LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Papa Fransis katika dominika ya leo kutoka Vatican amewatakia heri waukraine waliyo katika mstari wa mbele
 
Raia wengi wa urusi wangekuwa wanakubaliana na alichofanya Putin, wasingefungiwa mitandao kma facebook nk

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Africa ipi hiyo? Yaani uache kukaa kwa mahindi ukae kwa wapuuzi na loosers hao maskini wa Russia?

Egypt na South Africa wote wamemzingua huyo Russia.

Pia mimi hapa ntakuwa wa kwanza kutungua wanaounga mkono Russia.
Ww subiri Afghanstani naye yupo tayari ku join kwa Urusi
 
Jawabu ni kwamba: Inakubidi urudi katika historia mwanzo wa vita baridi baada ya ww2 mpaka 1997.
Huwezi kujifunga kwenye minyororo ya historia,huyo Russia angetaka hicho anachodai asingeruhusu Nchi zilizokuwa sehemu ya federations ziwe Republics.

Kwa kuruhusu tuu hilo hana haki tena na anachodai.Ndio maana sasa ameamua kupandikiza watu kwenye majingo yanayojitenga,anatumia njia ile ile walioyotumia west so vita ya nini sasa.
 
Baadhi ya nchi zinazidi kuvunja policies zao za kijeshi ambazo zimekuwa zikizoeleka. Sweden nayo imetangaza kupeleka misaada ya kijeshi Ukraine zikiwemo rocket launchers, helmets, anti-tank missiles bamoja na body amours.

Ila Ujerumani ndiyo inayoongoza kwa kuvunja policies zake za kijeshi na kupiga U-turns nyingi kwa muda mfupi sana.
 
Kuna shida gani? Kwani yeye kakatazwa kuweka base Cuba?

Mbona kapeleka wanajeshi Venezuela nani kamkatalia?

Amemtushia na Sweden na Finland eti watakumbana na hatua za kijeshi wakijiunga
Bora zako wewe Mmarekani wa Tandahimba una ana akili sana kuliko hata Colonel Macgregor wa Jeshi la Marekani ktk kuona kuwa hakuna ubaya kwa Marekani na NATO kuweka ngome zao za kijeshi Ukraine na pia Russia kuweka ngome ya kijeshi Cuba.

Colonel Macgregor, afisa mstaafu wa jeshi la Marekani anakujibu hivi Marekani ina nafasi ya kuepusha vita na Putin (Russia). Jambo la kwanza wanalopaswa kufanya Wamarekani ni kukiri na kukubaliana na nukta ya msingi ya Putin (Russia), ambayo serekali ya Russia imeiweka wazi kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Nukta yenyewe ni kuwa Russia hawataki majeshi ya Marekani, mizinga ya Marekani, na majeshi ya NATO kwenye mpaka wake na Ukraine (Mashariki ya Ukraine kwenye majimbo yaliyotangazwa huru na Putin).

Colonel Douglas akaendelea kusema: Kiukweli kabisa hata sisi Wamarekani hatukuyataka majeshi ya Russia na mizinga yake ndani ya Cuba, Putin naye hataki mambo hayo mashariki mwa Ukraine. Lazima tukubali madai hayo. Tuache kujifanyisha kuwa madai hayo hayana maana (ni ya kipuuzi).
======



COL. DOUGLAS MACGREGOR: Let me just reiterate something. I, like you and millions of Americans, would prefer that the troops headed to Eastern Europe right now were headed to the Mexican border. But I’m also very concerned that we find a way to avoid a conflict with Russia. The first thing we have to do is acknowledge that Putin’s basic point, not just his point, the Russian government’s point, which they’ve made for 25 years, is valid. They don’t want U.S. forces and missiles and NATO troops immediately across the border in eastern Ukraine. Absolutely. We didn’t want them in Cuba, he doesn’t want them in eastern Ukraine. We should acknowledge that. Stop pretending it’s a nonissue. It is a major issue for them. Let’s acknowledge it and then let’s get down to business and tell them fine, our concern at this point is we don’t want you to proceed west towards the polish border over the Dnieper River in Ukraine.
 
Si ilipigwa mkwara juzi na Russia,nadhani hii ni wake up kwa Sweden,Finland na Nordic countries zingine wakiwemo akina Kazakhstan,hazitakubali kupangiwa maisha tena na Russia.

Hii ni technical error Russia imefanya.
 
Sema Nini!!!.
Msalimie huyo solokoto juu ya jiwe hapo.
 
Lakini mm mkuu naona hatua ya Ujerumani kupeleka silaha Ukraine ni mbaya maana ninahofia wenda Urusi ika lazimika kuanza kutumia nguvu kubwa sana kitu ambacho kitasababisha maafa makubwa kwa Ukraine ikageuka Siyria ya Ulaya.
Maana nikikumbuka yale mashambulizi ya anga yaliyo fanywa na Urusi kule Allepo na pata hofu.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Nani kasema anataka kupeleka silaha kwenye majimbo yaliyojitangaza huru?

Kisingizio cha Russia ni kwamba hayo majimbo wakazi wake wengi wanaongea ki Russia so wananyanyaswa na Ukraine.

Lakini sidhani kama ni kweli wananyanyaswa, ukweli ni kwamba ni sehemu ya ku destabilise Ukraine na kuharibu ku push NATO nje zaidi ya mipaka ya Russia.
 
Unaijua lakini Ka50/52
Mi 35/24,Mi28 nk.
Hizo baylatkar zenyewe Ukraine walikua nazo nyingitu lakini hazijafanya kazi. Kama katushka tu na Idd Amin Dadaa
 
Na watu wengi hawaelewi kuwa nguvu anayoitumia Urusi ni ndogo. Ikiwa mkakati wake hautokamilika kwa muda aliyojiwekea. Suala litakalobaki ni moja tu nalo amalize vita. Akifikia hapo yule Rais anayetaka kuonekana shujaa watu wataanza kumuita mjinga.
Hata mm hili jambo nimewambia watu wengi lakini wamekomaza vichwa Ukraine akiendeleza ukaidi atageuka kuwa Syriya ya Ulaya.
Nikikumbuka Aleppo ulivyo teketezwa ndani ya wiki moja nawaonea huruma raia wa Ukraine.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…