Hoja kubwa hapa ni.HII THREAD SI YA KUSHINDANISHA URUSI NA UKRAINE BALI PICHA NA VIDEO ZA MAFANIKIO YA UKRAINE WALIO FRONTLINE VITANI.
1. Tunafurahia mafanikio ya Ukraine sababu wameonewa, wanauawa bila hatia na wamevamiwa bila sababu ya msingi eti kwa sababu Rusia ana uwezo wa kijeshi. Kitendo cha kumtoa Russia kwenye ardhi ya Ukraine na kumpiga tunafurahia sana.
2. Tunafurahia ushindi wa Ukraine kwa sababu kamvua nguo aliyekuwa anafanya propaganda kuwa yeye ni super power, matokeo yake tumejua kumbe hana lolote.
3. Tunafurahia Ukraine kwa sababu amesimama imara kutetea nchi na watu wake. Haiwezekani jilani akuchagulie marafiki. Ukoloni mamboleo tunaupinga.
4. Tunafurahia ushindi wa Ukraine sababu, malengo na ndoto ya Putin kuiteka Ukraine yamepotea, badala yake yeye ndo kanasa. Wanaume wamemsubiri siku nyingi sasa kashanasa hawezi kutoboa. Atafurushwa kwa aibu kubwa. Muda utaongea.