Wataalamu wa mambo ya nuclear kwa utaalamu wao wanatuambia nuclear ni hatari wewe ambaye hatujui kama una utaalamu wowote kwenye mambo hayo unapinga! Ajabu!!!
Unapinga tafiti za kitaalamu kwa kutumia hisia zako mkuu.
Bw. Alex wellerstein mtaalamu wa masuala ya nuclear (Nuclear Historian) ametengeneza website ya 'Nukemap' inayoweza kuruhusu mtumiaji adondoshe bomu fulani la nyuklia kwenye mji fulani ili aweze kujionea mwenyewe madhara yanaweza kuwaje kuanzia vifo, majerui, uharibifu wa majengo/miundombinu/mazingira, madhara ya mionzi, fallouts nk. Unaweza mwenyewe kuingia hapo ujionee. Bomu dogo la kt 140 lililojaribiwa na NK 2017 linaweza kuathiri eneo la ukubwa wa mile za mraba 134 na kuua na kujeruhi zaidi ya watu 700k
Na kinachotishia zaidi kuhusu vita vya nyuklia wala hata sio milipuko yenyewe hasa bali ni madhara ya muda mrefu ambayo huja baadae vikishapiganwa vita vya Nuclear. Wataalamu wa masuala ya nyuklia na wanasayansi mbalimbali wametafiti kuhusu hili na wamekuja na majibu kadhaa wa kadhaa.
Mfano. Profesa wa mazingira wa chuo cha rutgers bwana alan robock ametafiti kuhusu yanayoweza kuwa madhara ya muda mrefu ya 'vita vya nyuklia' duniani kwa kuzingatia models tofauti za uchumi, sayansi na agriculture.
Miji na majiji yaliyoathirika na vita vya nyuklia kwa kuunguzwa yatasababisha moshi mweusi ambao unaweza kupanda mpaka kwenye level ya stratosphere na kuathiri kiwango cha joto na mvua duniani. Tani milioni 5 mpaka 50 ya huu moshi utaleta kitu wanaita 'nuclear autumn' na ikiwa ni tani milioni 50 mpaka 150 basi 'nuclear winter'.
Nuclear Autumn
Pakistani na India (ambao hawana idadi kubwa ya silaha za nyuklia) endapo kutazuka vita vya nyuklia baina yao wanaweza kupelekea nuclear autumn. Km kila mmoja akimpiga mwenzake na mabomu at list 50 ya size ya yale ya hiroshima basi moshi mweuisi unaotokana na kuungua vitu na miji unakadiriwa kufikia tani milioni 5 mpaka 6. Huu moshi ukifika juu unazuia miale ya jua kufika duniani kwa kiasi kikubwa baadae inapelekea kushuka kwa joto na hivyo less precipitation. Ndani ya miaka mi5 ya kwanza itaathiri zaidi ya 40% ya kilimo duniani kote na kufikia miaka 10 joto duniani litashuka zaidi na kufikia level ya chini zaidi kuwahi kushuhudiwa ndani ya miaka 1000 ilopita.
Watu bilioni 2 wanaweza kufa kwa njaa. Imagine hiyo ni vita tu dhidi ya Pakistani na India kama ikihusisha nuclear.
A. Ward kutoka mtandaoni
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app