Kweli ulisema nikajibu ujielimishe kwa bahati mbaya hujafanya. Hakuna jeshi linalogoma???
Unachekesha, kwanza fungua macho yako Afrika, eti serikali hizo zote za kijeshi zimetokea kwa kumtii amiri jeshi mkuu?? Unachekesha! Walimpindua na kujiweka mahali pake.
Amiri jeshi mkuu kabisa katika historia (angalau mmojawapo) alikuwa Aleksander Mashuhuri. Jeshi lake liligoma mw. 326 KK alipotaka kuvamia Uhindi (hujasikia bado? Basi jisomee!).
Mgomo mashuhuri wa wanamaji wa Urusi kwenye manowari Potemkin mwaka 1905
Mgomo wa jeshi la Urusi kwenye mwaka 2017 uliompindua Tsar (mfalme) wa Urusi
Vilevile 1917 mgomo mashuhuri wa jeshi la Ufaransa, ulikandamizwa kwa kupeleka maelfu mbele ya mahakama ya kijeshi na kuua wengi
Mfalme wa Ujerumani (kisheria wakati ule hata mfalme wa Tanganyika) alipinduliwa baada ya mgomo wa jeshi la wanamaji mjini Wilhelmshaven mwaka 1918
Jeshi la Pakistan iliona mgomo wa vikosi vyake katika Pakistan-MAshariki walioamua kupigania upande wa uhuru wa Bangla Desh
2014 wanajeshi 54 wa jeshi la Nigeria walipewa adhabu ya mauti kwa sababu walikataa kushambulia mji uliovamiwa na Boko Haram (sijui kama ilitekelezwa)
2022 uvamizi wa Odessa ilisimamishwa kwa sababu kundi la wanamaji Warudi waligoma ghafla walipoambiwa washambulie kutoka meli zao (ona
Российские морпехи-срочники устроили бунт, когда им приказали высадиться «прямо в Одессу» | Новости Одессы)
Na huyu dikteta wa Belarus yuko to kwa sababu Putim alisaidia baada yeye kugushi uchaguzi. Wafanya kazi wa reli ya Belarus waliharibu njia za reli mara kadhaa ili Warusi wasipeleke vifaa Ukraine. Wengi walishangaa kwa nini jeshi la Belarus haikushiriki hadi sasa. BAsi kuna habari mara kwa mara kwamba wanaogopa mgomo.
Kama wewe, mtaalamu wa historia ya mgomo wa kijeshi, unaona haiwezekani, labda ninapaswa kusalimu amri mbele ya ubora wa elimu yako???