Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Sberbank said that due to sanctions, it stopped foreign currency transfers abroad, while transfers abroad in rubles are still available.
Galip SV View attachment 2180572
Unyama unyamani [emoji3][emoji3][emoji3]
Huu mgogoro ukiisha kuna majambo mengi sana yatakua yamebadilika
PUT IN tafadhali kamatia hapo hapo ulipokamatia mwisho tutajua nani ninani nanani ninani
TWENDENI NA RUBO
 
IMEKUWA ROCKET YA URUSI TENA Galip SV
20220408_164249.png
 
Nuclear ni habari nyingine kbs. Na mungu nae anasaidia

Kuna stori ya mwamba mmoja inanifikirishaga kidg ni ya kusisimua pia.

Stanislav Petrov cheo chake alikuwa lt. Col. Akiwa afisa wa zamu kwenye kituo cha kamandi ya mfumo wa kutoa tahadhari za awali za (mashambulizi ya) nyuklia wa (OKO nuclear early warning system). Hiyo siku mfumo huu wa OKO ulileta shida kidogo (malfunction) na kutoa taarifa ya makosa kuwa kuna kombora 5 za nyuklia zipo njiani kushambulia USSR kutokea marekani. Huyu bwana akiwa kama afisa in charge wa mfumo huo kwa kutumia sijui ndio tuseme hekima yake hakureport kwa wakubwa zake kuwa nchi yao ipo kwenye mashambulizi ya nyuklia kutoka marekani kwa kuwa aliamua kuwa ile ilikiwa ni tahadhari ya kimakosa. Laiti kama angelitoa taarifa ya tahadhari hiyo hapohapo USSR wangelaunch nao retaliatory strikes dhidi ya NATO na US kitendo ambacho kingepelekea vita vya nyuklia.
Baadae wasovieti walikuja kugundua kweli kulikuwa na shida kwenye mfumo wao na huyu jamaa akawa kasave dunia na vita mbaya ingeyoweza kutokea

Kuna mahali nilisoma makala flani wanasayansi mbalimbali wa mambo ya nyuklia wanaelezea madhara ya vita vya nyuklia yanavyoweza kuwa nikahitimisha hata Urusi leo aipige nchi yoyote mwanachama wa NATO au US aipige urusi popote au aingize jeshi lake Ukr kupambana na urusi vyovyote itavyokuwa hakuna atakayekuwa tayari kuanzisha vita vya nyuklia. Madhara yake ni makubwa sana na pengine ikawa ndio mwisho wa ustaarabu au uhai wa binadamu duniani.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Nuclear ni hatari sana kweli lakini sio kwa kiwango hicho , vinginevyo hakuna taifa lingekubali kuwa nazo. Narudià kusema kwamba Nuclear zina madhara makubwa sana lakini sio kwa kiwango kinachozungumziwa. Ni kama ilivyokuwa inazungumzwa kuwa Russia inatisha sana na baada yakuingiza majeshi Ukraine UKWELI UMEJULIKANA KUWA NI MKUBWA KWELI LAKINI SIO KIVIIILE KAMA ILIVYOAMINIKA
 
Nuclear ni hatari sana kweli lakini sio kwa kiwango hicho , vinginevyo hakuna taifa lingekubali kuwa nazo. Narudià kusema kwamba Nuclear zina madhara makubwa sana lakini sio kwa kiwango kinachozungumziwa. Ni kama ilivyokuwa inazungumzwa kuwa Russia inatisha sana na baada yakuingiza majeshi Ukraine UKWELI UMEJULIKANA KUWA NI MKUBWA KWELI LAKINI SIO KIVIIILE KAMA ILIVYOAMINIKA
We jamaa unaongea tu, according to historia atomic bombs zile zizoangushwa Nagasaki na Hiroshima ilikuwa na radius ya kuunguza tu ya kilometa 4, yani ikiripuka mfano daraja la ubungo apo, sehem itayoungua na mripuko yani moto, ni mpaka kanisa la mama Rwakatare, upande mwingine ni mpaka magomeni mataa, upande mwingine ni mpaka buguruni, na pia mpaka kimara stop over, hii ni kwa fat Man enzi izo iloyoangushwa Nagasaki

Sa mabom ya sikuizi ya nuclear ni Hydrogen bomb, tofauti na atomic bomb ya zamani, hydrogen bomb unatengeneza tu, ukitaka ata bomb la kulipua dunia nzima unaweza kutengeneza, litakuwa kubwa tu sana, linaweza chukua ukubwa wa Dsm nzima, ila theoretically inawezekana
Kati ya yote yalojaribiwa, kubwa kulko lilikuwa ni Tsar bomba, ni la mrusi, radius yake ya kuunguza ni 35 km
Yani ikiangushwa daraja la ubungo, litaharibu kilakitu ndani ya radius 35 kitaungua, nachomaanisha ni kilometer 35 pande zote
Kama ni apo ubungo, mpaka kibaha kutaharibika, kama na pia apoapo mpaka chanika mbele uko kama unaelekea chin uko pia pataungua, inshort ni kitu cha ONE BOMB ONE CITY, kwa Tsar,
Na who knows whats the most powerfull nuclear bomb Yet

Usiseme tu kwa kuhisi kuwa nuclear bomb sio hatari bila kujua, nchi kama marekani au Russia, wana nuclear warheads fuctional kama 5000 hivi kila moja( yaweza kuwa zaidi)
Na marekani na russia miji mikubwa ni mingapi???

Nuclear ni hatari sana, sio kidogo tu
 
Nuclear ni hatari sana kweli lakini sio kwa kiwango hicho , vinginevyo hakuna taifa lingekubali kuwa nazo. Narudià kusema kwamba Nuclear zina madhara makubwa sana lakini sio kwa kiwango kinachozungumziwa. Ni kama ilivyokuwa inazungumzwa kuwa Russia inatisha sana na baada yakuingiza majeshi Ukraine UKWELI UMEJULIKANA KUWA NI MKUBWA KWELI LAKINI SIO KIVIIILE KAMA ILIVYOAMINIKA
Naomba ujielimishe. Hali halisi hatari ya vita ya nyuklia ni haiwezekani kuisimamisha. Kuna makombora madogo, takriban nguvu kama Hiroshima. Inaandaliwa na Urusi pia na NATO (Ukraine walikabidhi silaha hizo kwa Urusi katika mkataba wa Budapest 1994) kwa matumizi a) kupitia mizinga b) kupitia makombora c) kupitia ndegevita. hayo mabomu "madogo" au "tactical nuclear weapons" huhesabiwa kuwa na nguvu ya kilotani (=tani elfu za baruti kali ya TNT) 1- chini ya 100. Halafu ziko hizi kubwa zinazoitwa "strategic nuclear weapons", zinazoandliwa kutumiwa kupitia roketi na ndegevita kubwa.

Bomu la Hiroshima ni "ndogo" kwa vipimo vya leo, ilikuwa na kilotani 12, iliua watu 70,000 mara moja na idadii hiyohiyo katika miezi na miaka iliyofuata kutokana na majeruhi na ugonjwa wa kansa.
Mara upande mmoja unaanza kutumia silaha hizo, upande mwingine utajibu vile. Katika mazoezi mengi yaliyofanywa kila upande ulionekana hakuna njia ya uhakika kusimamisha matumizi hadi kuingia katika silaha za kimkakati (strategic). Maana wangeweza kutumia mabomu madogo mwanzoni dhidi ya vikosi vya adui, uwanja wa ndege, kituo cha roketi na kadhalika. baadaye upande mwingine utatafakari kuitumia dhidi ya eneo ambako inajua kuna makao ya viongotzi; hata usipojua mahali kamili, unaweza kufyeka kilomita kadhaa mara moja. Hapa litatokea tena jibu.... Hasa kwa sababu silaha ndogo hazina usalama kama silaha kubwa. Zile za mikakati zinaweza kurushwa tu kwa kibali cha mkuu wa jeshi (raisi..) Lakini zile ndogo kwa matumizi kupitia mzinga, marta zimegawiwa kwa vikosi, ziko mkonono mwa kamanda wa kikosi.
Hii yote inajulikana imejadiliwa tangu miaka mingi, Narudia: hakuna anayejua namna ya kusimamisha mapigano ya kinyuklia mara imeanza. Hii sababu hazikutumiwa na Marekani na Warusi hawakupigana katika miaka 70 ingawa walikuwa maadui wakali kwa muda mrefu.
Mara silaha za kimkakati zinatumiwa, athira itasambaa hadi hapa Afrika hasa machafuko ya kinyuklia pamoja na athira ya tabianchi (baridi, giza..).
Si mchezo.
 
The Russian team was not invited to the esports tournament, the current winner of which they are

🎮 Russian esports players were not invited to the PUBG Nations Cup series tournament, which will be held in Bangkok from June 16 to 19. The place of the Russian team will be taken by representatives of Indonesia.

🏆 At the same time, the Russian team is the winner of the first PUBG Nations Cup, which took place in 2019.
Galip SV
IMG_20220408_174331_140.jpg
 
Transgender cyclists have been banned from competing with women in the UK.

The country's cycling federation has deemed it "unfair" for men who have changed sex to compete against women and earn points for national competitions.

The organization noted that they still welcome the support of transgender people and non-binary cyclists, but the effect of such a policy in competitive disciplines will still be stopped.

Galip SV
20220408_124936.png
 
When tyranny loses the war against Ukraine, it will be one of the greatest contributions to Europe's security in decades. Consequently, one of the greatest contributions to the security of Finland. That is why we need the weapons that Finland's partners in the European Union have. That is why we need truly effective sanctions against Russia. A sanction cocktail that will be remembered just as Molotov cocktails. People and politicians of Finland, insist on this!
Galip SV

download.jpeg
 
Transgender cyclists have been banned from competing with women in the UK.

The country's cycling federation has deemed it "unfair" for men who have changed sex to compete against women and earn points for national competitions.

The organization noted that they still welcome the support of transgender people and non-binary cyclists, but the effect of such a policy in competitive disciplines will still be stopped.

Galip SV View attachment 2180705
Can you provide definition for the word 'woman'?😎
 
Nuclear ni hatari sana kweli lakini sio kwa kiwango hicho , vinginevyo hakuna taifa lingekubali kuwa nazo. Narudià kusema kwamba Nuclear zina madhara makubwa sana lakini sio kwa kiwango kinachozungumziwa. Ni kama ilivyokuwa inazungumzwa kuwa Russia inatisha sana na baada yakuingiza majeshi Ukraine UKWELI UMEJULIKANA KUWA NI MKUBWA KWELI LAKINI SIO KIVIIILE KAMA ILIVYOAMINIKA
Wataalamu wa mambo ya nuclear kwa utaalamu wao wanatuambia nuclear ni hatari wewe ambaye hatujui kama una utaalamu wowote kwenye mambo hayo unapinga! Ajabu!!!

Unapinga tafiti za kitaalamu kwa kutumia hisia zako mkuu.

Bw. Alex wellerstein mtaalamu wa masuala ya nuclear (Nuclear Historian) ametengeneza website ya 'Nukemap' inayoweza kuruhusu mtumiaji adondoshe bomu fulani la nyuklia kwenye mji fulani ili aweze kujionea mwenyewe madhara yanaweza kuwaje kuanzia vifo, majerui, uharibifu wa majengo/miundombinu/mazingira, madhara ya mionzi, fallouts nk. Unaweza mwenyewe kuingia hapo ujionee. Bomu dogo la kt 140 lililojaribiwa na NK 2017 linaweza kuathiri eneo la ukubwa wa mile za mraba 134 na kuua na kujeruhi zaidi ya watu 700k

Na kinachotishia zaidi kuhusu vita vya nyuklia wala hata sio milipuko yenyewe hasa bali ni madhara ya muda mrefu ambayo huja baadae vikishapiganwa vita vya Nuclear. Wataalamu wa masuala ya nyuklia na wanasayansi mbalimbali wametafiti kuhusu hili na wamekuja na majibu kadhaa wa kadhaa.
Mfano. Profesa wa mazingira wa chuo cha rutgers bwana alan robock ametafiti kuhusu yanayoweza kuwa madhara ya muda mrefu ya 'vita vya nyuklia' duniani kwa kuzingatia models tofauti za uchumi, sayansi na agriculture.

Miji na majiji yaliyoathirika na vita vya nyuklia kwa kuunguzwa yatasababisha moshi mweusi ambao unaweza kupanda mpaka kwenye level ya stratosphere na kuathiri kiwango cha joto na mvua duniani. Tani milioni 5 mpaka 50 ya huu moshi utaleta kitu wanaita 'nuclear autumn' na ikiwa ni tani milioni 50 mpaka 150 basi 'nuclear winter'.

Nuclear Autumn
Pakistani na India (ambao hawana idadi kubwa ya silaha za nyuklia) endapo kutazuka vita vya nyuklia baina yao wanaweza kupelekea nuclear autumn. Km kila mmoja akimpiga mwenzake na mabomu at list 50 ya size ya yale ya hiroshima basi moshi mweuisi unaotokana na kuungua vitu na miji unakadiriwa kufikia tani milioni 5 mpaka 6. Huu moshi ukifika juu unazuia miale ya jua kufika duniani kwa kiasi kikubwa baadae inapelekea kushuka kwa joto na hivyo less precipitation. Ndani ya miaka mi5 ya kwanza itaathiri zaidi ya 40% ya kilimo duniani kote na kufikia miaka 10 joto duniani litashuka zaidi na kufikia level ya chini zaidi kuwahi kushuhudiwa ndani ya miaka 1000 ilopita.
Watu bilioni 2 wanaweza kufa kwa njaa. Imagine hiyo ni vita tu dhidi ya Pakistani na India kama ikihusisha nuclear.

A. Ward kutoka mtandaoni


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kumbe kwenye mashambulio dhidi ya kituo cha treni Kramatorsk, Warusi walitumia mabomu ya kulenga watu (cluster bombs) ambayo yanapasuka hewani na kumwaga vipande vidogovodogo. Hii ni sababu watazamaji hapa walishngaa hawakuona mashimo makubwa kwenye picha. -- Ni uthibitisho kwamba maelezo ya Warusi hayana msingi eti Ukraine ilitaka kuzuia watu raia wasikimbie ili wapatikane kama ngao za kibinadamu. Ukitumia mabomu ya cluster, unataka kuua wengi,, si kuzuia usafiri maana unamaliza ngao zako. Tendo hili linahitaji kuchunguliwa kama ni jinai ya vita.

Russian troops attacked a packed railway station in eastern Ukraine Friday morning and dozens were feared dead.

At least 39 people were killed, according to the regional governor. More than 100 were also hurt in the attack, Ukraine's Ministry of Defense said.

"Russians carried out two missile strikes on railway station in Kramatorsk, where evacuation of civilians was taking place," the Ministry tweeted. "But Russian war criminals not only deliberately targeted thousands of people; they've used cluster munitions. More than 30 killed, more that 100 injured."
Chanzo: Russia attack on train station in eastern Kramatorsk leaves dozens dead, officials say
 
Back
Top Bottom