LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Israeli ina fanya surgical operations ndani ya iran kila siku hao urusi hawawezi wana uwa raia wasio na hatia
 
IMG_4826.jpg
 
kama rais, msimamo wowote unaouchukua unatakiwa kuupima kuona kama utaumiza raia wako au la. kujifanya yeye ni mjasiri wakati raia wanaumia kwasababu ya maamuzi yake sio busara. Ukrain ni nchi huru yenye maamuzi yake lakini kwenye kuamua ni busara kuamua kwa kupima mizani watoto wako wasiume au kufa. wakifa huwezi kuwafufua. na wanaweza kufa pasi na sababu ya msingi, unaingia vitani ukijua utashindwa tu, na unayo nafasi kuzuia, kwanini usichukue hatua mahsusi?
yaan wewe unabariki taifa lingine kulipangia taifa lililo huru kipi cha kufanya na kipi cha kutokufanya,
mfano leo wewe nini raisi wa tanzania
akatokea jiran yetu yeyoto ambae ana nguvu kukushinda,
akaja na masharti yake kuwa
anataka wanaume wawe mashoga, je wewe kama rais utakubaliana nae kwa sababu huyu jiran yako uwezo wa kukupga anao,
au utaamua kufa kiume,
 
point ni kwamba, wamagharibi wanajua kabisa ukrain mwisho wa siku atapigwa na wamejiandaa kumsaidia kujenga upya nchi. sasa, kama wanajua ukrain hatashinda kwanini wanamtumia kupigana na urusi? raia wake wanakufa wakati raia wa wamagaribi hawafi, wanajeshi wake wanakufa wakati wanajeshi wa magharibi hawafi, kinu cha nuklia kimeshatwaliwa na urusi wakati vinu vya nuke vya wamagharibi vipo salama. lengo la urusi ni kusambaratisha uwezo wa kijeshi na tayari ameharibu zaidi ya vituo vya jesho 200 hadi sasa. ungekuwa wewe ni ukrain ungekubali huu uchizi? au kwasababu unajua at the end of the day utashindwa tu vita bora ufupishe maelezo kwa kukaa mezani mjadili kwa faida ya raia wako na miundombinu yako? sasaivi kuna mwekezaji gani atawekeza ukrain ambako man power imekimbilia nchi zingine, na hana uhakika kama urusi itarudi tena anytime soon? uchumi wao labda tuseme walijikita zaidi kwenye kilimio cha ngano, wanalima nini sasa? au wanapokimbia wamekimbia pamoja na magunia ya ngano? na wamagaribi watakaposaidia kuijenga baada ya kuwa magofu, je? watakuwa wanagawa pesa mifukoni? au mtu hadi apate kazi za kuwa kibarua wa ujenzi ndio azipate izo pesa wakati pengine alikuwa msomi wa white colour job na alikuwa na biashara zake zinaenda vizuri. biashara za watu zitasimamaje? watapewa mitaji? ukrain wameshaumia sana, hata kama kuna ahadi ya kuijenga ni kujenga tu ila raia wanaanza chini kabisa, na wengine wengi wameshakufa ambao hawatafufua. na urusi ameshakalia vituo vyao vya kijeshi walichobaki wao ni kuhamia mitaani kurushiana risasi, jambo ambalo hatawapa tena nafasi kujijenga kijeshi. why all this wakati kulikuwa na nafasi kuyaepuka?
Mkuu na wewe una ushabiki mwingi sana kuliko uhalisia,unaandika maneno mengi lakini unarudia mambo yale yale ambayo tangu uemanza kujibizana na Tsh keshakujibu zaidi ya mara kumi,nachokiona hapa wewe ni hodari wa kuandika comment ndefu zilizojaa kile unachofikiria na unapenda kiwe kulingana na matakwa yako.
 
Wafuasi wa udikteta na mauaji Tanzania wanateseka sana. Wakati Warusi wenyewe wanampinga gaidi Put-in na genge lake, kuna Warusi wa Tanzania wanamuunga mkono!!!

Jana vyombo vya habari na mitandao ya kijamii Urusi imepigwa pini na Put-in ili Warusi wasifuatilie kwa karibu ujinga unaotekelezwa kule Ukraine 🙄 Ni aibu!
 
Wamepiga U-turn baada ya kugoma kwa muda mrefu kupeleka silaha! Zile kofia ngumu zipatazo 5000 zilipelekwa siku ya pili baada ya kuanza kwa mapigano.
Watu walilaani sana maana Ukraine alitaka kofia 100K yeye akapeleka 5K
 
Kuyaepuka kwa kufuata matakwa ya Russia ambayo si matakwa ya Eukraine? Hapa swali linakuja, Eukraine ni nchi inayotakiwa kufuata matakwa ya Russia tu? Au ina misimamo yake?
Mkuu naona umeamua kwenda nae sambamba, na una press the right button
 
Eukraine imekataa kufuata matakwa ya Russia. Raia wake wapo na raisi wao. Jeshi lipo na raisi wake. Hujasikia maandamano ya raia kupinga kutokumsikiliza Russia kuepusha vita, badala yake umesikia wakijiandaa kwa lolote. Russia imeamua kuivamia nchi huru. Wameamua kulinda nchi yao. Hawana makosa.
Sababu Media ndio agenda yao huko East of Ukraine Russia wana support kubwa sana na ukumbuke upinzani ulianza siku nyingi huko sisi tutaona wanachotaka tuone tu wala hawa report ukweli wewe nchi kama wanavyotaka tuamini jeshi lao liko vizuri sasa wanagawa silaha kama njugu tujilinde unawapa watu AK 47 hizo ndio watazuia ma Tanks? si kama kujinyonga tu. Na sisi wa Africa tuache unafiki kidogo kujifanya inatuuma sana na hao wa Ukraine toka lini hao west walijali maisha ya wengine ila sababu mambo yako kwao basi Media zote wamejaa huko na kutu brain wash maana vitua vya habari hawa report uhalisia ila wanatuambia maoni yao.
 
kama rais, msimamo wowote unaouchukua unatakiwa kuupima kuona kama utaumiza raia wako au la. kujifanya yeye ni mjasiri wakati raia wanaumia kwasababu ya maamuzi yake sio busara. Ukrain ni nchi huru yenye maamuzi yake lakini kwenye kuamua ni busara kuamua kwa kupima mizani watoto wako wasiume au kufa. wakifa huwezi kuwafufua. na wanaweza kufa pasi na sababu ya msingi, unaingia vitani ukijua utashindwa tu, na unayo nafasi kuzuia, kwanini usichukue hatua mahsusi?
Mkuu kwa huu msimamo wako,ingekuwa una ndoto za kuwa kiongozi,hata kuongoza kitongoji hutakiwi kuwa kiongozi.Kwa hiyo kina Kiduku wanavyokuwaga wanasimamia maslahi ya Nchi zao huwa ni wajinga? Yani umwache tu jirani yako aje alale mpaka kitandani kwako na mkeo kisa unapima madhara ya kupambana nae yatakuwa makubwa zaidi kuliko maslahi ya Ndoa yako?
 
Back
Top Bottom