Siku ya 65 ya oparesheni ya Urusi nchini Ukraine.
Leo kuna mengi sana yametokea, nitachukua machache yale makubwa makubwa tu ili twende sawa.
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kwamba shambulizi la jana mjini Kyiv lilirushwa kutoka kwenye Submarine iliyoko katika Bahari nyeusi. Wakati huo Rais wa Ukraine Volodmr Zelensk amelaani shambulizi hilo lililolenga kiwanda cha kutengenezea makombora na uwanja wa ndege mjini Kyiv, Zelensk anasema Urusi imedharau UN ambapo Katibu Mkuu alikuwa bado yuko katika mji huo wakati mashambulizi yanafanyika. Katika majibu, Moscow imesema wajibu wake ni kulenga shabaha, na shabaha haina muda, shabaha haina kinga popote ilipo Moscow itaruhusu pigo.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, amesema NATO iko tayari kuilinda Kyiv dhidi ya Moscow, NATO iko tayari kuilinda kwa miaka yoyote Kyiv dhidi ya Sera za Kisoviet, Jens Stoltenberg amezitaka nchi za Magharibi kujiandaa kwa silaha bora na za kisasa kupsmbana na Moscow kwa miaka mingi zaidi. Moscow imejibu kuwa iko tayari, kidole gumba chao kiko kwenye batani ya Sarmat system na intercontinental ballistic missiles inawasubiribtu wafanye provocations tu ili dunia ishuhudie reactions ya Moscow.
Jasusi wa mtandao (Cyber security) bwana Vladimir Soliev, ameonya kwamba Urusi ina silaha ambazo zinaweza kuifuta kabisa nchi katika ramani ya dunia, Akitolea mfano Uingereza kwamba kombora moja la Sarmat linaweza kuifuta kabisa kwenye uso wa dunia nchi hiyo. Nanukuu, "We wil remove Britain from the map with just one Sarmat missile. To destroy the whole of Britain only one of our Sarmat missiles is enough and after firing the first missile, it will no longer have a British one".
Moscow imewawekea vikwazo vya maisha raia 600 akiwemo Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau kuingia Urusi na maeneo yake yote ya kimbinu. (Nchi washirika). Moscow imesema itaendelea kuchukua hatua zaidi ya hizi kwa mataifa mengine yote maadui wa Moscow.
Marekani imeweka wasiwasi kwamba kitisho kinachoikumba Urusi kwa sasa kinaweza kuifanys nchi hiyo ichukue hatua za nyuklia. Washington inaamini kuwa bado haijafika tishio kubwa la Moscow kutumia silaha zake za maangamizi dhidi ya maadui, Marekani inaamini kuw Moscow unafanya vitisho tu haiwezi kuchukua hatu kali hivyo. Japo wanashangazwa na hatua ya kushambulia mji mkuu Kyiv ilihali mji huo umekrimu Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Hii inawafanya Washington watathimini upya makadirio yao ya awali dhidi ya uthubutu wa Moscow.
Majeshi ya Urusi yamemua Mamluki wa Marekani Willy Joseph Cancel, huyu ni mwanajeshi mstaafu Komandoo kutoka kikosi cha Marine, Kwamujibu wa Mama yake mzazi, Willy alisaini mkataba na kampuni moja ambayo hajaitaja jina lakini amesema alihudumu kwa masaa 24 na hajawahi kuoneka nyumbani tangu asafiri kwenye Ukraine. Bado Marekani inasita kuthibitiha kifo hicho ambacho idara za Ujasusi Moscow zimethibitisha.
Mamluki Scott Sibley mwenye miaka 36, ameuawa na majeshi ya Urusi, Scott ni mwanajeshi wa jeshi la Uingereza ambae anahudumu kikosi cha Wanamaji. Wizara ya ulinzi Urusi Imethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa ni mmoja ya mamluki zaidi ya 7,000 wanaowindwa na Moscow mmoja mmoja na hadi sasa wamesha wa elemminate zaidi ya 360 kwamjibu wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi.
Nchi za Germany, Austria, Hungary na Slovakia zimeanza mchakato wa kufungua akaunti ya benki katika benki ya Gazprombank kwaajili ya manunuzi ya Gas kama takwa la Moscow linavyo taka. Amri ya Kirais ya Putin inamtaka kila aliyena uhitaji wa mafuta na gas ambae ni adui wa Moscow atalazimika kununua kwa srafu ya Moscow ya Ruble. Majadiliano kati ya makampuni ya usambazaji gas ulaya na Moscow yanaendelea huku amri ikiwa palepale kwamba bila Ruble hupati gas.
Rais wa Urusi Vladmir Putin na Rais wa Ukraine Volodmr Zelensk ni miongoni mwa walioalikwa katika mkutano wa nchi zenye uchumi mkubwa na kati wa G20. Mwaliko huo unakuja huku hali ya mambo katika mataifa hayo ikiwa tata, huku Urusi ikiendelea na oparesheni yake Mashariki mwa Ukraine. Na leo jioni mji wa Bryansk mpakani mwa Ukraine umeshambuliwa na makombora ya Ukraine.
Jamhuri ya Czech imesema kwamba haitalipia gas kwa Sarafu ya Ruble kama takwa la Moscow lilivyo, Waziri Mkuu wa nchi hiyo amesema nchi yake itaendelea kulipa kwa Euro kama mkataba wa Moscow na Czech unavyotaka. Moscow imejibu na kusema muda ukifika wa kuhitaji gas wataamua wao Czech kama wanunue kwa Ruble au wakalale na Euro yao.
Moldova imekamata silaha za kijeshi zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Houston Marekani kwenda Ukraine, Idara za Ujasusi za Moldiva kwamsaada wa taarifa za kijasusi za Kimataifa (Moscow) ziliweka mtego matika uwanja wa ndege wa Chisinau ambapo abiria mmoja alikuwa anasafirisha shehena ya silaha kuelekea Ukraine.
Majeshi ya Urusi yamefanikiwa kuingia katika miji ya Russkaya, Lozovaya, Ukronazis na Kharkov, ambako mapigano makali sana yanaendelea hadi, Vikosi vya Urusi vilikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa majeshi ya Ukraine na mamluki wa kigeni, lakini Majeshi ya Urusi yamefanikiwa kuvunja ngome ya maadui na kufanikiwa kuingia katika miji hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetoa taarifa kwamba Majeshi yake yamefanikiwa kudhibiti na kuangamiza kabisa mfumo wa makombora ya Tochka-U ya Ukraine katika miji ya Gorokhovsky kwenye mkoa wa Nikolaev, na mkoa wa Kherson ambayo yalikuwa yamelengwa kwa raia, Oparesheni inaendelea mji kwa mji na nyumba kwa nyumba.
Majeshi ya Urusi katika mji wa Kherson yamemkamata Kamanda wa zamani wa Majeshi ya Ukraine aliyekuwa akiongoza platoon katika mji huo wa Kherson, katika Oparesheni hiyo majeshi ya Ukraine yamefanikiwa kuamata silaha mbali ikiwemo magruneti yakiwa yameshategwa tayari kwa mashambulizi za ghala la silaha aina ya AK-47 zikiwa zimepokelewa toka Magharibi, Visu vya kikomandoo 260, na nyingine nyingi.
Urusi ikitumia makombora ya Kalibr High-Precision Cruise Missiles na GM-94 hand grenade launcher imeendelea kubamiza maeneo ya shabaha muhimu za kijeshi na miundombinu huko Donbass, Rubizhne, Fastov, Krasnoselka na Polonnoe
Kwa mara ya kwanza dola imeuzwa kwa bei rais mbele ya Ruble, ambapo leo imebadilishwa kwa Ruble 71, tangu mwezi November. Vile vile pia EUR imeshuka bei ambapo imebadilishwa kwa ruble 74, anguko hilo linatokea kwa mara ya kwanza tangu Mwaka 2020.
Rais wa Indonesia Joko Widodo ametupilia mbali ombi la Rais wa Ukraine Volodmr Zelensk la kupatiwa silaha za kivita zimsaidie aendelee kupambana na Urusi, Katika taarifa ya Rais Mjini Jakata imesema sera ya kigeni ya serikali ya Indonesia inaibana nchi hiyo kujihusisha na mgogoro huo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Bunge la urusi la Duma, General Zavarzin ametaka makombora yaelekezwe Ikulu ya Kyiv na katika mji wa Lviv ambako ndiko kituo muhimu cha shughuli za uchochezi zaidi wa vita unaofanywa na Marekani na Umoja wa Ulaya.
Source: Novost news