Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Mji unaofuata ni Donetsk. Ila bado Mariupol ipo mbali. Hadi Jeshi la Ukraine wafike sio leo. Nadhani Jumatatu tunaweza ikomboa Donetsk. Izyum ndo ilikuwa inachelewesha. Tukiipata Mariupol nasi tunawazingira Wanajeshi wa Urusi waliopo Melitopol. Subiri muone huu Mchezo.
View attachment 2224248View attachment 2224249
Hawa jamaa kwa jinsi wanavyojua madhara ya kuzungukwa wakizidiwa wanaweza kukimbia wakaacha kila kitu wakiogopa kile kitu walifanyiwa na Hitler Leningrad, hakuna kutoka wala kuingia, hakuna chakula wala maji mpaka ikatokea Cannibalism.

Mtu yeyote anayeshadadia vita ajifunze madhara yake. Vita iepukwe kwa nguvu zote,kama kuna kuongea busara zitumike kwa sehemu kubwa. Hata nchi ikiwa na nguvu kiasi ganu kuna madhara itayapata tu.
 
Mkuu Putin alikariri alishazoea alibeba crimea kirahisi tu kama mali yake. Sasa this time hakupiga hesabu zake vizuri na hii si kwamba eti tunaleta propaganda kwamba hawana intelligrnce nzuri lakini ukirejea wakati wanaanza operation walianza kwa nguvu sana za mashambulizi bila resistance kubwa ikafika mahali Putin akaanza kuwatahadhatisha wanajeshi wa ukraine waweke silaha chini wampindue Zelensky.

Kumbe mambo yanabadilika kaingia chaka bovu this time kama akishinda basi ni kwa jasho na damu na hasara chungu nzima.
Ni kweli Mwanzo huwa mzuri lakini adui yako akishakusoma udhaifu wako unaumia.

Chukulia Nazi walivyowapiga Europe akitaka kuimarisha utawala wa himaya ya the third Reich Czechoslovakia iwe ndipo makao makuu.

Japan US pale Pearl Harbour.

Ug na Tz Kagera war.

Russia Afghanistan.

US na Vietname.

Lakini ukiangalia upande uliokuja kuathirika zaidi na kupigwa ni wale wote walioanza kuwapiga wenzao. Vita ikageuka aibu ikawa kwao. HAKI HUSHINDA UOVU.
 
Putin hawezi kushinda hii Vita. Kwq kuwa alishindwa kuzuia Silaha kuingi Ukraine, basi kila kitu atashimdwa. Anapigwa na Silaha za Kisasa. Analeta Vitisho vya nyuklia lakini NATO ndo nyumbani mwq Nyuklia naye ajaua. Moscow itachakazwa sana.. Mbaya wa Urusi ni LEGION
Makamanda wake hawatamruhusu atumie Nyuklia kirahisi. Halafu akishindwa hii vita kabla hajaondoka madarakani wananchi wake hawatamuamini mama shujaa wao kwa jinsi alivyowaaminisha atashinda.

Aibu yake itakuwa kubwa atakosa ujasiri wa kuongoza watu wake tena.
 
Tumefika Luhansk
20220514_224801.jpg
20220514_224759.jpg
20220514_224757.jpg
 
Hawa waliolala hapa ni kikosi cha anga cha Urusi Wakishambulia Vifaru vya Urusi kwa FGM-148 Javelin huko Donbas. Kumbe wapo Vizuri hata Ardhini.
 
Hawa wanaotumia hii 60-mm M224 mortar ni Wapiganaji wa kujitolea kwa ajili ya Ukraine kutoka Georgia
 
Hii bunduki anayoitumia Sniper wa Ukraine ni hatari. Unatakiwa uwe umekula
 
Back
Top Bottom