Nilichojifunza kuhusu sakata la makombora yaliyotua Poland;
1. Russia kumbe anaiogopa sana NATO, alivyokanusha kwa haraka na kwa utetezi mkubwa ni dhahiri anaogopa vita kati yake na NATO.
2. Russia alijua kagusa sharubu za Simba, hasa ukizingatia kuwa hili limetokea wakubwa wa Dunia wakiwa wamekusanyika Indonesia. Alijua watasema apigwe au asulubiwe.
3. USA na NATO ni watu wastaarabu sana na wanaofanya kazi zao kwa misingi ya haki. Walikuwa na uwezo wa kumsingizia Russia kuwa kapiga kwenye NATO territory na kuchukuliwa kama sababu ya kumpiga Russia. Lakini Pentagon na Biden wamekuwa wa kwanza kuweka angalizo kuwa "Unlikely Russia ......" japo wanajua Russia hakurusha hilo Kombora Poland.
4. Pro Russia wamekuwa wa kwanza kueneza habari kuwa USA imesema kuwa Russia haijahusika huku wakijua uchunguzi haujakamilika. Lile Neno lililotumiwa na Mzee Biden na Pentagon kuwa "Unlikely Russia ........., we are waiting for investigation". Hawajataka hata kusikia maneno mengine "....... waiting for investigation", wao wame conclude kuwa USA na NATO wamesema Russia haijahusika.
Kwa kifupi, kumbe anayejiita super powers anaiogopa NATO. Alijua akikaa kimya hata kwa siku moja bila kukanusha wanaume wanaweza kumfanyizia.