Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo Ukraine wanazidi kupata ujasiri na kuwajua zaidi warussia.

Mwisho wa hivi vita ni Russia kuchakazwa na kufurumishwa kutoka kwenye ardhi ya Ukraine na mambo yatakuwa mabaya zaidi pale wanajeshi wa Ukraine wanaopewa mafunzo nje ya nchi watakaporejea vitani na silaha za hatari.
 
PROPAGANDA hizo; Kwa Mtogole & Co. wanadai hivyo.
 
... kwa kichapo alichokula leo lazima fashisti aweweseke vibaya.
 
Teh teh teh taratibu mnaanza kumkubali Comedian Zelensky kwa dozi ya kutwa mara tatu anayompa Putin.
Habari ni yakweli kabisa na imelipotiwa na kila chombo cha habari lakini watu mnataka kuzidisha chumvi.

Natumaini na ww umeiona hiyo video ya shambulizi haya tuambie magari sijui 76 na wanajeshi 1000 wako wapi hapo ?
Mm nilicho kiona ni vifaru na mizinga visivyo zidi 15.
 
... Pale sio harusini Mkuu kwamba mpiga picha angekuletea matukio yote ukumbini.
 
Kwahiyo watapewa mafunzo ya kujikinga na vifo hatapale wataposhambuliwa na hypersonic??
 
View attachment 2223301
Polisi Israel wanawapiga waombolezaji wanapemda kumzika Mwandishi wa habari aliyeuliwa Kwa risasi na polisi wa Israel .... Lakini dunia IPO kimya tu.
Dunia ipo kimya as if hilo tukio limetokea mbinguni. Kuna watu wanadai hawana upande humu wanakemea uonevu haijalishi nani kafanya. Lakini hadi sasa sijamskia hata mmoja wao kukemea. Huo tunaita ni unafiki mkubwa.

So they want us to stand with Ukraine, je Palestine and other Victim duniani kote sio watu? Don't they need our attention? Ukiwa mbaguzi ukubali kubaguliwa.

For those who weren't aware why Middle east wote are standing with Russia hivi sasa we bet majibu mnayo.
 

Wamekuja na video za kuokoteza eti Russia kachezea snake island. Wamefanya attemps nyings sana wamefeli tena wamepewa pigo takatifu. Ili kukwepa aibu wakaja na propaganda zao kuonesha Russia alichezea.

Propaganda za west zitaendelea kuwashika MATACORE hawa vijana wa NATO.

West is worst [emoji706][emoji706]
 
[emoji631][emoji1255] US Senator Rand Paul has blocked a fast-track vote to allocate $40 billion to Kyiv.

According to him, the United States cannot save Ukraine by dooming its own economy.
View attachment 2223327

US wajanja sana wameona maeneo yote muhimu yashabebwa na Russia kapiga hesabu kaona hasara hiii kwanini usikimbieee maaamaaaeeeeeeehhh[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Urusi hakuwa na aircover hata ya recon drone?
Mkuu kwani lini Urusi alikuwa na air cover. Hata Kyev aliingia kama gurioni vifaru vinakuja kama viko parade angani hamna kitu wanapigwa tu.
Pale Snake island wiki hii ambapo boti tatu za Raptor ambazo mojawapo iliwahi msindikiza Putin kwenye naval base ziliposhambuliwa na Bayraktar TB2 kuna radio communication zilinaswa Warusi waliokuwemo kwenye boti wanalalamika hakuna air cover.

Palepale Snake island ambapo video clip moja ipo YouTube inaonesha Bayraktar inashambulia Russian position na Pantsir air defence system ipo active na radar inazunguka ila ikashindwa kufanya engagement. Tatizo lao ni lile lile mbona hata Moskva cruiser ilikuwa na radar na mizinga kibao ila ilishindwa kuipiga Bayraktar na ikashindwa kuzuia makombora mawili ya Neptune.

Hapo hapo Snake island kuna video nyingine ilionesha Bayraktar inashambulia helicopter ni kama jamii ya Mi-17 na kuilipua kwa kutumia guided bomb.

Sasa kama walishindwa kulinda Snake island wangewezaje kulinda pontoon bridge iliyoshambuliwa na artillery. Kumbuka artillery haina ulinzi, ni kumuwahi anayekushambulia ukatumia counter battery radar ukasoma yuko wapi na ukamshambulia kwa artillery zako. Sasa Russia artillery wanazotumia zina range fupi kuliko baadhi ya artillery walizopewa Ukraine mfano Caesar ya Ufaransa. Russia anazo Koalitsiya zina range ndefu sana ila kama kawaida yake, silaha nzuri na zenye gharama hana uchumi wa kufanya mass production kwahiyo hazipo sana kwenye matumizi.

Pontoon bridge ni very vulnerable ni kama beach landing kunakuwa na uhakika wa kupoteza wanajeshi na silaha kadhaa. Ila sio kupoteza kikosi kizima
 
Ukiwauliza baada ya kuwapa kichapo mbona hamjaichukua wanatoka mbio
 
Huyu Zelensky ni muongeaji mzuri sana anajua kupanga maneno utadhani alikuwa kwenye siasa kitambo kumbe ndio kwanza ameanza na gundu. Tumwombe mungu aiepushe dunia na majanga ya vita.
Huyu Zele Hana muda nawaambieni...Putin na majasusi wenzake wenzake walijipanga aisee..they planned for a long war....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…