Hivi kwa nini NATO ipo?. Nchi zote zikijiunga NATO nani atakuwa adui yao.
Mi nahisi hawa wababe wanatafuta kutawala dunia sera zao ndio zitamalaki. Imagine USA na sera zake kusaidia wengine kwa kukopa huku ikiacha wananchi wake hohehahe. Na Russia kutumia gharama kudhihirisha uwepo wake?. Mwisho wa hii vita ni mbaya sana kwa dunia hasa Russia akishindwa. Sera za USA zitatamalaki na upinde ndio itakuwa Dini ya dunia.
Swali fikirishi na zuri mno tena mno... Nchi zote zijiunge NATO... Zitakuwa zinajilinda dhidi ya nani???
US kila mwaka ana spend more than 60Billions Dollars kwenye silaha za nyuklia peke ake. Hii inakaribia budget ya Russia ya millitary kwa ujumla ndani ya mwaka mzima... Kwa ajili ya nani na ili iweje ilhal mwingine yoyote akijaribu kutengeneza anaambiwa anahatarisha usalama wa dunia.
US Majeshi yake yametapakaa kila kona hasa Europe na nchi zinginezo afrika na uko baadh ya nchi huko Asia. Ila Russia, China majeshi yao yapo kwenye nchi zao tu. Je kati yao who is offensive na who is defensive?
US anavuka bahari kwa mwendo wa masaa kuitafuta Europe na Asia akiwa anaizunguka Russia na China kutengeneza urafik na nchi za karibua ya maeneo hayo. Kama ni urafiki wa democracy anayoinadi mbona haifanyi na jiran zake wa karibu kama Mexico na nchi zinginezo hapo Latin America na South America?
Kama waliona ni tishio kubwa kwao kwa USSR kuhost vifaa vya kivita apo Cuba inakuaje wao wanamsogelea mwenzao mlangoni mwake.
Utatangazaje amani mkononi umeshikilia upanga, huku ukimkata yoyote mbele yako unayeona ha-fit kwenye interest zako???
Kwanini kila anayepishana na huu mfumo wa kingese wanaouita democracy kwao mi Adui?
Democracy ni a system of government by the whole population or all the eligible members of a state, typically through elected representatives... Kwa tafsiri hiyo kwani Russia na China viongozi huwa wanajichagua wenyewe? Hakuna mfumo wa Multiparty, hakuna bunge? Hakuna wawakilishi wanaochaguliwa na wananchi?
If their goal ni democracy, kwanini wasianze na UK ndani ya NATO na EU hao hao ambako mkuu wa nchi ni always anatoka ndani ya familia moja tu. Eeeh, Is this democracy mfumo wa serikali ya watu au democracy ni kuwa na serikali inayotii matakwa yao?