Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Tuambie vigezo vya kujitosheleza vikoje.
Ushahidi uliokamilika mfano nyaraka zinazoelezea shughuli ya hizo maabara.

Ushahidi wa silaha zilizozalishwa ndani ya hizo maabara.

Hizo tuhuma zilikuwa sehemu ya propaganda za Putin tu ili kupata uungwaji mkono wa walimwengu.
 
Ukraine yadai kuizamisha meli ya Urusi karibu na kisiwa cha Snake..

Kama tulivyoripoti hapo awali, meli nyingine ya Urusi imezama karibu na Kisiwa cha Zmiinyi (Snake) katika shambulio dhahiri la makombora la Ukrain.

Sasa, mkuu wa ujasusi wa Ukraine, Kirill Budanov, anasema wanajeshi wa nchi hiyo watapigania kisiwa hicho "mradi tu", akiongeza kuwa watakiteka tena kutoka kwa Warusi.

Kisiwa cha Snake ni eneo muhimu kimkakati kwa Ukraine na Urusi, kwa vile kinaruhusu ufikiaji wa Bahari Nyeusi kwa njia za biashara zilizo wazi, uagizaji wa silaha na kwa suala la uwezo wa Urusi pia kutekeleza kutua kwa majini kwa busara.

"Mtu yeyote anayedhibiti kisiwa hicho anaweza kuzuia harakati za meli za raia katika pande zote kuelekea kusini mwa Ukraine wakati wowote," Budanov alisema.
 

​

HABARI ZA HIVI PUNDE: Picha ya vifaru vya Urusi vilivyoshambuliwa na kuharibiwa na Ukraine wakati wa jaribio la kuvuka mto​

Mtaalamu wa masuala ya usalama na mhudumu wa zamani wa Uingereza Justin Crump anasema juhudi za Urusi "zimeshindwa pakubwa".

Lakini anasema madai ya Ukraine ya kuwaangamiza zaidi ya wanaume 1,000 huenda sio kweli.

Akizungumza na BBC, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la usalama la Sibylline Ltd anakadiria kuwa zaidi ya Warusi 140-180 waliuawa.

Anaeleza kuwa magari 70 au 80 yaliripotiwa kuharibiwa katika shambulio la Ukraine.
1652451386176.png
 
Ushahidi uliokamilika mfano nyaraka zinazoelezea shughuli ya hizo maabara.

Ushahidi wa silaha zilizozalishwa ndani ya hizo maabara.

Hizo tuhuma zilikuwa sehemu ya propaganda za Putin tu ili kupata uungwaji mkono wa walimwengu.
Tuambie kwny nyaraka zilizowasilishwa na Russia Ni nyaraka gani ambazo wewe uliona zime-miss.
 
Muda ni rafiki ngoja tuwe wapole tu.. maana hapa tunashabikia vitu vidogo.... ni sawa na msemo unaosema " mnatufunga lakini chenga twawala" hiyo ukraine inazidi kuzama, jamaa Putin yuko serious sana tofauti na tynavyomsikia kwenye vyombo vya habari vya magharibi.. hiyo ukraine anazidi kuikata na sidhani kama ardhi aliyochuku atairudisha nafikiri tunakumbuka krimea.. angalia hiyo ramani.. miji yote ya kherson, Morioupa, donets, luhansiki yote kachukua.. sasahivi odesa bado masaa tu maana bandari yake kaifunga kabisa....

View attachment 2222951
mwanzon walisema alikuwa kafika Kyiv , au ilikuwa propaganda?
 
Kufananisha US invasion in Afghanistan vs Russian operation in Ukraine kunaonesha jinsi gani ujuzi wako kwenye haya mambo ulivyo, no offense!

1. Us invasion of Afghanistan ilifanywa baada ya Afghanistan kudhaifishwa na vikwazo. 1999 UNSC walipitisha resolution no 1267 lililoitambua Alqaeda na Taliban kama makundi ya kigaidi na kuwawekea vikwazo kwenye funding, travel na silaha. Kitendo hiki kiliidhohofusha sana Afghanistan iliyokuwa chini ya taliban. Ukraine [emoji1255] kabla ya kuvamiwa haikuwekewa vikwazo kwanza walikuwa na ushirikiano mzuri na west na tangu 2014 Us/Nato wamekuwa wakiifadhili jeshi la ukr kwa hali na mali.

2. Us hakuivamia Afghanistan peke yake bali alikuwa na Uk ambaye baadaye alisaidiwa na Canada France Germany Australia wakati Urusi kaingia Ukraine mwenyewe. Kumbuka US walitangaza vita kbs dhidi ya /TalibanAlqaedaAfghanistan wakati urusi anafanya special operation tu. Learn the difference

3. Afghanistan baada ya kuvamiwa walikuwa isolated kbs na dunia nzima hakuna hata aliyewaonea huruma achilia mbali kuwasaidia kwa silaha na military infos wakati Ukraine anasaidiwa na majority ya dunia kuanzia silaha taarifa za kiitelijensia na hata solidarity kila mahali ss hv utaona #IstandwithUkraine

4. Us hakuwekewa vikwazo kufuatia uvamizi wake Afghanistan wakati urusi amewekewa vikwazo visivyoidadi mpk sasa

5. US hawakuwa na utaratibu wowote wa kuzingatia maisha na usalama wa raia wasio na hatia. Wengi waliuliwa wakati wa uvamizi huo hasa wanawake na watoto na hakukua na nafasi ya diplomasia. Urusi anachukua tahadhari kuruhusu raia waondoke maeneo hatarishi (humanitarian corridors) wakati huo mazungumzo yanaendelea na yanapopiga hatua mapigano anayapunguza ref. Kuretreat kiev baada ya kupiga hatua kidogo kwenye diplomasia, anatoa misaada ya kibinaadamu kwa raia wa ukr na wanajeshi waliojisalimisha na waliotekwa.


Ukiachilia hayo yote bado haikuwa rahisi kudefeat taliban wakati huo. Iliwachukua miezi miwili takriban mpaka kuwadefeat taliban na kuweka serikali ya muda (uvamizi ulianza oct 7 mpaka Taliban kukolapse dec 9). Mataifa makubwa kuungana na kuidefeat taliban dhaifu (vile) kwa muda wa miezi miwili sio jambo la kujifaharisha kwalo. They should have done better. Miaka 20 baadae mambo yamerudi kama zamani na hakuna kilichokuwa tofauti, what a waste!

Unaposema lengo lilikuwa kuhakikisha US soil haishambuliwi tena na magaidi unakosea kwa sababu huwezi kujua what the future holds. Tunaombea yasitokee lkn magaidi hawatabiriki miaka michache kuanzia ss hv huwezi kujua yepi yatatokea ndio kwanza muda mchache ss hv tangu us atoke afghan. Ugaidi ni swala la kukemewa duniani kote

Urusi amefanya operation yake hali ya kuwa ana vikwazo kwa maelfu. Anazingatia raia waso na hatia na kutoa nafasi kwa diplomasia, misaada ya kiutu, hajatumia silaha nzito sana (sio vita kamili), hajasaidiwa na taifa lolote lile, ukraine wanapata misaada kila uchwao, propaganda dhidi yake kila mahali duniani, mamluki kwa maelfu kuisaidia ukr, nk. Nk. Lkn bado anafanya progress kuelekea kukamilisha malengo yake.

1. Demilitarization
2. Denazification
3. Russian speaking UKRnians
4. Ukr not to join Nato*
Nakazia
US kashatumia mpaka MOAB huko AFGHAN
Ila US dhaifu sanaa!!!
 


HABARI ZA HIVI PUNDE: Picha ya vifaru vya Urusi vilivyoshambuliwa na kuharibiwa na Ukraine wakati wa jaribio la kuvuka mto​

Mtaalamu wa masuala ya usalama na mhudumu wa zamani wa Uingereza Justin Crump anasema juhudi za Urusi "zimeshindwa pakubwa". Lakini anasema madai ya Ukraine ya kuwaangamiza zaidi ya wanaume 1,000 huenda sio kweli.
Akizungumza na BBC, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la usalama la Sibylline Ltd anakadiria kuwa zaidi ya Warusi 140-180 waliuawa.
Anaeleza kuwa magari 70 au 80 yaliripotiwa kuharibiwa katika shambulio la Ukraine.
View attachment 2223077
Uzuri wa Ukraine akikupiga analeta na picha. Lakini hawa wengine wanasema wamelipua meli 3, ndege 4, helicopter 3, drones 30 za Ukraine pale snake island lakini hakuna picha hata moja.
 
Ila hii ambush waliyofanya Ukraine ni hatari,siku mbili zilizopita drone za Ukraine ziligundua uwepo wa hilo pantoon bridge la Urusi wakijiandaa kupitisha vifaa vya kivita Kama vifaru,magari ya mizinga,na vifaa vingine vya kijeshi jamaa wakaacha warusi wajae waanze kuvuka wakashambulia Kwa artillery karibu vifaa vyote vimeharibiwa



Baada ya mashambulizi



Magari takribani 73 pamoja na vifaru vimeharibiwa vibaya na artillery za Ukraine.

Kweli Marekani hakukosea alovyosema sasa NI mwendo wa kupigana mizinga tu,hizi Howitzer alizotuma US kule Ukraine zitawatesa Sana warusi
Urusi hakuwa na aircover hata ya recon drone?
 
Back
Top Bottom