kikiboxer
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 3,668
- 9,809
Mkuu hii nakubaliana na wewe.Russia ni super power wa kwenye sinema siyo frontline battles.
Hoja zifuatazo zinadhibitisha hayo;
1. Kushindwa kuiteka Ukraine ndani ya masaa 72 na badala yake mwaka 1 na ushehe hajateka hata 25% ya ardhi ya Ukraine ni ushahidi kuwa kumbe Russia ni super power wa kwenye sinema.
2. Ukraine imetudhibitishia kuwa ina jeshi imara lenye mbinu za kisasa kuliko Russia/Wagner. Ndiyo maana ameweza ku hold frontline ya zaidi ya km 1,200 na kumthibiti Russia ashindwe ku advance ni ushahidi tosha kuwa Russia ni super power wa kwenye sinema.
3. Russia anayejiita super power kashindwa kuteka vimji vidogo kama Bakhmut, Vulhleder na Avdiivika zaidi ya mwaka sasa. Matokeo yake maeneo hayo yamekuwa machinjio ya wanajeshi wa anayejiita super power. Hii inadhibitisha kuwa ni super power wa kwenye sinema siyo frontline.
4. Kitendo cha kuelekeza hasira zake kwenye nyumba za makazi ya watu na kubomoa miundo mbinu ya umeme na maji badala ya kambi za jeshi na frontline ya Ukraine ni ushahidi mwingine kuwa Russia frontline battle hawezi. Ni ushahidi mwingine kuwa Russia hana uwezo mkubwa wa kijeshi tofauti na ambavyo tuliaminishwa kuwa ni super power.
Hitimisho.
1. Russia hatashinda vita hii iwe jua au mvua.
2. Russia mwaka huu ataondolewa kwenye maeneo yote ya Ukraine ikiwemo Crimea kwa aibu kubwa.
3. Russia baada ya kufurushwa maeneo yote ya Ukraine atabaki kurusha vikombora ambavyo vimeshinda kuwafanya wananchi wa ukraine ku frozen wakati wa winter kama alivyokusudia. Sasa hawezi tena na u super power wake wa kwenye sinema.
Russia kuna kipindi nilijua ataichukua bakhmut lakini kwa hali ya sasahvi naona hata hiyo bakhmut hana muda hapo watamfurusha mbali.