Mmmh! Mm nadhani tatizo linaweza kuwa Wagner hajagundua kwamba boss wake aliyemkodishia vita (outsource) Urussi, mambo yamemkalia vibaya na alichobaki nacho huyo boss ni uwezo wa kulipa kwa mujibu wa Mkataba. Hii ni kwa sababu wanajeshi wake waliokuwa mahiri + makamanda (majenerali) katika vita wameuawa wengi hadi amefikia mahali anahiari kumpa mkuu wa askari wa Wagner Ukuu na amsimamie mkuu wa majeshi ya Urussi. Yan inachekesha sana, ni kama kwa mfano hapa Tz, kiongozi wa NGO fulani ndani ya Wilaya apewe mamlaka ya kumsimamia DED wa wilaya husika katika utendaji wake wa siku kwa siku....ikimaanisha DED atapokea maelekezo ya ni nini cha kufanya kutoka kwa kiongozi wa NGO ambayo ipo ndani ya wilaya yake.