kama URUSI itatumia Nuclear aisee dunia itakuwa kwenye wakati mgumu mno.. hakuna atakayekuwa salama sababu US wataingia, EU wataingia, NATO wataingia, UK itaingia - Vita itakuwa na pande mbili - of course North Korea na China watakuwa upande wa URUSI.Russia inapinga sana hili jambo la NATO kupeleka silaha Ukraine na kuwapa mafunzo.
Russia imeongea mara kwa mara, Russia imetoa onyo lakini NATO hawasikii.
Russia imesema zaidi ya mara moja kwamba kuna uwezekano kukawa na matumizi ya nuclear na wwIII kutokea any time kama NATO wakiendelea, jamani tusibeze hili, inaelekea kuna mtu atapigwa na kitu kizito kichwani aje alete fujo, Russia akili zao wanazijua wenyewe.
Nafikiri baada ya vita watakaobakia hai watasimulia - tusiombe tufike huko - temeni mate chini.