Aisee, Mrussi imekuwa ni bahati mbaya sana kwake kwani kila juhudi anayoifanya kuhusu vita hii anajikuta anazidi kujisokota kama samaki kwenye nyavu. Ukifuatilia mtiririko wa kauli zake ambazo ndo juhudi zake kujinasua utamsikitikia. Alianza na vitisho kwa Rais Zele kwa kumwambia akimbie au ajisalimishe bila mashartiyoyote Akatoa vitisho kwa mataifa yatakayothubutu kumsaidia dogo Zele, Akatishia matumizi ya nyuklia, Akaonya upelekwaji wa silaha Ukraine, Akatishia kulipua mtambo wa nuklia uliopo Ukraine, mara akaanza hoja hizi za kijinga e.g. mikoa 4-5 iliyotekwa 2014 ibakie kuwa ni ya Urussi ili vita iishe, mara Ukraine akubali mikoa hiyo 4-5 ikaliwe na Urussi kwa miaka 7 then irudishwe Ukraine, mara Ukraine tukae meza moja tufanye makubaliano ....sasa anabadilika anasema Ukraine atambue mikoa mitatu ni Urussi, juzi kasema kuwe na mkataba baina yake na USA&NATO kwamba atakuwa salama na NATO hawatajipanua kuongeza maeneo ....dah! mzee mpuuzi kweli kweli anadhani wenzake ni std 7 wakuyumbishwa yumbishwa kivile. Ndo maana wakubwa wamefikia mahali wamemwona "ananuka" hafai.