Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

1. Naunga mkono hoja. Kwa plan hiyo watakufa sana bila ku-achieve chochote. Ukraine inatumia technology kujua adui amekaaje na yuko wapi' siyo ŕahisi kuwa-trap.

2. HIMARS au M270 ni machine hatari sana, laiti Russia wangekuwa na uwezo wa kuteka hata HIMARS au M270 moja tu, wangepiga propaganda sana.
Hata wakiteka, hawana makombora yake. Labda wapeleke Makumbusho. Hata software yake hawana
 
Yaani mara mia Mji Uchukuliwe kuliko vifaa vya jeshi kutekwa au kuteketezwa. Pia hali ya hewa imechangia.. Njia za Pori hazipitiki.

Mimi bado nawapongeza Ukraine sababu ukilinganisha nguvu ya Ukriane na Urusi, ni kama mara nne yake. But wanaweza wakazui mji usichukuliwe hata miezi 5.

Lazima kuwepo na mipango mikakati. Ungekuwa ni mji wa kuzui usichukuliwe ilikuwa ni Mariupol. Lakini Ukraine iliachia.. Tangu 2014 ni mara ya nne Ukraine inapoteza Mji wa Mariupol lakini baada ya muda unarudi. Hivyo kuna miji hata ikichukuliwa itarudi tu hata baada ya miaka 10. Mfano Odessa, Mariupol Bakhmut na hata Dnipro. Bado wafuasi wa Ukraine inabidi watambue sisi tunategemea nguvu za washirika kwani peke yetu hatuwezi. Pia jeshi la Ukriane limeiva.

Pia tuliamini jeshi la Ukraine. Kumbuka pia asilimia kubwa ya Vifaa vinavyo tumika sasa vingi ni vya Urusi wanatumia. Kuna sehemu Ukriane wanamudu then wanawaachia Urusi waingize vifaa vya Jeshi ili Wavizingire wapate Silaha na Risasi. Tumeiona ikifanyika Kherson na kharkiv. Silaha zilizotekwa zimetumika kuikomboa Izyum na Bakhmut hadi soledar na Sloviansk. Tuwapongeze wanajeshi wa Ukraine kwani bila wao hakuna wa kutupigania na hawana makosa.

Kila siku hatuwezi kushinda sisi tu.
Slava Ukraine [emoji1255]
Slava Ukraine [emoji1255]
Slava Ukraine [emoji1255]
 
Mkuu samahani, hii ya kuona uvivu kufuatilia ni wewe. Sisi wenzio tunafuatilia kuanzia Frontline hadi mipango ya Urusi na ile ya NATO.

Kuna majukumu lazima yaendelee. Sio kila siku utakuwa online kitegemea na Mazingira. Sio kila sehemu kuna intaneti pia kuna Uchovu. Mimi nipo na Ukraine hadi dakika ya mwisho wa piumzi yangu na nitaitetea Ukraine hadi tone la mwisho la damu yangu. Nimekushangaa unachoka kufuatilia. Vipi ungepewa mtutu? Ungeuza kambi na kusaliti. Timu inafanya vizuri unailaumu, vipi ikifanya vibaya? Soledar na Bakhmut ni sehemu ndogo sanaaaa....! Ingekuwa imechukuliwa mikoa mitano tungewaza lakini kuchukuliwa kata ituvunje moyo? Hapana. [emoji123]
Slava Ukraine [emoji1255]
 
Zingine ni propaganda. Mfano habari gani? Shukuru kwa kile ulichonacho. Wapi jeshi limepoteza ambapo ni Muhimu? Izyum ipo Ukraine vipi ingetekwa? Si ungelia kabisa? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Slava Ukraine [emoji1255]
 
Pia hata Ukraine wana propaganda sio kila kitu wanachosema ni sahihi. Mfano kombora lilitua Poland wakasema ni Urusi lakini ukweli ilikuwa ni Ukriane ndo maana iliisha kimya kimya. Sio kila habari napost hadi nijihakikishie kwani kuna connection ya watu wengi frontline japo washikaji wengi kama Dany na wengine nane walikufa kule Mariupol. Tangu wafe niliteteleka sana kupata habari sahihi. Ila sasa tupo sawa. Uliza swali. Mimi ni Timu Azov
Asante sana Kwa majibu mzuri .usife moyi endelea kutuletea updates
 
Hiki ndo kiwanda kinachotengeneza zile Shahed 136 zinazotusumbua kule Ukraine?.

Hii vita naona mdogomdogo inapanuka. Tusije tukaingia WW3
WW3 ni kugusa tu yaani chap maana hakuna anayetaka kurudi nyuma. wanamlainisha kwanza mrusi kabla ya kumvamia.
 
Hiki ndo kiwanda kinachotengeneza zile Shahed 136 zinazotusumbua kule Ukraine?.

Hii vita naona mdogomdogo inapanuka. Tusije tukaingia WW3
1. Huko hatuwezi kufika. USA, NATO na washirika wako extra care kwenye hilo.

2. Russia hana ubavu wa kupigana na mataifa haya makubwa. Yakipeleka vifaa vya NATO na askali wa NATO na USA, vita itaisha ndani ya mwezi tu Kremlin itakuwa imepigwa.

3. Russia ana washirika dhaifu in terms of military power. Ndo maana it is unlikely for WW3 to happen. Kama aliyekuwa anatamba kuwa ni super power ana kiwango kile, washirika wake wenye majina yanayoishi na ....stan, wana nini cha kutustaajabisha kwenye military.
 
Hiki ndo kiwanda kinachotengeneza zile Shahed 136 zinazotusumbua kule Ukraine?.

Hii vita naona mdogomdogo inapanuka. Tusije tukaingia WW3
1.Usipoziba ufa utajenga ukuta 2. Mwanzo wa ngoma ni lele
Kweli tuwe makini au waangalifu. Haka kamchezo kataifikisha dunia mahali pa baya.
Japokuwa sio rahisi kivile.
 
"Over the weekend, an Iranian military factory was hit by a drone attack that a US official said appeared to have been carried out by Israel. Israel has not commented."

Source: Aljazeera
A drone factory hit by a Drone attack - wonderful, amazing 💪 🔨🔨
The Drone Factory manager must know if it is one of his products. If not, then he/she should appreciate that the factory is producing inferior drones and somebody there has superior drones.
 
Back
Top Bottom