Wataalam wa Vita, wanasema Urusi haijawahi kushinda Vita yoyote tangu kuumbwa kwake. Nimeanza kuamini
Picha. Maiti za Urusi zikipelekwa jalalani. Hamna wa kuwazika
View attachment 2217487
Inaweza kuwa kweli kwasababu hata vita ya pili kama siyo Marekani kumsaidia kwa kumpa silaha,vyakula, dawa na intelijensia wakisaidiana na Uingereza Mnazi alikuwa anampiga mapema mno.
Kumbuka Hitler alikuwa ameshaanza kuichungulia Moscow.
Alienda Finland kinchi kidogo na population ndogo kushinda Ukraine lakini alipigwa mpaka akaomba mazungumzo ya amani na kusainishana mkataba kwamba hataivamia tena.
Ndipo Hitler akamcheka Stalin kwamba ameshindwa kuivamia nchi ndogo hivyo, akaamua naye kuvunja makubaliano ya kuigawa Poland katikati. Akaanzisha Operation Barborasa mwaka 1941 kumuenzi mfalme wa Italy wa karne ya 15 kama sijakosea.
Kwahiyo unachosema kinaweza kuwa kweli hata kama akishinda ni kwa kusaidiwa na wakati huo huo anakuwa ameaua wanajeshi wake na raia wengi sana.
Ukiangalia ile vita ya pili inasemekana watu zaidi milioni 65 walikufa. Lakini nchi ambayo watu wake wengi walikufa ni Urusi zaidi ya milioni 25.
Hii ni kwasababu mbinu zao za upiganaji si nzuri wanaamini no step back , mtu anaenda uelekeo huo huo mahali machine gun inapiga, ukielekeo uelekeo mwingine unapigwa shaba na kiongozi wako kwamba una dissert. Sijui wanajivunia wingi wao (personnel).
Mipango mikakati ya vita si mizuri.Ukraine kwa Urusi ni aibu alitakiwa awe ameshamaliza kazi ndani ya zile siku 3.Watu wanasema eti Ukraine anapewa jeuri na Marekani na NATO, ni sawa kwa upande mwingine kwani kabla hajavamia hakujua kwamba atasaidiwa?
Na kama alijua alipuuzia kwa kuamini kwamba atampiga jirani yake, intelijensia yake haikujua kwamba Ukraine atasaidiwa,kama alijua alipuuzia kwa kujiona yeye ni bora.
Lakini aliambiwa pia kwamba Ukraine haitakuwa peke yake. Asilalamike kwamba anasaidiwa apambane nao wote ili tumpe heshima yake. Huwezi kuamka asubuhi unasema unaenda kumpiga jirani yako kwasababu zako binafsi halafu watu wengine wakuache tu utambe ifike mahali dunia tuheshimiane sote.