Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

😃😃😃😃
Aisee. Sasa gesi itarudi kuuzwa kwa dola? 😁😁
 
Does not mean...
Hii kauli njema sana
Waendelee kupeleka moto hao RAIA WEMA wakiondoka
 
Russia wameshindwa kuipindua serikali halali ya Ukraine pamoja na uwepo wa hizo S-400 air defence systems na matokeo yake wamepoteza maaskari wengi na silaha kibau.
We na wewe em sumbua ubongo kidogo ....rashia hana shida na kuipindua serikali ...ingekuwa inataka kufanya hivo wangeshamuua zelensky kitambo tu.....rashia anachokitaka kwa ukraine ni mashart aloweka rashia mezani yafanyike ...yaaki zelensky na selikali yake watii kile russia anachokitaka na ndo maana wamekubali hawatajiunga na nato wala hawatakuwa na silaha za nyuklia na kuna majimbo mawili yanatakiwa yawe huru ....
 
Russia wameshindwa kuipindua serikali halali ya Ukraine pamoja na uwepo wa hizo S-400 air defence systems na matokeo yake wamepoteza maaskari wengi na silaha kibau.
Sawaaa...

Haya tueleze pisi 250 za S-300 air-defense systems zilizokuwepo Ukraine kabla ya vita kuanza zilienda wapi? Hadi kufikia Zelensky anampigia magoti Biden na kumuomba walau ampatie pisi moja tu ya S-300 (wakati tayari alikuwa na pisi 250!)!




 
It is simple,yeye ndio kamuweka Putin kwenye hiyo nafasi-ukisoma historia ya maisha ya Putin kufika hapo ni sababu ya Abromvich.Ukraine wanajua fika MTU wa mwisho ambaye Putin anaweza msikiliza Urusi nzima ni jamaa.
 
Kaka asante kwa salamu zako kutoka Abunuwasi!!
Kumbe Putin hakutaka kuchukua Kiev, hii ni sababu alikusanya jeshi kubwa ndani ya Belarus (iliyo karibu na Kiev) na kutuma maelfu ya magari na vifaru na askari kuelekea Kiev, akajaribu kuviringisha Kiev na kupoteza maelfu ya vijana wake.
Putin kutolenga Kiev ilikuwa pia sababu ya kuona foleni ya vifaru na magari ya kilomita 60 iliyokwama umbali mdogo mbele ya Kiev kwenye barabara kutoka Prybirsk na kuharibika pale.
Bila shaka vifaru hivi vilipotea njia tu katika nchi ya kigeni, hawakutaka kuelekea Kiev!
Sema kaka, ni vigumu sana kujidanganya?
 
sasa manmbo yakiisha namna hii nani anakuwa mshindi wa siatuation nzima?? je makubaliano haya ni kwamba ukraine atakamilisha ndoto nyingine ya kujiunga EU baada ya nato kuota mbawa, je waukrane na urusi ule undugu aliosema putin utaendelea au ndio unaishia hapa?
 
It is simple,yeye ndio kamuweka Putin kwenye hiyo nafasi-ukisoma historia ya maisha ya Putin kufika hapo ni sababu ya Abromvich.Ukraine wanajua fika MTU wa mwisho ambaye Putin anaweza msikiliza Urusi nzima ni jamaa.
mkuu Berezovsky ndie alieinjinia kumuweka putin FSB then baada ya moto wake huko ndio wakaona wamuweke PM then urais, abromovich alikua bado bw mdg kwa Boris, sema Boris alipoznguana na putin baadae ndio abromovich akamzd mwalimu wake
 
Nahofia undugu utasitishwa kwa miaka mingi. Putin amefaulu kujenga chuki. Sioni bado washindi. Ukraine imepoteza watu wengi na mali nyingi. Urusi imepoteza askari wengi pia. Vikwazo havitakwisha, na mataifa ya Ulaya yataendelea kupunguza ununuzi wa gesi na mafuta kutoka Urusi (kama biashara hiyo haisimamishwa sasa shauri ya fitina kuhusi namna ya malipo). Uchumi wa Urusi utaendelea kushuka chini.
Mataifa ya Ulaya yataona matatizo pia.
Sijui kama tunaona tayari mwisho wa mapigano.
Inawezekana Putin anacheza tu hadi anaweza kupeleka wanajeshi wapya kwenye medani?
 
niliposoma marengo badala ya Malengo nikaacha kusoma gazeti lako all in all jifunze kuandika kiswahili vizuri
ngoja nipate muda nitasoma hili gazeti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…