Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Na Putin kamuambia nini? sababu kuna mtu kaniuliza unajua Rais wa Finland alichoambiwa? Yaani leo Putin anapigiwa simu kupigwa biti? wonders will never end?

Putin has become a punching bag now. even Finland.
Putin alimwambia Finland haina haja ya kujiunga sababu hakuna kitisho chochote ambacho kinatishia usalama wa Finland.

Lakini tukumbuke ni Putin huyuhuyu alisema hatoivamia Ukraine na akaja ivamia.
 
Lavrov wiki hii inayoisha alikuja afrika baadae akaenda arabun
Anakula perdiem na madem wakati wanajeshi wao wanauwawa Ukraine. Huyu jamaa na Putin sijui watawaeleza nini warusi vile ambavyo wanajeshi hawatarudi nyumbani baada ya hii operation.
 
Putin alimwambia Finland haina haja ya kujiunga sababu hakuna kitisho chochote ambacho kinatishia usalama wa Finland.

Lakini tukumbuke ni Putin huyuhuyu alisema hatoivamia Ukraine na akaja ivamia.
mbona kuna jamaa hapa anatoa kauli kama vile Putin amempiga jamaa biti kali sana?

haya mambo bwana, kuna siku nilikuwa na mfinland mmoja iringa tunakula bia, kwa maelezo yake ni kwamba Finland wanaitamani sana russia, wana historical feelings kali sana against the russians.
 
Mdogo wangu huwa sipendi watu wanaoandika uongo:-

1. Blue jeans were actually an accidental discovery in the 18th century, when people in Nimes, France attempted to replicate a sturdy Italian fabric called serge.

2. White Castle traces the origin of the hamburger to Hamburg, Germany with its invention by Otto Kuase. Some have pointed to a recipe for “Hamburgh sausages” on toasted bread, which was published in “The Art of Cookery Made Plain and Easy” by Hannah Glasse in 1747.

SASA REKEBISHA TAARIFA YAKO KWANZA NDIO UJE TUJADILIANE.
Kwanza nashukuru unakubali milenia ya Urusi ilikuwa ama 1998 (ukiamini masimulizi yao) au kihistoria zaidi itakuja bado baada ya 2200.

Kuhusu blue jeans sina sababu ya kukukubali. Suruali yoyote ya kitambaa kizito si Blue Jeans. Asili ya neno "jeans" ni mji wa Genova, italia ambako kitambaa hicho kilianzishwa. Asili ya Blue Jeans alikuwa bwana Jacob David aliyeimarisha suruali kwa kutumia ribiti akazitengeneza pamoja na Levi Strauss kuanzia mwaka 1872.

Hamburger ya Marekani haina soseji, ilibuniwa New York,
 
Jeshi za kijamaa huwa zimejaa ufisadi
Angalia jeshi la Tz la kipindi hiki ni kama sehemu ya ajira tu
Kuna mzee mtaa naoishi nyumba yake ni kama kambi ya jeshi ana watoto 6 watano ni wanajeshi

Kajaza pia jeshini mashemeji zake kama wote nadhani ikitokea vita atawandikia watoto wake UN-FIT ili wasiingie mstari wa mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha nimecheka Sana aisee.....😁😂😁😂 Umeiweka hoja hii kimzahamzaha lakini hoja yako ni nyeti Sana na hasa kuhusu ajira kwa vyombo vya dola in our beloved country...ngoja nisiendelee...
 
Wewe umesema n mdau wa siasa andaeni viongozi wazalendo kama uko kwenye nafasi ya kutunga sheria onyesha ushawishi Tanzania itakukumbuka daima kwa ujasiri, uthubutu na ushujaa wako.
Hakuna kitu kisichobadilika wakipatikana watu sahihi kwa wakati sahihi.
Mkuu, Viongozi wazalendo wanaandaliwa na jamii. Wote sisi ni wadau muhimu katika siasa na upatikanaji wa viongozi. Ukumbuke viongozi wa chini kuanzia level ya kijiji mpaka uwaziri wana nafasi kubwa sana ya kuonyesha matokeo kuliko viongozi wa juu kama waziri mkuu na raisi.

Raisi akiwa mzalendo lakini ana watendaji wasio wazalendo atakachofanya ni kuonyesha ushujaa wake kwenye nchi kwa mtindo wa misimamo tu ila hatafanikiwa kwa sababu watendaji wake watakuwa wanafiki kwake na wengine waoga hawatataka kufanya maamuzi na atahujumiwa.

Raisi asipokuwa mzalendo ila makatibu wakuu, wakurugenzi, madiwani, mabalozi, mawaziri na wananchi ni wazalendo atapata wakati mgumu sana kuongoza maana atakosa watendaji wa kufanya mambo kwa maslahi yake binafsi.

Tunahitaji jamii kwa ujumla wake izalishe wazalendo na si tutegemee chama cha siasa au viongozi kufanya hii kazi.
 
Kwanza nashukuru unakubali milenia ya Urusi ilikuwa ama 1998 (ukiamini masimulizi yao) au kihistoria zaidi itakuja bado baada ya 2200.
Kuhusu blue jeans sina sababu ya kukukubali. Suruali yoyote ya kitambaa kizito si Blue Jeans. Asili ya neno "jeans" ni mji wa Genova, italia ambako kitambaa hicho kilianzishwa. Asili ya Blue Jeans alikuwa bwana Jacob David aliyeimarisha suruali kwa kutumia ribiti akazitengeneza pamoja na Levi Strauss kuanzia mwaka 1872.

Hamburger ya Marekani haina soseji, ilibuniwa New York,
oya mwana, huu uzi wa vita bwana.
 
Tubaki kwenye tekinolojia. Urusi inafahamika ni nchi iliyobaki nyuma lakini iliwekeza asilimia kubwa ya mapato yake kwenye jeshi kushinda nchi yoyote nyingine (tukiacha kibete kabisa kama Korea Kaskazini kando).
Silaha hizi nyingi za nyuklia hazisaidii kitu. Kuanzia idadi fulani umefikia uwezo wa kuua adui yako mara mbili au tatu, kuna faida gani kuongeza uwezo wako kumwua mara kumi au ishirini?? Marekani na Urusi wameshapita viwango hivi. Ona:
View attachment 2224485
Maana pande zote mbili walipunguza idadi wakielewa haina faida. Uwezo wa "overkill" bado upo mara kadhaa. Kila upande unaweza kuangamiza upande mwingine mara kadhaa.
Tena kuna uhakika kwamba, hata kama nchi imeshaharibika, kuna nyambizi za kutosha zenye roketi zinazoweza kumaliza upande mwingine.

Kuhusu "hypersonic": istilahi hii inamaanisha roketi ianyofikia kasi juu ya mach 5. je unajua roketi moja ya kimabara (intercontinental rocket) ya nchi yoyote ambayo haifikii kasi hiyo??? Mimi sijui.

Hii Sarmat RS-28 iwasaidie nini?? Ubora wake kulingana na roketi zilizopo unaonaje??

Ila udhaifu wa Urusi kitekinolojia upo katika tekinolojia ya kompyuta ambayo ni muhimu kwa mashine, magari, silaha, hata kilimo. Hapo nimetaja mfano wa droni: Urusi haina uwezo wa kutosha kuunda silaha ya kisasa kwa tekinolojia yake yenyewe. Wanategemea vipuri kutoka Marekani, Asia na Ulaya Magharibi.
China haipeleki chipsi ambazo ni muhimu Urusi kwa sababu wanategemea hataza za Marekani. Makampuni yake hayaruhusiwi kuuza elektroniki hiyo kwa Urusi. Watatafakari mara kadhaa kabla wasianze kuuzia Urusi maana wanategemea biashara na magharibi - Urusi si mteja muhimu vile.
Nimegundua jambo moja. Wewe huijui Urusi.

Hebu taja vipuli vipi kwenye military weapons Russia anaagiza kutoka huko. Naomba utaje.
 
Anakula perdiem na madem wakati wanajeshi wao wanauwawa Ukraine. Huyu jamaa na Putin sijui watawaeleza nini warusi vile ambavyo wanajeshi hawatarudi nyumbani baada ya hii operation.
Najiuliza hiv huu msaada wa dola b.kadhaa Biden anaoidhinisha Ukraine apewe km wangewekeza kwenye nyumba za bei rahisi us kungekuwa kweli na walala nje??? Wanasiasa watu wabaya sana[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Kwanza nashukuru unakubali milenia ya Urusi ilikuwa ama 1998 (ukiamini masimulizi yao) au kihistoria zaidi itakuja bado baada ya 2200.
Kuhusu blue jeans sina sababu ya kukukubali. Suruali yoyote ya kitambaa kizito si Blue Jeans. Asili ya neno "jeans" ni mji wa Genova, italia ambako kitambaa hicho kilianzishwa. Asili ya Blue Jeans alikuwa bwana Jacob David aliyeimarisha suruali kwa kutumia ribiti akazitengeneza pamoja na Levi Strauss kuanzia mwaka 1872.

Hamburger ya Marekani haina soseji, ilibuniwa New York,
Mzee unaongea upupu tu unanipotezea muda wangu. Sipendi ubabaishaji.
Neno Hamburger limetokana na mji ukiopo ujerumani. Acha ubabaishaji iki tujadiliane vizuri.

Nikikwambia USA haina utamaduni maana ni nchi iliyoanzishwa siyo muda mrefu sana. I meanzishwa miaka ya 1776.

Halafu hakuna sehemu nimekubaliana na ideas zako ambazo hazina mashiko.

Ukipata elimu vizuri njoo tujadiliane.
 
Najiuliza hiv huu msaada wa dola b.kadhaa Biden anaoidhinisha Ukraine apewe km wangewekeza kwenye nyumba za bei rahisi us kungekuwa kweli na walala nje??? Wanasiasa watu wabaya sana[emoji41][emoji41][emoji41]
Basis ya Uchumi wa US ni private economy, na hizo nyumba za bei ghari ndio zinawafanya wawe hapo walipo.
 
Raisi wa Ukraine huenda alifanya kosa kutaka kujiunga NATO na kuleta huu mzozo, nasema huenda sababu sijajua ni nn kilimsukuma kutaka hilo na kwann raia wake hawakumzuia. Huenda walimuona Urusi kama adui zaidi ya mshirika na jirani maana ni mzozo wa muda mrefu.

Jambo ninalopinga mm ni maamuzi ya Urusi kuipiga Ukraine kwa sababu hii move imemfanya aonekane bully na kuhalalisha sababu ya Ukraine kutaka kujilinda naye. Amezipa uhalali pia nchi jirani kufikiria kufanya hivyo.
Yaani jamaa alifanya wrong move hili wala halitaki tochi.

Kuhusiana na raia lipo wazi maamuzi ya wachache ambao ndio sirikali wanaweza wakaamua wawapelekeshe vp.

Mwisho kuna hotuba moja aliwahi kuhojiwa PUT IN sijajua yalini ila inaonesha yamuda.

Alisema aliishi katika mitaa gan cjui huko RUSSIA akajifunza kwamba ukiona kuna tishio lakutaka kupigana basi uwe wakwanza kupiga (nahisi umenielewa MKUU)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Hapo umesema.Hizi ndio diplomasia katikati ya matatizo,Kitu kimoja tu hutakiwi kurudi nyuma nacho ni iwapo kuna mwanamume anamnyatia mkeo halafu anafanya hivyo mbele yako na mbele ya wanaume wenzako.Hapo hata kama umwembamba kama sindano tuna inavyowezekana na pigana mpaka mwisho na huenda ukashinda. Haya mambo mengine ya vita vita lazima utumie akili na mara nyengine vuta masafa.Si ushujaa kupigana na mtu unayemuona kakuzidi kwa namna nyingi kwenye ulingo. Iwapo zelensky ameona lazima awatii mayahudi wenzake na airidhishe Marekani.Baada ya hasara aliyowatia wananchi wake mpaka hapa angepaswa kusema haya basi yaishe na hapo angevuta muda kurudia ajenda yake huko mbele.Sio muda huu kila siku nchi inanyakuliwa na uti wa mgongo wa nchi yake umeshamtoka na bado anatoa jeuri.,
Anachokifanya mrusi baadhi ya maeneo ni namna bora ya kupigana.Iwapo imekuwa shida kuiteka Kyiv au kuvuka mto kwanza anarudi nyuma kuweka sawa silaha zake na kupanga mbinu nyengine za kukwepa vikwazo na wala si kukimbia au kuwaachia Ukraine.Yeye Zelensky kila siku analazimisha kusonga mbele hata kama ameshagonga ukuta.Huo ni ujinga wa mapambano.Wale askari wake wa Azov/Mariupol wameshamshtukia na kama wachache waliobaki wakitoka salama nahisi wataanza kumuwinda na yeye kwa kuwatoa muhanga.
Hakika MKUU
Jamaa akili zake buure kabisaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani jamaa alifanya wrong move hili wala halitaki tochi
Kuhusiana na raia lipo wazi maamuzi ya wachache ambao ndio sirikali wanaweza wakaamua wawapelekeshe vp
Mwisho kuna hotuba moja aliwahi kuhojiwa PUT IN sijajua yalini ila inaonesha yamuda
Alisema aliishi katika mitaa gan cjui huko RUSSIA akajifunza kwamba ukiona kuna tishio lakutaka kupigana basi uwe wakwanza kupiga (nahisi umenielewa MKUU)

Sent using Jamii Forums mobile app
🤣. Kwa hiyo amekuwa wa kwanza kupiga? Anyway, mm namuombea ashindwe na arudi kwenye mipaka yake halali.

Masuala mengine yafuate diplomasia au mbinu za kijasusi zisizohusisha uvamizi wa kijeshi.
 
Back
Top Bottom