Watu wa Dunia nzima wanajua kua Ukraine inapigwa vibaya sana licha ya kusaidiwa Silaha na NATO.
Watu wa Dunia nzima wanajua kuwa NATO si lolote si chochote kwa Urusi.
Watu wa Dunia nzima wanajua kua Urusi haiwaogopi NATO na inawadharai sana,Iko tayari kupigana nao lakini NATO haiko tayari kupigana na Urusi.
Ndugu yangu 1954,binadamu Wana akili sana ,kwa asili ni viumbe pekee wadadisi sana.
Hivyo bila kuambiwa na mtu yoyote kwa vita hii,huangalia,husilikiza au kusoma vyombo vya habari vya west Kisha hufanya udadisi kwa kuangalia au kisoma au kusikiliza vyanzo vingine vya habari,na hapo ndipo hujua ukweli na kuwaacha wanaofanya propaganda waendelee na propaganda zao.
Kilichowafanya watu wa Dunia hii kuifuatilia kwa undani vita hii,ni tabia za west walizoonesha.
Kwa mfano watu walishuhudia vita ya USA na Allies wake dhidi ya Iraq mara mbili,USA dhidi ya watalaban na Alqaida huko Afghanistan,NATO na Yugoslavia,Kosovo na serbia na hata Syria.hapa watu wa Dunia hii wanajiuliza kwa Nini west wamehamaki namna hii kwa Ukraine na Urusi?
Mbona vita hizo nilizozitaja walipeleka vikosi vya NATO ama USA na Allies lkn kwa Russia wanaishiabkutoa silaha TU?
Kwa machache hayo ndio Sasa watu wa duniani wameamua kuifuatilia mwenendo wa vita hii kwa vyanzo tofauti tofauti