Kwanza nikurekebishe kiswahili kidogo japo mimi siyo mwalimu wa kiswahili.
Badala ya kuandika nazani hebu andika nadhani.
Back to topic:-
Nimejaribu kukueleza mambo mengi ili kidogo upate ABC za Russia.
USA huwa wanasherehekea uhuru wao waliopata mwaka 1776. Kipindi hicho Urusi ipo na imekula Millennium na inaelekea kula ya pili.
USA ni kikundi cha wafanya biashara kadha wa kadha. Wapo hapo kwaajili ya maslahi yao wenyewe. Huku Russia ipo pale kama taifa lenye historia yake na utamaduni wake. USA haina utamaduni wake. Is a big tent.
Huyo huyo USA tulimpatia nafasi kujipima ubavu wake huko Vietnam nadhani unakumbuka namna alivyoangukia pua.
Basi tusiongelee masuala ya Vietnam tuongelee tu issue za miaka ya 2000s. Juzi kati tu. Sujui issue ya Afghanistan ilipovamiwa na USA ulikuwa na umri wa miaka mingapi. Lakini nakupatia ndo ndo ndo tu. USA mpaka leo wanahaha hawajui cha kufanya.
Nisiende mbali sana, kuna nchi ya Waajemi inaitwa Iran hao USA kila siku wanabweka tu na sanctions kibao. Wamefanya nini!?
Nikikuambia huyu USA kwa Russia ni mchumba uwe unaelewa. Achana na movie za akina Rambo watazififisha akili zako. Unatakiwa ujue hizo ni movie zinatengenezwa kwenye computer are not real.
Nimejaribu kukupatia conflict iliyopo arctic ocean Russia anawaburuza USA na washirika wake. Wamebaki kupiga kelele tu kwenye media.
Kama unataka tujadili hebu leta hoja zito zenye mashiko utuoneshe ni wapi USA anaweza kupambana na Russia.
Kaka unapenda historia. Utapenda kusikia: Mwaka 1776 Urusi ilikuwa mbali na milenia yake ya kwanza. Warusi wenyewe wanapenda kuanza historia mnamo mwaka 998, wakati mtawala ya Kyiv alibatizwa na kuamuru watu wake wote wabatizwe pia.
Waukraine wanaihesabu kama kuzaliwa kwa Ukraine. sehemu zilizoendelea kuwa Urusi zilikuwa mkoa wa kando wa Kyiv wakati ule.
Urusi yenyewe ilianzishwa kama utemi wa Moscow kuanzia mnamo 1263, wakati ule nchi ndogo chini ya utawala wa Wamongolia.
Sasa Urusi kuburuza Marekani kwenye Aktiki?? Tutaona. Kwa historia itoshe kujua kwamba Alaska ilikuwa koloni ya Urusi, ikauzwa na Urusi na Marekani ilinunua mwaka 1867 kwa dolar 7,200,000.
Maana tayari wakati ule Urusi ilikuwa kubwa lakini dhaifu kiuchumi, ilhali Marekani ilisogea mbele.
Nakubali kabisa kwamba Rambo, superman na Captain America ni mambo ya kitoto na Marekani inaonekana imepita kilele chake.
Ila kuhusu Marekani kukosa utamaduni??
Hmmm, mbona Warusi wanapenda kuvaa Blue Jeans, wamekopi musiki wa Jazz (wakiwa na bendi nzuri sana ya aina hiyo) na bado wakati wa ukomunisti waliomba Cola ije kwao. Baada ya mwisho wa ukomunisti, walipanga foleni kuonja chakula kile (cha ajabu) cha Hamburger (ambayo mimi sipendi).
Mwaka 2021 kulikuwa na vituo 847 za MacDonald's nchini Urusi.
Hii itoshe kukumbuka udhaifu wa utamaduni wa Marekani nchini Urusi.