Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Urusi walikuwa wanatutisha eti kipindi cha baridi Ukraine itapigika. Mbona haipigiki sasa? Hadi sasa hakuna raia wa Ukraine kafa kwa baridi.. Eti oooh tutawakatia gesi mafuta na ujinga ujinga mwingi walikuwa wanaongea. Kwani Ukraine haina gesi? Haina mafuta? Hahahaaa[emoji1787][emoji1787]

Sasa wiki hii vifaa vya Urusi vimeshindwa kwenda Ukraine sababu wamekutana na barafu nyingi huko Urusi Mkoani Rostov. Nilijua Urusi wana mbingu yao ambayo barafu haiwasumbui
View attachment 2571603
Slava Ukraine [emoji1255]
 
FsnI0AqWAAAWwRU
 
SHUJAA ALIYEGUSA HISIA ZANGU
im-754977

Paraskoviya Demchuk akiwa ametembelea Kaburi la mwanawe Oleksandr Matsievskiy. Picha kwa hisani ya Wall Street Journal

Wakati mamluki wanaopigana upande wa Urusi walipotaka kumtisha Oleksandr Matsievskiy kwa kifo, wenyewe waliambulia kukerwa na Oleksandr. Oleksandr alielewa kwamba wale mamluki ni watu wabaya sana na hakuwa na haja ya kujipendekeza kwao. Yeye alikuwa anapigania nchi yake wakate wale mamluki wengi wao wakiwa ni majambazi,wauza madawa ya kulevya na waliokuwa wamehukumiwa kifo toka kwenye magereza ya Urusi, walikuwa wanapigana ili waachiliwe huru au walipwe kwa kuua waukraine.

Oleksandr akiwa na uthabiti wa moyo alisema "Slava Ukraini!" na bila shaka malaika Mbinguni nao waliitkia "Heroiam slava!" wakati wakiipokea roho yake shujaa huyu wa Ukraine. Uzalendo na ushujaa ni kusimamia kile unachokiamini hata wakati wa mauti ikikukaribia mikononi mwa maadui zako.
 
Hawa Warusi waliambiwa Wajisalimishe wakakataa. Bila kujua wanainwa na drone. Ikabidi Mwanajeshi wa Ukraine kwa kusaidiwa na wanaocontrol drone wakamuelekeza walipo akawamaliza
 
Back
Top Bottom