtu (Ukraine)anayepigana kwa uzalendo na kuipenda nchi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…