Putin alivyotangaza kuingia Ukraine maazimio aliyoyataja ni nini? Au Operation hiyo ilikuwa inahusu nini?
Naomba unijibu tafadhali!
Kisha ndiyo tuje kwenye malengo yamefanikiwa au hayajafanikiwa? Na hapa naomba unijibu tafadhali.
Ngoja nikusaidie Kidogo.
Kiufupi,Malengo ya Putin hayajatimia hata Kidogo.
KIUCHUMI
Marekani ilipotangaza kwamba itaweka vikwazo,Russia ilisema haitishiki na Vikwazo. Hapa,Russia alijua kwamba Ulaya haitaungana na Marekani kuuwekea vikwazo Russia Kama ilivyokuwa mwaka 2014 baada ya kuichukua Crimea ambapo Ujerumani na nchizo zote za Ulaya isipokuwa TU Uingereza zilikataa kutii vikwazo vya Marekani,MATOKEO Yake yamekuwa tofauti,Bomba la Gas limepigwa Chini(Putin hakuamini make alijua German atagoma shinikizo la marekani),Mali zote za Urusi na Matajili wa Urusi Duniani kote(Marekani,Canada,Japan,S.Korea, na Ulaya yote) zimegandishwa/Freezed. Bank karibia zote za Urusi zimepikwa mkasi. Putin mwenyewe Binafsi na waziri wake wa Mambo ya nje Mali zao zimetaifishwa Ulaya,Canada,Japani na Marekani.
KIVITA
Urusi ilikuwa na lengo la Kuisambaratisha Serikali ya Ukraine na kuweka Rais Mwingine,Ndio maana Putin aliwaambia Wanajeshi wa Ukraine waipindue Serikali,lakini Waligoma badala yake wakaenda Frontline kupigana Kama Zelensky alivyowaamrisha. Lengo la Putin Limegoma.
Pia,Mpaka Sasa Russia wameshindwa kabisa kuuteka mji Mkuu wa Ukraine,Kila wakienda wanakutana na Upinzani mkubwa Sana. Mpaka wameshaanza kusema eti Kuna Mamluki kutoka Marekani na Uingereza wanapigana sambamba na Wanajeshi wa Ukraine.
Kuhusu kutumia Nyuklia,hivyo ni vitisho vya Putin ili Ulaya wagawanyike katika kuiadhibu Urusi kiuchumi. Hiyo inaitwa DIVIDE AND RULE. Nalo hatafanikiwa. Endapo kweli atawaagiza Majenero wake warushe Nukes kuelekea nchi yoyote ile ya Ulaya au Marekani,hapo ndipo atakapojua jua kwamba maamuzi ya uvamizi wake kwa Ukraine yalikuwa kichwani mwake TU,Watampindua na Kumuondoa Madarakani.