SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Jeshi la Iran:
Israel waondoe watu haraka kwenye kituo cha kinyuklia Dimona maana wana jambo lao hapo muda wowote.

Wakati huohuo Bado US anasita hana uhakika kama B2 bomber hata KWA kutumia Satan 2 missile wanaweza kuharibu mitambo ya nuclear ya Iran chini ya Ardhi.

Russia anasema chini ya ardhi huko Kuna wanasayansi wake wa Nyuklia na haiwatoi.


Ni hayo tu
 
Hawana cha kufanya kwanza nchi kama uae, quatar na nyingine zilizoendelea haziwezi hatarisha miundombinu ambayo wamejenga kwa miaka mingi kisa ujinga wa Iran, tena zinaweza toa msaada kupambana na Utawala wa Iran hutaamin
Nikisema wewe huna unalojua unaanza kubisha.
Nchi ulizotaja UAE na Qatar ni SUNNI kiitikadi.
Mimi nazungumzia nchi SHIA kiitikadi.
Yemeni,Lebanon ni shia kiitikadi.
Zipo nchi nyingine hapo mid east shia kiitikadi.
Usikurupuke kujibu pasi na kusoma.
 
Mkuu hauwezi kuzuia surface to surface missile labda uharibu launcher zote zilizopo aridhini

Kilichotokea Gaza ni kwamba Israel ilihakikisha inaharibu launcher kuondoa uwezo wa kurusha hizo roketi...... na hichi ndio kitu Israel inajaribu kufanya pale Iran

Inaposemwa anga la Iran kivita limetawaliwa na Israel ina maanisha kwamba kwa kiasi kikubwa mifumo ya kiulinzi ya Iran imeharibiwa na kufanya Israel kulitumia anga itakavyo tena kwa kutumia ndege

Missile za Iran zitaendelea kurushwa as long as missile launcher zikiwepo.....
Mnajisahau kuwa hata drone za shahed zinaruka kutoka Iran kwenda Israel.
Unataka kunambia drone pia sio rahisi kuzuiliwa?
Sijui mtadanganya kwa lipi.
 
Jeshi la Iran:
Israel waondoe watu haraka kwenye kituo cha kinyuklia Dimona maana wana jambo lao hapo muda wowote.

Wakati huohuo Bado US anasita hana uhakika kama B2 bomber hata KWA kutumia Satan 2 missile wanaweza kuharibu mitambo ya nuclear ya Iran chini ya Ardhi.

Russia anasema chini ya ardhi kuho Kuna wanasayansi wake wa Nyuklia na haiwatoi.


Ni hayo tu
Ohoooo
 
Mkuu ubishe usibishe Israel ipo taabani.
Kitendo hadi cha raia kuanza kukimbia nchi hiyo inaonesha Israel iko taabani.
Vita ya Hamas Israel walikua bado wako imara ndio maana raia walioamua kuondoka ni wachache.
Ila vita hii ya Iran hakuna sehemu salama Israel kiasi malaki ya raia wanahama nchi.
Tubishe tusibishe Israel iko taabani.
Mkuu samahani raia wanakimbia nchi kivipi? Unasema Malaki ya raia wanahama nchi??

Hizi ndio hisia. Hata mtu akisema maelfu ya Wana Iran wanahama nchi nae atakua kaweka tu hisia.
Kuhama nchi hufanywa na wenye uwezo mkubwa tu na pia endapo nchi imevamiwa.

Tatizo mnachagua kusema like ambacho mnakitamani, hili tatizo litawasumbua sababu litakua halifikii matarajio yako ya ukweli.
 
Mnajisahau kuwa hata drone za shahed zinaruka kutoka Iran kwenda Israel.
Unataka kunambia drone pia sio rahisi kuzuiliwa?
Sijui mtadanganya kwa lipi.
Drone zinatumwa na pia zinakua intercepted, drone ni rahisi kutunguliwa ndio maana hazifiki hata mbali zikiwa tu mipakani zinatunguliwa. Labda zirushwe wakowa ndani ya hiyo nchi
 
Huu mgogoro hauishi salama. Sure, Israel watafanikisha azma yao, watalipua na kuangamiza viwanda vya kutengeneza silaha za nuklia. Waneweza kuumua hadi ayatollah, hilo liko ndani ya uwezo wao. Iran imeonekana kuwa highly disorganized hata kuliko vikundi vya kigaidi ambavyo Israel amepigana navyo siku za hivi karibuni.

Lakin sasa, what hapoens next ndo mtihani mkubwa. Iran ni taifa kubwa lenye raia takribani milioni 100. Kukosa uongozi kwa jamii yake inayotofautiana itikadi za kidini na tamaduni ni mtihani sana. Shida wameishi under control ya regime ya hawa ayatollahs kwa miaka kibao, they don't know amani ni nine and how to practice one. Uhuru utaibua magaidi na wale wanaotaka amani wataibuka kutetea mwelekeo sahihi. Kufikia makubaliano ni ngumu sana. Angalia kilichotokea Libya. Hadi Leo ni taharuki tupu ingawa wana Imani moja ya kidini, sembuse Irani yenye mchanganyiko wa kila jamii!
Mda utaongea
 
Mkuu samahani raia wanakimbia nchi kivipi? Unasema Malaki ya raia wanahama nchi??

Hizi ndio hisia. Hata mtu akisema maelfu ya Wana Iran wanahama nchi nae atakua kaweka tu hisia.
Kuhama nchi hufanywa na wenye uwezo mkubwa tu na pia endapo nchi imevamiwa.

Tatizo mnachagua kusema like ambacho mnakitamani, hili tatizo litawasumbua sababu litakua halifikii matarajio yako ya ukweli.
Uliliona tangazo la waziri wa usafirishaji wa Israel?
Aliongea live alisema serikali isiruhusu raia yeyote wa Israel kutoka nchini.
Wanaoruhusiwa kutoka ni raia wa kigeni na diplomats wa kigeni.
Kaa fikiria hii inaashiria nini.
Vita ya Hamas imewaohamisha raia million Moja na robo wa Israel.
Hii imeonesha raia wengi zaidi ya vita ya Hamas wanataka kuondoka.
Na hao walioondoka kipindi cha vita ya Hamas ni laki tatu tu ndio wamerudi.
 
Mkuu samahani raia wanakimbia nchi kivipi? Unasema Malaki ya raia wanahama nchi??

Hizi ndio hisia. Hata mtu akisema maelfu ya Wana Iran wanahama nchi nae atakua kaweka tu hisia.
Kuhama nchi hufanywa na wenye uwezo mkubwa tu na pia endapo nchi imevamiwa.

Tatizo mnachagua kusema like ambacho mnakitamani, hili tatizo litawasumbua sababu litakua halifikii matarajio yako ya ukweli.
Iran wanahama mji sio nchi, ni kweli Israel raia wanakimbia wengine wanapanda boat kwenda Cyprusus, nauli mwanzoni kwa boat ilikuwa $20 hivi sasa ni $5000..
 
Mnajisahau kuwa hata drone za shahed zinaruka kutoka Iran kwenda Israel.
Unataka kunambia drone pia sio rahisi kuzuiliwa?
Sijui mtadanganya kwa lipi.
Mkuu tuna maanisha anga la Iran lipo UCHI

At anytime Zina ingia ndege zaidi ya 100 zinapiga zinapotaka na zinatoka salama salmini

Hatumaanishi Iran hawezi kufanya chochote ndani ya Iran

Iran bado ana struggle na ANGA la Israel kwasababu sio makombora yote yanatua na drone karibu zote zinaangushwa njiani...... vinginevyo Israel ingekua kama Gaza
 
Jeshi la Iran:
Israel waondoe watu haraka kwenye kituo cha kinyuklia Dimona maana wana jambo lao hapo muda wowote.

Wakati huohuo Bado US anasita hana uhakika kama B2 bomber hata KWA kutumia Satan 2 missile wanaweza kuharibu mitambo ya nuclear ya Iran chini ya Ardhi.

Russia anasema chini ya ardhi huko Kuna wanasayansi wake wa Nyuklia na haiwatoi.


Ni hayo tu
Netapaka aliwaza nini kuchokonoa mzinga kwa mkono? 🤔
 
Kuna mtu anaweza kunambia uhusiano gani wa kindugu, kisiasa, kitamaduni, kijamii, kijeshi au wa aina ina yoyote ule alionao Israel na mataifa makubwa ya Ulaya na US?

Yaani ukimgusa Israel kidogo tu ni kama umekanyaga kende za USA na washirika wake.
NB. Asitokee mtu akanambia wanasyansi wa Israel ndio wanaoiongoza USA na upuuzi kama huo.
 
Back
Top Bottom