Mimi ni pro Ukraine. Mkuu wa majeshi hajatangaza kwamba sehemu fulani tumepoteza, kwanini niseme? Sababu taarifa zipo wazi na Jeshi likipoteza linasema. Mfano pale Soledar, rais Zelensky kasema mapambano yanaendelea. Mimi nawasikiliza Viongozi wangu. Siwezi kucheza ngoma ya Pro Urusi. Tuongee vitu tukiwa na chanzo cha habari.
Je, chanzo cha kusema Ukraine imeretreat Soledar ni kipi? Hadi sasa sijaona. Ninachojua Urusi wameadvance kwa mara ya kwanza ndani ya miezi miwili. Hivyo mimi ninachopinga ni watu kuleta habari za upotoshaji ambazo hazijafanyiwa uhakiki. Bora mtu apost kama swali kuliko kuhitimisha kwamba tayari Soledar imechukuliwa wakati sio kweli. Tunawavunja moyo wanajeshi wetu.