Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,402
Sioni mwisho bado. Maana vita anaweza kuendesha kwa mud bila dolar. Rubel anaweza kuchapisha anavyotaka (itaharibu uchumi zaidi, lakini anaweza kuendelea bado kwa kufanya wananchi maskini zaidi); kwa rubel analipa jeshi, analipa wafanyakazi kwenye viwanda, viwanda vya kutengenezea silaha anavyo.Huu ndiyo mwisho wa Putin,huwezi survive kwa vile vikwazo na mbaya zaidi ana rafiki mnafiki kupindukia yule mvimba macho Xi jinping,hana msaada kwake
Hanunui silaha nje.
Isipokuwa vipuli vya compyuta anazohitaji kwa silaha za kisasa, ataona matatizo mara akiba zinakwisha. Hapa anahitaji soko la dunia maana hajitegemei.
Atazipata kwa bei maradufu au zaidi kwa njia ya magendo, na hapo anataka kutunza dolar / Euro alizo nazo Urusi (hii sababu kutolipa madeni maana angeweza)
Hivyo naogopa kwa miezi kadhaa bado atakuwa na uwezo wa kuendelea na kuleta vifo na uharibifu.
Isipokuwa akiona hali inaanza kuwa mbaya kweli, atatangaza ushindi bila shaka.
Ilhali hadi sasa asilimia kubwa ya wananchi bado wanaamini propaganda yake, atatumaini watamwamini pia ushindi...
