Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?


Interesting.. Nikisoma majenerali wa Marekani wanashangaa kwa nini Warusi hawakujifunza kutumia jeshi la anga kwa namna ya kisasa.

Maana siku ya kwanza walishindwa kumaliza roketi zote za SAM na baadaye walidungwa na Javelin, hivyo hatuoni tena ndegevita za Urusi katikati na maghribi mwa Ukraine.

Kinyume chake ndege za Ukraine bado ziko, kama juzi walishambulia hadi Kisiwa cha Nyoka, ingawa ndegevita za Ukraine si za kisasa....
 
Unaandika kwa hisia kali sana huku ukiandika porojo tu.
Ni mahaba niue yanakufanya uandike haya.

Mwenzako nilimuuliza USA akishawahi kupambana na nani akashinda!? Mnabakk kutuketea ngojera mara ho!! Tubishane mara oh!! Sijui nini.

Mimi nataka ulete taarifa zako hizo kwa evidences. Mimi nakupiga kwa fimbo za knowledge siyo hisia.
Kwanza tunaanza na Wagriki. Hivi unajua boundaries za utawala wa ugriki!? Wale wakiishia mashariki ya kati tu mwanangu. Hata huku africa hatuna hata harufu ya wagriki.

Urusi ilikuwepo miaka na miaka. Na itaendelea kuwpo sana.

Kwanza unatakiwa ujue kuwa Russia ni nchi inayojitosheleza kwenye natural resources. Haihitajj kwenda kwenye nchi zingine dhaifu ili kuiba mali zao.

Unaongelea USSR ya juzi tu. Mwanangu nakusihi jifunze kuhusu urusi na upate kuijua.

Nakupatia mfano wa hivi karibuni tu. Mgogoro wa Syria, USA na wenzake walitaka kuleta mapinduzi. Lakini mzee Russia alipoingia pale wote waliufyata mkia. Sijajua kama wewe ni mfuatiliaji wa Geopolitics.

Basi ngoja tuachane na Syria. Tuongekee Venezuela. Hawa hawa USA walitaka kuleta mapinduzi. Lakini mzee wa siku Russia akatia timu tena wazi wazi hao USA wakaufyata mkia wakabaki kubwekea tu kwenye CNN, BBC na Aljazeera.

Sehemu yoyote Russia akitia timu USA lazima akimbie.

Nakushangaa unaongelea B2 Bomber. Mwanangu nadhani hufuatilii issue za international weapons. Russia anakudungua akiwa amekaa home. Anakupiga huko huko kwako bila kutumia ndege.

Nikutoe tongotongo tena. Unajua Arctic Ocean!? Mzee huko Russia kapakana na USA, Canada na wengine. Huko Russia anatumia ubabe kuchukua maeneo ya USA na Canada. Hakuna yoyote anayeweza kukoroma. Maana Russia is the father of this planet.

Nakusubiri ulete hoja ya nguvu ili tuweze jadiliana.
 
Ukitaka ustaarab kujadiliana mwenzetu hapa sio mahala pake, umezungumza vizuri ila sio ajabu kuna mtu atakutukana hapa.

JF ya sasa sio ya miaka hiyo. Kumejaa utoto na upuuzi mwingi sana mzee...
 
Ushauri mzuri saana
 
Analysis ya kibabe...

Ingawa hakuna kuelekezana kwa hoja hapa ni ushabiki kwa kwenda mbele [emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Nakuvutia picha na kiroho chako kidogo ukijaribu kutoa mfano [emoji847], hapa huezi kueleweka jomba bila kujichetua akili kusifu yaliyopo.
 
Umeongea kishabiki sana kama wazee wa kahawa, hauna detailed information kujenga mantic ya hoja yako
 


Kama kalinigrad mpaka leo wameshindwa ichukua kwa Mrussi sijui wataweza nini hao NATO. Hapo ni somo tosha kuonesha udhaifu wao.
 
Siku hizi harushi ndege maana zinadondoshwa...
Urusi alitudanganya kaharibu ndege zote za Ukraine, nashangaa snake Island imelipuliwa na ndege za Ukraine
Siku zote idadi kamili ya siraha huwa ni siri.
 
Acha kulia lia kitoto apa leta mafanikio ya Russia kwenye hii operation yake ili na sisis tuyajue tofauti na apo utakuwa unampigia mbuzi gitaa yaani wewe tuwekee mafanikio ambayo Russia kayapata kutokana na huu uvamizi wake
Safi kabisa atuletee mienendo ya vikosi vya Russia tuone walivyokuwa bora.
 
Umeandaka MASHUDU
 

Jeshi la Russia lilifukuzwa Kiev?! I don't think so...the Russian army withdrew from areas near Kiev.

A tactical retreat...majeshi ya Ukraine yalifika kwenye maeneo kama Bucha after three days days when the Russian army had withdrwan...ila kwa propaganda west na Zele watasema the Russian army was defeated...never on Earth

The Russian army will be back in Kiev...there is no doubt about it...
 
Umeongea kishabiki sana kama wazee wa kahawa, hauna detailed information kujenga mantic ya hoja yako
Nina uhakika kisu changu kimegonga mfupa. Hapa Nkerebhuke unashusha pumzi ya moto huku unajipiga kifua.

Kijana wangu nakusihi jitahidi kujielimisha na uiruhusu akili yako itunike vizuri.

Kijana wangu. Russia ni nchi inayoogopwa sana na NATO. Nanajitahidi sana kukwepa direct conflict na Russia. Nimejaribu kumfumbua macho mdogo wako kwamba kunaeneo la Arctic Ocean. Hebu nenda kajielimishe kidogo. Hao USA na NATO ni wababe wa Africa na nchi za kiarabu. Lakini mbabe wao hao wote ni Russia.

Nimekuambia uende ukasome mgogoro uliopo huko Arctic Ocean. USA yupo NATO wapo lakini Russia kawaambia jaribuni muone. Wamebaki kuzunguka na makaratasi huko UN.

Ngoja nikua chape na nondo nyingine. Unaujua mgogoro ukiopo huko japani kwenye Kuril Islands!? Russia aliwaruhusu wajapani wawe wanaenda kutembelea huko bila VISA. Baada ya kujifanya kiherehere wamezuiliwa hawatakiwi kwenda tena kula upepo.

Kijana wangu unajua hivyo visiwa vipo karibu sana na Japani. Na japani anaendelea kupiga kelele tu kuwa visiwa ni vya kwake lakini dunia yote inaogopa maana hawataki direct conflict with Russia.

Ngoja niishie hapa nisikuchoshe maana watu wengi wenye mwandiko kama wako ni wazembe kusoma.
 
Urusi waWamepigwa mpaka Marekani wameanzisha "DISINFORMATION BOARD" Na director wake Nina Jankowicz kuregulate taarifa za mitandaoni na wapemewa rungu la kufuta ama kuedit taarifa yeyote.

Ni jinsi Gani Urusi anachapika mpaka wanaficha taarifa za Urusi Marekani na ulaya ..... Aseee Mungu tusaidie Urusi tumepigwa aseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…