Hii ni wazi kuwa kuna kitu hakiko sawa. Binafsi sishangai. Ipo siku tutasikia Wagner group (Russia mercenary group) hawamtaki Putin.Warusi wanagombana wao kwa wao Frontline. Kuna nini tena? 🤣🤣🤣
View attachment 2397206
Hili group ndo linafanya vita iwe ngumu na kwenye hii vita Wagner militia group wana play role kubwa sana kuliko hata jeshi la Russia sababu ya uzoefu wao kwenye vita. Siku majeshi yote ya Russia including Wagner group wakifurushwa Ukraine, sitashangaa kusikia mzozo kati ya Putin na hilo group. Kwa kuwa lina nguvu lina uwezo wa kumwondoa Putin madarakani kwa kushirikisha na wanasiasa wa Russia.
Ukraine haisongi mbele kwa kasi Donetsk, Kherson na Zaporizhzha sababu hawa jamaa (Wagner group) wamejidhatiti sana maeneo hayo yenye rasilimali nyingi na utajiri mkubwa. Wagner group wananufaika sana na kufurushwa pale ni kukoseshwa rasilimali wanazochuma hapo.