Kama Urusi ingejikita kuyatwaa hayo maeneo ya Ukraine mashariki toka awali huenda wangeshayatwaa na wasingeangukia kwenye fedhedha waliyonayo hivi sasa hasa baada ya kushindwa kuiteka Kyiv.
lee van cliff idawa
Proved
Hakuna fedheha yoyote Urusi imepata.
Mimi,wewe,CIA na NATO hatujui mipango ya Urusi ikoje.
Pia hata baadhi ya wanajeshi wa Urusi hawajui mipango yote ya Urusi ikoje ili kuepuka kutoa Siri pindi wakitekwa.
Mipango ya vita hua ni Siri za makao makuu ya jeshi na makamanda wa ngazi za juu.
Kwa hiyo Mimi na wewe tuangalie vita kwa nje inakwendaje.
Nakumbuka Putin alisema hawataki kupiga Kyiev kwa sababu huko Kuna Decision makers,hivyo bado wanategemea mazungumzo kumaliza vita hii,hayo ni Nia njema sana.
Kama unaamini kweli kuwa Urusi kashindwa kuikamata Kyiev basi nakupa pole sana.
Kwa resources alizonazo Urusi na akidhamilia kweli Kyiev haisumbui.
Kuna General mmoja wa German juzi katoa maoni yake kua Urusi inaipiga Ukraine kistaarabu,na Ukraine waisidhani wanaweza kuishinda Urusi.
Bandiko liko humu.
Huyo ni kama anamuunga mkono Gen wa Marekani nae alitoa kauli kama hiyo
Andiko limo humu.
Hakuna fedheha yoyote Urusi kapata zaidi ya fedheha kwa NATO.
Unaamini Urusi inapigana na nchi zaidi ya 30?