Hakika mkuu. Putin alicalculate vibaya kwenye hii vita. Halafu ukiangalia historia yake kwenye vita huwa anapoteza askari wake wengi kwa uzembe tu ,sijui mafunzo yao yakoje, hata kwa mtu ambaye siyo expert wa jeshi na vita unajiuliza why hakupita pale badala yake amekuja open namna hii?
Ukiangalia askari wa majeshi mengine unaona kama vile ulivyowaza ndivyo na yeye anavyofanya.
Putin alijiamini katika wingi wa personnels na equipments, akasahau wenzake wako na strong strategies and morale ya kutosha.
Luteni Generali Silas Mayunga kipindi cha Kagera war askari wake walimpenda sana kwasababu alikuwa anawapa mzuka sana,maneno yake yalikuwa yanawapa hamasa wapiganaji.
Baadhi aliwaambia askari kushinda vita siyo wingi wa kuwa na silaha bora na za kisasa bali kupigana kwa kumsogeza adui nyuma na wewe kusonga mbele..."
Askari yoyote ambaye hayuko tayari kupigana hata umpe silaha nzito na bora kiasi gani hawezi kushinda vita sana sana hatazilinda ataziacha na kutumiwa na adui kukupiga wewe mwenyewe.
Ukubwa wa nchi Siyo ushindi wa vita bali hiyo vita unapigana kwa ajili ya nini. Tusiidharau nchi yoyote mkuu kwa udogo wake.