SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Sawa..lakini ukiishia hapo na kuhitimisha unajilimit na inakua sio critical thinking tena.
Maswali bado mengi..je yalirushwa kutoka umbali gani,je uwezo wake kwenda chini ni upi,je hicho kituo kilikua umbali gani kwenda chini,je blast yake inakua na imbact kwa circumference ipi likipigwa kwenye majabali..je walilenga focal point?ke kulikua na uranium huko ndani kwa muda huo wanaolenga???

Haya maswali yooote majibu tunayapata kutokana na impact iliyokua reported..hadi leo utasikia huyu anasema kituo hakikuharibika sana..mwingine anasema kiliharobika kwa kiasi kinachorekebishika kwa miezi kadhaa tu..mwingine anasema miaka kadhaa..mwingine anasema hawakulenga shabaha sahihi..mwingine anasema impact ni physical damage kwenye vifaa vichache sana visivyo na madhara..hawa wooooote ni upande wa west ndo wanasema

Upande wa iran wao wanasema kuna impact inayorekebishika ndani ya kiezi kadhaa na hapakua na enriched uranium maana ilishahamishwa.

Sasa hapo unaona upande mmoja una majibu mengi upande mwingine una jibu moja

Upande wa west hauna ushahidi wowote wa kusupport hata kwa experience ya mahali pengine ambako hua panaharibiwa kua kuna madhara ya wazi lakini hapa tunapata maswali kwa nini hapana madhara ya waziii??kwa nini ni hapo tu ndio pasiwe na chemical impacts zozote??

Ndio maana wengi tunaishia kuamini kua ni kweli pamepigwa hili liko wazi kila upande unakubali..lakini impact yake haikua iliyokusudiwa na huenda uharibifu haukua mkubwa kiasi hicho ndio maana Israel wanapanga kurudi tena.
Sawa mkuu ngoja tusubiri
 
Mkuu..
West wanahangaika sana na kulazimisha kuionyesha dunia uwezo wa ndege zake za B-2..
Hata migodini ambapo huwa wanalipua miamba, ukilipua mwamba ukalipuka kama njia inatafutwa lazima mtafika eneo husika na kutoa vipande vilivyolipuka.. ili kutengeneza njia ya kuweka vilipuzi tena ili kuzidi kulipua...

Ukilipua mwamba vipande vya miamba vitarudi pale pale, inakuwa ni kama vimeziba tena njia, unakuwa unatwanga maji kwenye kinu..
Iran vinu vyake vimejengwa makusudi sehemu ambako kuna miamba migumu kwa maana walifahamu siku moja suala kama hili litatokea...

Ili shambulizi lile kufanikiwa zaidi baada ya kupiga bomu ilipaswa waondoe vipande vya miamba halafu waachie tena bunker buster tena na tena kwa kurudia zoezi... kitu ambacho huo muda haukuwepo...

Kama bunker buster ingefumua vizuri hivyo vinu, na centrifuge zingeharibiwa, lile vumbi likichangnayikana na uranium ambayo ingetoka kama gas ingesambaa hewani na kwenye udongo.. hivyo raia wangeambiwa waondoke haraka maeneo yale... maana uranium ni kitu hatari sana..

Yaani hivi sasa tungeona wale jamaa ambao huwa wanavaa nguo kama wapo kwenye space/protective suits wapo maeneo yale namashine zao wakipima na kufanya shughuli zingine...
Mkuu tatizo nalolionaga kwenda hizi mijadala ya hii vita ni watu mnaweka sana hisia
 
Mkuu tatizo nalolionaga kwenda hizi mijadala ya hii vita ni watu mnaweka sana hisia
Tatizo ni kutokujibu kwa facts, huwezi kuja kuniambia kwamba farasi anapaa, lazima nitakuuliza mbona hana mbawa? kuna mambo mengine lazima mtu uhoji maana habari hazileti uhalisia kabisa.. only way ya kuthibitisha ni kuelezea kitaalamu na kwa uthibitisho...
 
Polite reminder!!! Hao ndiyo mbwa unaowaona wana maana, lakini kwao wewe ni just another Goyim if you know what I mean. Hawa merciless, most racist people the World has ever known.
Unapochanganya lugha unataka tukuelewe wewe umesoma sana au tukuelewe wewe kiswahili hujui? Ongea kwa lugha unayoijua ili tukuelewe vizuri kama kiingereza Annika chote kama kiswahili andika Kiswahili ueleweke!!

Ulichoandika hapo unanijua wewe mwenyewe tu!!
 
Sawa sawa...
Russia sio wa kuwaamini sana wakati huu..
Kuna habari nilielezea humu zamani sana kuhusu Russia walivyopiga dili na Israel mwaka 2007/2006, Russia aliwauzia codes Israel za s300 zilizokuwepo Syria na Israel akamuuzia codes za drone za Israel zilizokuwa zinatumiwa na Georgia 🇬🇪 kuishambulia Russia...

Yaani Russia alikuwa anapambana na Georgia huku Israel akipambana na Syria, hivyo wakapiga deal, Israel ikawa inaingia Syria kama sebuleni kwake pasipo s300 kufanya lolote, huku Russia akiwa anaziteremsha drones za Georgia...

Georgia wakastuka wanachezewa, Syria na wao wakaomba msaada Iran, Iran ikapeleka engineers wa air defense systems hadi Damascus, wale engineers wakabadili codes za s300 na kuifanyia settings upya kabisa ndipo s300 zikaanza kuona ndege vita za Israel, lakini mwanzoni zilikuwa zinatambua ni friendly plane..

Huku Georgia na yeye akaenda Mexico akiwaomba wampe drones ambazo zilikuwa konki kuliko zile za Israel ambazo Russia alikuwa anazibutua hovyo kwa sababu amepewa codes zake na Israel watengenezaji wenyewe...

Mexico ilikataa kwa kuhofia kuingia kwenye ugomvi na Israel, Georgia ilibidi wauze zile drones kwa nchi moja sikumbuki vyema itakuwa Kazakhstan...

Lengo la kusema hivi, ni kama Iran haiamini Russia 100%, kwa maana kwa hii vita ya Ukraine, Russia aaweza kufanya tena kama hayo yaliyotokea 2007... maana Russia sasa anaweza kurubuniwa kupewa codes za silaha za west zilizopo Ukraine ili nae aiuze Iran..

Ndio maana kama umeusoma mchezo, Iran inatoa kauli za kishujaa kwamba wao wapo vizuri bado hawajahitaji msaada, sio kwamba hawapendi ila kuchezeana nahisi kumo...

Hio issue ipo chini sana watu wengi hawaijui, mtu yeyote atafute hio habari hata youtube haipo, hata wikipedia haipo, hio niliisoma kwenye leaked documents za wikileaks... nilikuwa nasoma email ni kama agents fulani walikuwa wakipeana hio siri..

Kama umeusoma mchezo utagundua ni kama Iran anakuwa mzito kuiomba Russia msaada wa ADs n.k, hadi siku ile Putin alisema, tuliwauliza Iran kama watahitaji msaada wetu wakasema hapana... haya mambo yanatisha sana..
Hata hivyo hata wasingezikubali maana zilifeli mwaka Jana kulinda Khomeini airport.
 
Za Iran zilikua Khordak-15 na Bavar-373,s300 zilifeli mwaka Jana zilipokua zinazuia shambulizi la Israel la ndege kwa Iran.
Kwa China naamini silaha zao nzuri hawawezi kumuangusha mtu wamethibisha hilo kwa Pakistan.

Sio tu Iran hata EU na USA hawakuamini namna Iran alivyo advance katika jeshi.
Walidhani Iran hii ni kama Iran Ile ya 1980s.
Israel haijioni salama tena lazima tuu ahangaike kumuangusha Iran.
Pale unapopambana kumuangusha mtu aliyekuzidi matokeo yake unapotea ww . Vita ya gaza imemaliza resilimali zote za maana za israel na za washirika wake .. halafu unaenda kuazzisha tena vita vingine vigumu
 
Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa Rais Masoud Pezeshkian alijeruhiwa kidogo katika shambulio la anga la Israel asubuhi ya tatu ya Operesheni Rising lion. Ndege za kivita za Israel zilizoripotiwa kulenga ngome ya chinichini ni Pezeshkian na Spika wa Bunge la Iran alikuwa amekimbilia pamoja na maafisa wengine wakuu wa serikali.
 

Attachments

  • IMG_3646.jpeg
    IMG_3646.jpeg
    72.4 KB · Views: 21
Dunia sio sehemu nzuri tena ya kuishi ni vile Binadamu hana chaguo la kuzalliwa au kubaki huko huko alipo.
 
💥
Ndege ze uchunguzi na drones za jeshi la marekani zinazunguka kufanya uchunguzi/upelelezi eneo la ghuba ya uajemi kwa zaidi ya masaa matano sasa
 
Back
Top Bottom