Kaka kama huna habari jinsi gani gesi inavyotumiwa na jinsi gani soko la gesi linavyofanya kazi, labda utafakari kidogo kabla ya kutukana??
Ndiyo, Ujerumani wanazo ghala kubwa za gesi. Ona chini maelezo (yenye namba za siku kabla ya vita):
Soma: "The total capacity for injection and withdrawal from German gas storage facilities is around 23 billion cubic meters of gas. Germany ranks fourth among the world’s largest storage countries. Only in the US, Ukraine and Russia there are even greater capacities."
Chanzo: Gas Storage Capacities - INES Initiative Energien Speichern
Soma "About half of German imports of gas.., and about one third of its oil imports originate from Russia."
Chanzo: What if Germany is cut off from Russian oil and gas?
Kwa hiyo wanahitaji kupata mbadala kwa nusu ya mahitaji yao ya gesi (sehemu inayotoka Urusi).
Matumizi ya gesi ya Ujerumani mwaka 2021 yalikuwa mita za ujazo bilioni 87; nusu yake (=gesi kutoka Urusi) ni takriban bilioni 45; hivyo serikali yao inaona kwamba gesi kutoka nchi nyingine pamoja na akiba inaleta kiasi cha kutosha ili kudumu mwaka 1.
Kuhusu mafuta wametanagza kwamba wameshapunguza matumizi ya mafuta ya Urusi kutoka asilimia 34 hadi asilimia 12.