Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hahaha, ngoja tuone, tuombe uzima.
 
Inama upigwe nyembe,
Kumbe unapenda sana kuchezea nyembe? Tafadhali usijiumize!
Niongete: Nyembe za Putin zilisaidia pia maazimio ya Uswidi na Finland kutuma silaha Ukraine.

Ona: STOCKHOLM (Reuters) - Sweden will provide Ukraine with an additional 5,000 anti-tank weapons, TT news agency quoted the Swedish Defence Minister saying on Wednesday. Sweden has already sent 5,000 anti-tank weapons, along with other military materiel to Ukraine.
 
Maskini Putin! Anapaswa kuchapisha rubel tena ili kugharamia maigizo ya waajiriwa wake huko DPR na LPR kuwa na ofisi Moscow, ilhali wenyewe ni ofisi ya Moscow tu katika Ukraine...
 
Unaandika vitu usivyo vijua
 
Mabeberu ndiyo yametufikisha hapa mkuu, wao ndiyo waliendesha operations nyingi za kuangamiza kizazi kipya cha wasomi na wazalendo wa kweli na kutuwekea viongozi wajinga,walafi na wabinafsi kibaya zaidi hao viongozi wameweka ndugu na jamaa zao sehemu muhimu za maamuzi matokeo yake sehemu muhimu wale decision makers ni wajinga na wapumbavu ndiyo chanzo cha matatizo haya yote
 

Hizo weapons zimesaidia nini mpaka sasa?? Kama tunaendelea kujichukulia miji kila siku?? Acha mahaba kijana
 
Embassies of the DPR and LPR may be opened in Moscow in the next one to two months.

RIA Novosti writes about this, citing a diplomatic source.

β€œWe will try to [be] done in the near future, the sooner the better. We are engaged in specific work, ”said the source of the agency.
 
Marekani anataman sana kupeleka silaha za kisasa ukraine ila sasa ana ogopa zitamtia aibu. Anaogopa kupeleka Mabati yake Patriot na Thaad ila anamtaka turkey apeleke S-400 ya Mrussi.

Kwanini asipeleke Ndege za kivita za kisasa kama raphale, F series nk. Yote anajua haziwezi kumsumbua Mrussi zitaishia kutia aibu silaha zinazopelekwa ni za kingese kweli ambazo zinaishia kuharibiwa na kuchukuliwa na Russia.

Russia amewaambia watume silaha za kisasa na sio hzo Javelina hazina impact kwa Russia. Hichi ndo kipindi ambacho marekani ilibidi atangaze silaha zake kwa navyo mjua mpenda sifa ingekua nchi nyingine kama libya angekua kashapeleka muda.

Anaogopa kupeleka Ukraine ataishia kupewa aibu tu na hii Operation inamsumbua sana anataman sana iishe lakin aibu duniani coz ishajulikana ni Russia vs USA & NATO. Nchi 30 zenye nguvu mnasumbuliwa na Taifa moja [emoji635] ambalo ni maskini?? Sasa Russia+China+India+NK mtaweza mziki wao ikianza WW3??
 
Ukraine peke yake imewatoa kinyesi. Wakati marekani inapigana na Iraq, mwezi mmoja kazi imeisha. Wakati huo Iraq ilikua dola kubwa yenye uwezo wa kuvamia jirani zake kina Kuwait na Iran. Hizi losses marekani hajapata tangia ww2View attachment 2197367
Ww kweli huna akili iraki ambayo ilikua Haina mshirika hata mmoja vikwazo vyote mpaka vya anga marekani alikua anatokea pande zote za majirani wa iraki unatobolea wapi
 
Hizo weapons zimesaidia nini mpaka sasa?? Kama tunaendelea kujichukulia miji kila siku?? Acha mahaba kijana
Silaha hizo zimeshasaidia kumfukuza Putin Kyiv. Jambo hapa si silaha, jambo ni dai lako eti Finland na Uswidi wataogopa kujiunga na NATO wka sababu ya kuhofia "nyembe za Putin".
Nyembe hizo ni sababu zao kubadilisha msimamo na kujadili NATO, pamoja na kutuma silaha Ukraine.
Maana sawa na nchi nyingine za Ulaya, wanamwona Putin sasa kama tishio. Wanaamini kunyamaza ni kosa baya, sawa na hali ya 1938 ambako mataifa ya Ulaya hayakumpinga Hitler aliyeanza kuvamia nchi jirani kama Austria na Chekoslovakia.
Putin alikadiria vibaya, pamoja na hali ya jeshi lake . . .
 
Unaandika vitu usivyo vijua
Labda unionyeshe kwamba sijui vitu? Mataifa ya Ulaya wamejifunza kwamba Putin ni hatari, ndiye kiongozi anayepuuza ahadi na mikataba. Ni tayari kuua watu kwa michezo yake ya kisiasa. Haheshimu haki za mataifa.
Tafadhali unionyehsa ambacho sijui.
 
Kama huyu Chalii aliwakalisha tuliii wakaishia kubwabwaja... Seuze Russia Wale waeandelee kuji'mwambafy Hollywood wakituonesha Mjeda mmoja anapigana na na watu buku bila mkwaruzo [emoji847]
 
Ww kweli huna akili iraki ambayo ilikua Haina mshirika hata mmoja vikwazo vyote mpaka vya anga marekani alikua anatokea pande zote za majirani wa iraki unatobolea wapi
Kaka tafadhali ujielimishe kidogo kabla ya kuandika. Vita ya Iraki - majirani yenye mipaka mirefu ya Iraki ni Iran na Syria. Marekani haikuweza kutumia maeneo yao. Kwa hiyo si kweli kwamba "alikua anatokea pande zote za majirani wa iraki" jinsi ulivyoandika.
 
Kuna mtu Humu ndani nimeona anasema Finland imeshaghairi kujiunga na NATO wakati last week Bunge lao lilikaa kujadili hili jambo na Wanatarajia May 16 waanze hatua Rasmi za kujiunga na NATO...

Ila Hawa watu wa Putin wanamtia aibu Mzee wao.

Kuna siku walisema Western countries haitaweza kutuma tena Silaha Ukraine, Jana Waziri wao analalamika USA anapeleka Silaha nyingi sana Ukraine πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…