Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Jana Jeshi la anga la Urusi, liliangusha na kuteketeza ndege zao nne wakijua ni ndege za Ukriane.

Nxege zilizolipulia ni Helkopta 2 aina ya Mi-8, ndege moja aina ya Su 34 na nyingine moja aina ya Su 35
20230514_131113.jpg
 
Huko Bakhmut kuna sehemu Urusi na Wagners wamepelekewa moto. Walivyoona wamekufa 200 ndani ya siku moja ikabidi waretreat. Wagners wanalalamika kwamba Wanajeshi wa urusi wakiachwa kwenye post wakirudi wanakuta wamekimbia
20230514_142140.jpg
 
Russia inapambana kuisambratisha mitambo miwii ya kuzuia makombora toka Marekani na Ujerumani iliyoko Ukraine. Mitambo hiyo aina ya "Patriotic" inaweza kutambua makombora yakiwa umbali mrefu sana hivyo kuwa na uwezo wa kuzuia makombora ya masafa ya kati ya Russia.

Kutokana na uwezo huo wa kutambua makombora (Detect) yakiwa mbali, hali hiyo inaifanya mitambo hiyo pia kuwa dhaifu kudukuliwa mahali ilipo. Tofauti na mitambo mingine ya kudungulia makombora ambayo inahamishika, Patriotic haihamishiki hivyo kufanya kama masafa yake yakidukuliwa kuwa rahisi kushambuliwa na Makombora ya adui,

Mitambo hiyo ambayo tangu iingie Ukraine ina chini ya mwezi, imepelekwa huko mapema baada ya wanajeshi wa Ukraine kufuzu mafunzo ya awali ya matumizi ya mitambo hiyo mapema zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

Sasa mitambo hiyo ndiyo inatumika kudungulia makombora ya Russia aina ya Hypersonic ya Kinzhal au Killjoy. Russia imesema mitambo hiyo ndiyo itakuwa lengo la kwanza kushambuliwa na makombora kwa lengo ya kuendelea kulifanya anga la Ukraine kuwa tupu dhidi ya mashambulizi hayo ya Russia.

Mei 6 Mwaka huu baada ya masafa ya Patriotic kudukuliwa na Russia, Russia ilirusha makombora kadhaa aina ya Kinzhal kwa lengo ya kuushambulia mmojawapo wa mitambo hiyo lakini makombora hayo yalidunguliwa na mitambo hiyo.

Kutokana na Russia kuwa na uwezo wa kudukua masafa ya mitambo hiyo hata kama kuna masafa Kanyaboya (camouflage frequency) yanayotumiwa na mitambo hiyo kupoteza ilipo, wizara ya Ulinzi ya Marekani na Jeshi la Ukraine wanatafuta njia ya kuilinda mitambo hiyo ili isishambuliwe na Russia kwa kuongeza ulinzi wa kielektronik ili kulinda masafa ya mitambo hiyo yasitambuliwe wakati ikitafuta uelekeo wa makombora yanayorushwa toka Russia.
Bro unasemaje patriotic ni ngumu kuhamisha wakati ni mobile?
images%20(1).jpg
Airday-Nordholz_2013_by-RaBoe_106.jpg
 
Back
Top Bottom