Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?


NAKAZIA
 
Huna ushahidi wowote maana hujafanya kazi yako ya kuchungulia vyanzo vyako. Hii post ni takataka. Yule bwana hakuwa "the editor" wa gazeti kubwa la Ujerumani, alikuwa mmojawapo wa wanahabari kama 50 walioajiriwa na gazeti hilo. Baada ya kuondoka (hakuenda kwa amani) aliandika kutunga vitabu akianza kusambaza nadharia za njama, hasa kuhusu maovu ya Uislamu, ya wakimbizi kutoka nje ya Ulaya, na athira aliyodai ya huduma za kijasusi. Hakuwahi kulipwa na CIA.
 
Leo Ujerumani kulikuwa na maandamano ya kuiunga mkono Russia unaliongeleaje hili?
Sema wapi, lete mfano jinsi walivyounga mkono vita ya Urusi,. Usirudie tu madai na picha yeye bendera ya Kirusi. Nimeeleza hapo juu kwa nini watu wengi Ujerumani wenye asili katika Urusi (waliokimbia Urusi kwa sababu hawakutaka kuishi huko) wanapinga ubaguzi dhidi watu wanaosema Kirusi.
 
Kuna tetesi kuwa Finland jirani yake Putin aliyekuwa hafungamani na upande wowote anataka kujiunga NATO. Sijajua kama ni habari sahihi au lah. Kama ni sahihi Putin anachokonolewa ili hasira zimpande zaidi.[emoji2]
Kama pana kosa atakuja lijutia ni la kuivamia Ukraine,ni kama aliwekewa mtego na akanasa mzima mzima.Hao kina Finland kwa sasa hawamuogopi tena,na watajiunga NATO na US atatia mguu wake pale Finland na hatokuwa na la kuwafanya.

Pro Putin wanajipa matumaini kuwa Ukraine kujiunga EU siyo tatizo bali tatizo ni kujiunga NATO,lakini wanasahau ni rahisi sana kupitia EU kuomba uanachama wa NATO ,Ukraine ndiyo kwanza keshaianza safari ya kujiunga NATO na hilo jambo atalikamilisha tu.
 
Moja ya hoja ya putin kuondoa wanazi Ukrain .pia selikali ya Ukrain ina fafhili wanazi.
Putin anafadhili Wanazi. Analipa kundi la Wagner walio na kikosi cha "Rusich" (Русич). Wanachukia watu weusi na wageni kwa jumla. Nenda uwachungulie , ona kama una kitu cha kupinga!
 
Putin anafadhili Wanazi. Analipa kundi la Wagner walio na kikosi cha "Rusich" (Русич). Wanachukia watu weusi na wageni kwa jumla. Nenda uwachungulie , ona kama una kitu cha kupinga!
Nadhan huja nipata mkuu.hizo ni miongon mwa hoja za putin kuivamia Ukraini ambazo si za kweli.
 
Ikikitokea nchi nyingine ifanye inachofanya Ukraine Urusi itakuwa ina kazi ya kuthibitisha ukuu wake anaohisiwa anao.
Huo uwezo na hiyo jeuri hana.Unakumbuka kama week 3 zilizopita ulihoji swali la msingi sana lakini kipindi hicho Pro Russia walikuwa hawashikiki.

Swali lenyewe ulihoji "Hii vita ya Ukraine inaweza kuisha haraka sana kama NATO/US watapenda iishe,lakini kwa nini wameamua kupeleka silaha zaidi kwa Ukraine badala ya kuimaliza hii Vita?" Hakuna aliyekujibu lile swali,sasa kwa kinachoendelea na ukiwaona kina Finland wanajitokeza kutaka kujiunga na NATO ni kama wanazidi kumsakizia auvae mkenge zaidi.
 
Sioni Ukraine kujiunga na NATO karibuni, NATO imekataa tangu 2008. Ila Finland wakitaka watapokelewa.
Hapo Putin anapata tokeo ambalo hakutegemea: Mpaka na nchi ya NATO kwa kilomita 1300. Hekima yake!
 
Mm hii habari nimeiona Dw ni raia wa Ujerumani ndio walikuwa wanaandamana walikuwa pande mbili unao iunga mkono Russia na wanaoiunga mkono Ukraine na polisi walikuwepo ili kuhakikisha hakutokei vurugu kati ya hizo pande.
 
Kama naanza kukupata iv mkuu.pia nangoja reaction putin juu Finland kutuma maombi Kujiunga na NATO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…