OSEFUKANY
JF-Expert Member
- Jan 16, 2011
- 2,437
- 3,896
Nyani katema bungo, Hahaa. Mrussi angelijua kwamba Ukraine hana shida na old fashioned silaha asingelihaha kiasi hicho kuzikimbiza. Ukraine alishasema na akarudia tena na tena: Mrussi aondoke kwenye ardhi ya Ukraine lakini wapi .Mrussi kakaza fuvu. Hayo machuma-chuma yake ya mwaka 47 nani anayataka? Ajibee makorokoro yake aliyoingiza huko Ukraine aondoke nayo akamwoneshe mke wake. La! Hataki basi ajue kuendelea kuwepo kimabavu kwa Mrussi kwenye ardhi ya Ukraine ni kichefuchefu.Urusi inaelekea imekubali matokeo huko Kherson Magharibi. Wameamua kuondoa vikosi vyao vya mizinga huko, nahisi wanahifia hivyo vikosi kutekwa na silaha kuangukia mikononi mwa WaUkraine