Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Sasa wewe uko Mombasa kama ulivyosema na una guts za kuwapangia Sweden,umenikumbusha na aliyekuwa na matokeo ya Uchaguzi wa France kuwa mpinzani wa Macron lazima atashinda kwa kuwa ana sera zinazoendana na Putin
Neno langu au maoni yangu sio sheria cc mie natoa maoni na mtazamo wangu kupitia hali ya mambo
Ila siioni FINI na SWED wakijiunga na NATO ila tuupe muda nafasi yake hua haudanganyi huu
 
Chanzo si Russia, EU ndio imekaa katika nafasi ya maamuzi either vita itokee au isitokee.
 
Mkuu nimekuuliza hizi habari unagoogle muda gani?
 
Hayo maneno ya kupata mbadara wa gesi ya Urusi ni ya kisiasa zaidi lakini kivitendo hayatekerezeki.
Kwa Poland sidhani. Wameshajenga bandari kubwa la gesi kwenye pwani, pia wameshajenga bomba la gesi kwenda Norwei. Hawatakosa gesi.
Bulgaria sijui, nadhani huko Warusi wanalenga kutenganisha vyama vinavyobeba serikali. Tuone.
Ujerumani ambayo ilitegemea sana Warusi imeshapunguza mafuta ya Urusi kutoka asilimia 35 ya mahitaji yake kabla ya vita hadi asilimia 12 tu sasa, hadi mwisho wa mwaka wanataka kuiacha kabisa. Gesi bado, lakini hata kama Putin angesimamisha pia gesi ya Ujerumani wanayo akiba ili wadumu mwaka 1 na katika kipindi hiki wanaamini watapata mbadala.
Ila Putin atatafakari mara tatu kabla ya kuzamisha gesi ya Ujerumani maana hana mteja mbadala, mabomba ya kwenda China hayatoshi hata kidogo, mpaka kujenga atahitaji miaka , atapoteza pesa nyingi.
 
Kabla kujiunga na KGB (1975) Putin hakua na mafundisho yeyote ya kijeshi wala cheo ndani ya Soviet union, mwisho wake ni mchezo wa Judo.

Kwahio ni ngumu kabisa kwake kuweza kufika Tanzania kwa niaba ya serikali yao. Alafu katika hio picha tunaona anaedaiwa kuwa Putin ni wa umri wa makamu.
 
Yaan wana akiba ya kutumia Mwaka na bado kila siku wanaagiza?? Mzee acha fix za kitoto.
 
Wamuache huyu Putin wasimshike shike Sharubu, Ukraine waendelee kujihami...Kumshambulia kwenye ardhi yake ni kumprovoke na retaliation inaweza kuwa na impact mbaya, Huyu jamaa bado ana akili ya kijamaa.
Kama wanao uwezo wa kumshambulia kwake wafanye hivyo harka na mapema itamlazimu pia ajihami kuanzia nyumbani kwake. Uajamaa hauheshimu uhai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…