Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Wagners wengine hawa huku wanaomba Makombora ya Vifaru vyao. Si wamuombe Urusi? Watakoma, ndo kwanza moto umeanza
View attachment 2521372
Inavyoelekea Viongozi wa jeshi rasmi la Urusi wanawaonea wivu Wagner, angalau Wagner wanasimama kiume ila jeshi rasmi wao wakipigwa offensive wanakimbia. Kwa hiyo ni kama wanahujumiana, hawawapi wagner kila wanachohitaji
 
Inavyoelekea Viongozi wa jeshi rasmi la Urusi wanawaonea wivu Wagner, angalau Wagner wanasimama kiume ila jeshi rasmi wao wakipigwa offensive wanakimbia. Kwa hiyo ni kama wanahujumiana, hawawapi wagner kila wanachohitaji
Tatizo linaweza kuwa supply route imekatwa. Sidhani kama Urusi anaweza kufanya sabotage wakati anataka ashinde vita.
 
Tatizo linaweza kuwa supply route imekatwa. Sidhani kama Urusi anaweza kufanya sabotage wakati anataka ashinde vita.
Mmmh! Mm nadhani tatizo linaweza kuwa Wagner hajagundua kwamba boss wake aliyemkodishia vita (outsource) Urussi, mambo yamemkalia vibaya na alichobaki nacho huyo boss ni uwezo wa kulipa kwa mujibu wa Mkataba. Hii ni kwa sababu wanajeshi wake waliokuwa mahiri + makamanda (majenerali) katika vita wameuawa wengi hadi amefikia mahali anahiari kumpa mkuu wa askari wa Wagner Ukuu na amsimamie mkuu wa majeshi ya Urussi. Yan inachekesha sana, ni kama kwa mfano hapa Tz, kiongozi wa NGO fulani ndani ya Wilaya apewe mamlaka ya kumsimamia DED wa wilaya husika katika utendaji wake wa siku kwa siku....ikimaanisha DED atapokea maelekezo ya ni nini cha kufanya kutoka kwa kiongozi wa NGO ambayo ipo ndani ya wilaya yake.
 
Inavyoelekea Viongozi wa jeshi rasmi la Urusi wanawaonea wivu Wagner, angalau Wagner wanasimama kiume ila jeshi rasmi wao wakipigwa offensive wanakimbia. Kwa hiyo ni kama wanahujumiana, hawawapi wagner kila wanachohitaji
Hahahaaa. Mkuu unasema jeshi rasmi hawawapi wagner kila wanachohitaji.
Jeshi rasmi watakitoa wapi hicho ambacho Wagner wanakihitaji??? HAWANA lakini hawaweki wazi. Ila Wagner nao ni duwanzi kweli kwa sababu hawashangai wala hawajiulizi kwamba inakuwaje imefika mahali mtu (Wagner) unapewa uongozi wa juu kabisa kuongoza majeshi ya Urussi wakati Warussi wenye ngoma yao hiyo wapo???
 
Hebu nitoeni tongotongo;

1. Ni lini Head of PMC aliteuliwa na Putin kuwa na mamlaka ambayo yalomfanya awe juu ya CDF wa Russia au commander kiongozi wa kinachoitwa SMO.?

2. Ni lini Head of PMC amekuwa Commander of SMO Ukraine.?

3. PMC anajinunulia military equipment au anapewa military equipment na Jeshi la Russia.?

Nitafurahi kama nitapata majibu ya kina yanayoambatana na ushahidi.
 
Hivi Bayraktaars ziliishia wapi?.
Ziliisaidia sana Ukraine kuthibiti advance ya Urusi kuelekea Kyiv
Kwa sasa tukonkwenye phase nyingine ya kivita zile drone hazina haziitajiki tena matumizi yake kwa aina hii ya vita iliyopo saiv haviendani kila phase ha vita na aina ha silaha ndo maana kwa sasa kwa sababu mbinu za kivita zimebadirika basi unaona ata matumizi ya HIMARS pia yamepungua hii ni kutokana na mbinu za kivita zinabadirika kila siku ma ujue na adui naye ni binadamu anayo mawazo na anawazua jinsi ya kuzizuia silaha zetu!!
 
Are you serious kuwa matumizi ya HIMARS yamepungua.

Kinachofanya Russia na Wagner walalamike upungufu wa risasi, vifaru na artillery frontline ni nini kama siyo HIMARS kunyemelea maghala ya silaha na kubomoa madaraja.

Kikosi cha HIMARS bado kinapiga mzigo wa maana.
 
Msaada wao ni wamempa darasa / kumsomesha huyo mshirika kwamba akomae na hali yake na kila mtu ashinde mechi zake. Wanampiga dana-dana.
N. Korea anafuatilia mechi yake na S.Korea; China naye yuko bize na hoja ya Taiwan.
Na msababishi mkuu, ni USA; kwa sababu Taiwan yupo, Korea kusini yupo, Ukraine yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…