Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

20230623_080408.jpg
 
Wanajeshi wa Ukriane wamepata Bonus baada ya kitoweo kujiingiza kwenye kifaru kilipokuwa kinakatiza mto
 
Urusi kazi wanayo. Sasa vita ipo Nchini mwake. Ukraine itaisambaratisha Urusi na itabaki vipande
 
Imedaiwa eti, Wagners watatumika kumtoa Madarakani Putin. Wenye hela zao washapanda dau. Last time kama mnakumbuka, Wagners waliomba ushirikiano na Marekani.
 
Moscow jana kulizuka taharuki ya kikosi Maalum kuvamia Moscow, ikabidi wakate internet na barabara zote zinazoingia mjini zikafungwa na Vifaru. Putin kaanza kutetemeka. Sasa atapigana vita ya Ukraine na Vita ya kubaki madarakani
 
Angalizo. Prigozny Yevgeny si mtu wa kuaminika, analosema na analolifanya huwa vinakinzana.
 
PMC Wagners wamelalamikia Jeshi la Urusi kwa kushambulia kambi yao kwa missiles. Wanadai wamefanya makisudi. Na Wagners nao wamelipiza kisasi kwa kutungua Helkopta mbili za kivita za Urusi. Hii ni Kambi ya PMC Wagners iloshambuliwa na Urusi
 
Msururu wa Magari ya kijeshi ya Wagners yakiwa Mkoani Voronezh huko Urusi yakiwa yanaelekea uelekeo wa Moscow. Kuna tetesi eti Putin anataka kutangaza Operation nyingine ya Kuilinda Urusi. Sasa zimekuwa operation mbili. Ya kuvamia Ukriane na nyingine kujilinda🤣🤣🤣
 
Wagners wakiwa wanaingia mjini Rostov huko Urusi. Hawa hawataki Serikali iliyopo madarakani Urusi. Hawa wataungana na The Freedom of Russia Legion. Kama ikiwa hivyo basi Urusi ajipange upya
 
Hapa si Ukraine bali ni Mkoani Rostov huko Urusi. Warusi. Hatimaye na Warusi leo wamekunywa chai yenye harufu ya risasi😂😂😂. Wakome
 
Hapa ni Urusi kila mtu kakunja ngumi. Nasubiri mtifuano. Uzuri kila upande una siraha za kutosha
 
Back
Top Bottom