Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Kifaru kiliwasigina Warusi kama karanga za kuungwa katika mboga ya kisamvu. Duh!
 
Slava Ukraine [emoji1255]
 
Wagner/Russia wanaopigana Bakhmut si wa kubezwa.

1. Wanajeshi wa wagner/Russia wanaopigana Bakhmut si wa kubezwa kwa propaganda ya aina yoyote. They are real fighting to take Bakhmut. Kwa mbinu za kivita Ukraine imezidiwa na Wagner/Russia kwa Bakhmut. Bakhmut ikichukuliwa mimi sitashangaa hata kidogo zaidi ya kuhuzunika.

2. Offensive waliyoifanya Wagner/Russia mashariki mwa Bakhmut na kaskazini kuanzia 26/03 hadi 04/04/2023 na kuwapa mafanikio kwa kusonga mbele hadi kuwa na control (be under their fire control) ya barabara zote 3 zinazoingia ndani ya mji kutoka mashariki, kaskazini na kusini mpaka makutano ya njia zote 4 (T1302, T0513, T0504). Njia pekee ambayo Wagner/Russia hawana control nayo ni kutokea makutano ya njia nne kuelekea Kostyantynivka(T0504). Hii ni dalili kuwa Bakhmut itachukuliwa muda si mrefu kama Ukraine hawatabadili mbinu ya kukabiliana na wagner/Russia.

3. Kama Ukraine wanasubilia mpaka waanze counter offensive yao ndo waimarishe frontline ya Bakhmut, basi watakuwa wanataka kuruhusu wagner/Russia watengeneze historia mpya kwa Bakhmut.

4. Kuruhusu wagner/Russia wachukue Bakhmut kutaondoa morali kwa wapiganaji wa Ukraine na wananchi wa Ukraine. Watawaathiri wapiganaji wa Ukraine kisaikolojia na kuwajengea confidence Wagner/Russia ya kuongeza mashambulizi zaidi na kumpa credit Putin kwa wananchi wake.

5. Wagner wakichukua Bakhmut, Ukraine itatumia nguvu kubwa sana kuikomboa tena Bakhmut.
 
Kitu kizuri ni kuwa wagner na jeshi la urusi wapo kwenye mgogoro tangu mwaka jana mwishoni wagner wanachukua ujiko huku jeshi la Russia likionekan si kitu.
 
Kitu kizuri ni kuwa wagner na jeshi la urusi wapo kwenye mgogoro tangu mwaka jana mwishoni wagner wanachukua ujiko huku jeshi la Russia likionekan si kitu.
That is obvious, Wagner wanataka kuionyesha dunia kuwa wana jeshi imara ili wapate kazi zaidi. Kazi yao kubwa ni kukodiwa si na Russia tu bali na nchi yoyote.

Wagner wanaitumia Bakhmut kama show ya kujitangaza mbele ya dunia kuwa "they are capable and can fight under intensified situation"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…