Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Taarifa za muda mchache uliopita zinaonyesha hali inazidi kuwa mbaya kwa jeshi la Urusi, kwa sasa ina upungufu mkubwa wa wapiganaji, kutokana na wanajeshi wengi wa Urusi kuuawa kwenye Vita ya Ukraine, hali hiyo imepelekea Bunge la Urusi kujadili mswada utakao waruhusu wazee na Raia wa Kigeni kujiunga na Jeshi kwa ajili ya Vita ya Ukraine. Hii ni fedhea kwa Jeshi la Urusi ambayo inajinasibu kuwa na Jeshi kubwa duniani.

Safari hii lazima Putin Afundishwe adabu na ndo kwaanza mapema kabisa hadi November nazani akili itakuwa imemkaa sawa.

________________________________________


Bunge la Russia linatarajiwa kujadili mswada utakaoruhusu raia wenye umri wa zaidi ya miaka 40 na raia wa kigeni wanaoishi nchini humo wenye umri wa kuanzia miaka 30 kujiunga na jeshi.

Hatua hii ni ya Russia kuimarisha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine, baada ya kupoteza wanajeshi kadhaa katika vita vinavyoendelea.

Taarifa iliyoandikwa kwenye wavuti wa habari za serikali ya Russia, Duma, imesema kwamba hatua hiyo ni ya dharura, inayolenga kutumia ujuzi wa watu wazee wenye uwezo wa kivita.

Kwa sasa, wanajeshi wenye umri wa kati ya miaka 18 na 40 ndio wanaoruhusiwa kujiunga na jeshi la Russia.

Russia imepata pigo kubwa sana kwa kupoteza wanajeshi na silaha katika vita vya siku 86 sasa, ambapo Ukraine umefanikiwa kuwashawishi raia wake kupigana na kupinga uvamizi wa Russia.

Japo Russia imedhibithi Mariupol, imeshindwa kufikia malengo yake katika vita hivyo pamoja na kushindwa kudhibithi Donbas, mashariki mwa Ukraine.

Wakati huo huo, waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu amesema kwamba Russia imeanda kuunda vikosi 12 vya jeshi katika sehemu za magharibi, kwa matayarisho ya kile ametaja kama vitisho vinavyoongezeka katika sehemu hiyo, akisema vinatokana na Finland na Sweden kuomba kuwa wanachama wa NATO.

Chanzo VOA

View attachment 2232267
Hakuna tatizo mbona hata Ukraine anao wazee vitani? tulia mmetaka vita ndefu sasa mtaipata
 
Anaeamini Urusi atashinda hii vita basi akapimwe akili sio mzima kabisa.Rusia anawezaje kushinda vita kwa wababe USA na NATO wakati mifumo yote ya kijeshi na kiuchumi wanaiendesha wao? Yani kuna watu Bado wanaamini Rusia awashinde NATO kweli basi haya ni maajabu .
Kwa kuwasaidia tu huu ndiyo mwisho wa Putin kama Rais wa Urus na ndo mwisho wake pia hapa Duniani.
Labda Putin wa Buza, kwahiyo Ukraine alipotangaza kuwa miaka 18 mpaka 60 wanaume wabaki ulifikiri wanakata vitunguu? vita hii NATO ametaka kuwa iwe ndefu sasa tulia hata Warusi wanao wazee
 
Unajua n nn mwamba......au basiii tuu siko kinyume na ww ila naona tunaelekea kama ya babeli maana kuna pro Russia mwingine alidai magu angekuwepo tungekua na barabara🤣🤣🤣🤣akajibiwa aaache ukichaaa wote hao n timu moja.
Tukianza kuforecast vitu hata CIA,M16 wameshindwa kunusa according to jamaa uliyemjibu ila wakagundua Russia inaivamia Ukraine na ikawa ivyo sisi wa huku ololosokwani tuchambue kutokana na tunavyovipokea kutoka source mbalimbali.

M nashauri tu stikii kwenye mada.
Mdau eeh... Au basi tu (Nimeiga intro yako)

Ni hivi mdau, mie nimependa Galip Vrl alivyopangua hoja. Ni kwa namna hiyo tunapata kujifunza na kupanua uelewa wetu, kua team moja isiwe kigezo cha kukubaliana kila jambo kisa limesemwa na member mwenzetu.

Hatupo kushambuliana wala kubishana hapa bali tupo kuelimishana au sio mdau? So mambo yanapendeza kama hivyo yaani. Itapendeza kama Mr Tyang nae akirudi kupangua hoja za Galip Vrl hakika mjadala utapendeza.

Every truth is perspective but not every perspective is truth. Kila ukweli ni mtazamo lakini sio kila mtazamo ni ukweli.

Umetoa mfano mzuri hapo mdau, MI6, Mossad, Pentagon + CIA na Intelligence nyingine ya mataifa zaidi ya 30 wameshindwa kung'amua mbinu za Putin na nini anataka. Sie tubaki na kile tunachokiona tu mbele yetu.

Ama tukiamua kuelezea ili kutowachanganya watu basi tuseme kwa kutanguliza neno "maoni yangu kwa kile kinachoendelea ni kadha wa kadha".

Maana hapa mwingine ambaye hana uwezo kama wa Galip Vrl wa kutazama mambo kwa kina kalibeba hilo kalipeleka kijiwe cha kahawa kuwaambia Putin anataka kuchukua eneo la mashariki awafanye Ulaya kua tegemezi wake ili kustablize Uchumi wake kitu ambacho na mimi naungana na Galip Vrl kusema si kweli.
 
Putin mwezi wa 3 huu bado unasumbuliwa na Zelensky.

Hebu njoo Tanzania tukupige makamanda waliomchakaza IDD Amin kwa muda mfupi bila kuwasahau M23 kule Congo.
 
My friend, Kuna Ndugu anaitwa Askari Kanzu tulikuwa wote humu Toka wahuni wa Benghaz wanafanya uhuni! Hakuna Askari wa Ghadaffy alihasi. Hao wahuni wa Benghazi hawakuwa Askari bali Mamluki kutuko Nje ukichanganya na dissidents wa kiraia!
====
Ngoja nikutafutie uzi wa sakata hilo la Libya lakini Sasa tujikite kwenye mjadala huu. Wa Ukraine kupigika!
Samahani, lakini nakumbuka askari wasio wachache wa Gaddafi walihamia upande wa upinzani. Ona hapa taarifa ya malta times, marubani mawili ya Gaddafi yalipeleka ndege zao Malta baada ya kuamriwa kutupa mabomu Bengazi.
Updated: Libyan fighter jets arrive in Malta
Kulikuwa na majenerali na makanali kama vile Abd el Fattah Yunis, Khalifa Haftar, Suleiman MAhmoudi, El Hariri na wengine waliohamia upande wa upinzani pamoja na sehemu za vikosi vyao.
 
Pro-NATO kwavile hawana akili ya kuelewa madini yanayotoka kwenye vichwa vyenye akili hawakumuelewa putin juu ya hii kauli na walimudhihaki na kumusodoa kama mtu muoga anae waogopa Azov battalion ila sasa muda wa wao kuelewa kauli hiyo ya kimukakati umefika baada ya kauli hiyo waliyoibeza kuwafukua panya zaidi ya 2400 ndani siku 3.

Siku Putin anatoa hiyo order nilisema "Putin ni mtu smart sana analijua vizuri eneo hilo na anajua kabisa hakuna shujaa wa njaa wala majeraha hivo nisuala tu la muda hao panya wataanza kujitoa wenyewe na watakuwa na faida kubwa kwa putin hapo baadae kuliko ambavyo wangegeuzwa kuwa majivu"
Hatimae muda umefika na lengo kukamilika kwa 100% kama kichwa cha Kremlin kilivyoplan. PUTIN is genius and strategy leader na ndo maana ukiwa na akili ndogo isiyo ona mbali utachelewa sana kuwa unaelewa mipango ya PUTIN.

PUTIN siyo Ramadhan Kingai anaedili na ugaidi wa laki5 ni Rais wa nchi kubwa zaidi kuliko zote Duniani inayoitwa THE GREAT RUSSIA FEDERATION [emoji635]
Pro Russia ni hazina ya taifa.
Wewe ni kichwa,"kichwa Kwerikweri"
In Jiwes voice
 
Samahani, lakini nakumbuka askari wasio wachache wa Gaddafi walihamia upande wa upinzani. Ona hapa taarifa ya malta times, marubani mawili ya Gaddafi yalipeleka ndege zao Malta baada ya kuamriwa kutupa mabomu Bengazi.
Updated: Libyan fighter jets arrive in Malta
Kulikuwa na majenerali na makanali kama vile Abd el Fattah Yunis, Khalifa Haftar, Suleiman MAhmoudi, El Hariri na wengine waliohamia upande wa upinzani pamoja na sehemu za vikosi vyao.
CIA hawafanyagi kazi kindezi na katu hamuwezi kuhisi wapo nyuma ya plotu. Unakijua kisa cha Patrice Lumumba.
Kifupi wanatumia resource za local.
Whatever ila Gadafi alikuwa mwiba kwao na bila wao angekuwepo mpaka leo.
 
Marekani yasikitika kuripoti kuwa majeshi ya Russia leo hii jumamosi yamezinywa shehena kubwa za silaha na vifaa vya kivita toka Marekani na nchi za Ulaya vilivyopelekwa Ukraine kuisaidia serikali ya Zelensky...

Shehena hizo za silaha za mabepari ya kimagharibi zilizoingizwa Ukraine, zimeshambuliwa na kuangamizwa katika mikoa ya Zhytomyr na Donbas kwa kutumia yale makombora 'pendwa' ya Russia yaitwayo Kalibr cruise missiles

Pia huko Odesa, majeshi ya Russia yameunguza miundombinu ya kuhifadhia mafuta, na pia yametungua ndege mbili za kivita za Ukraine aina ya Su-25 na kuziangusha droni 14 za Ukraine (watakuwa wamezichoma kwa kutumia zile silaha zao ngeni za mionzi ya leza za kuchomea drones)

View attachment 2232975
View attachment 2232925
Hizo ndege zimepigwa kwenye air combat chap zikashushwa na hizo drone uchwara
 
Yaani hawa jamaa wanatabia kama skirts wanaziba juu chini kuko wazi, sasa hapo kuna umuhimu gani wa vikwazo?????

Kitu pekee kinachowashinda ulaya sasa hivi ni kuona aibu kuomba msamaha Kwa Putin, lakini wanaumia pakubwa
Ha ha haa aisee Pro Russia mma vijineno kwa kukera .
"Tabia za Sketi,imeziba juu chini Iko wazi"
 
Hivi ndiyo vichwa vya Pro-Russia halisi, mahaba zero. Mnachuja ukweli wa kila taarifa mnayoipata haijalishi imetoka kwa nani.

Salute sana Mkuu 🤩👊
Ha ha ha kawaida tu Mkuu...😌

Unajua n nn mwamba......au basiii tuu siko kinyume na ww ila naona tunaelekea kama ya babeli maana kuna pro Russia mwingine alidai magu angekuwepo tungekua na barabara🤣🤣🤣🤣akajibiwa aaache ukichaaa wote hao n timu moja.
Tukianza kuforecast vitu hata CIA,M16 wameshindwa kunusa according to jamaa uliyemjibu ila wakagundua Russia inaivamia Ukraine na ikawa ivyo sisi wa huku ololosokwani tuchambue kutokana na tunavyovipokea kutoka source mbalimbali.

M nashauri tu stikii kwenye mada.
Yah ni kweli, jomba weye unashangaa Pro-Putin kupingana kwenye Issue ya Magu... Mbona hapa kitaaambo tu baadhi CDM wameungana na baadhi ya CCM kusimama upande wa Russia na hao hao baadhi wameungana kusimama upande wa Westerners.

Issue ni huwa ni kufanana kwa mitizamo, kisha kuungana kwa kile kilichopo mbele yenu kwa wakati huo 😂😂😂. Nyote mnavaa surual wa kiume na wa kike lakini haimaanishi kisa wamevaa wote surual basi wana jinsia moja.

Ko kupishana nje ya Russia we enjoy tu jomba.

Mdau eeh... Au basi tu (Nimeiga intro yako)

Ni hivi mdau, mie nimependa Galip Vrl alivyopangua hoja. Ni kwa namna hiyo tunapata kujifunza na kupanua uelewa wetu, kua team moja isiwe kigezo cha kukubaliana kila jambo kisa limesemwa na member mwenzetu.

Hatupo kushambuliana wala kubishana hapa bali tupo kuelimishana au sio mdau? So mambo yanapendeza kama hivyo yaani. Itapendeza kama Mr Tyang nae akirudi kupangua hoja za Galip Vrl hakika mjadala utapendeza.

Every truth is perspective but not every perspective is truth. Kila ukweli ni mtazamo lakini sio kila mtazamo ni ukweli.

Umetoa mfano mzuri hapo mdau, MI6, Mossad, Pentagon + CIA na Intelligence nyingine ya mataifa zaidi ya 30 wameshindwa kung'amua mbinu za Putin na nini anataka. Sie tubaki na kile tunachokiona tu mbele yetu.

Ama tukiamua kuelezea ili kutowachanganya watu basi tuseme kwa kutanguliza neno "maoni yangu kwa kile kinachoendelea ni kadha wa kadha".

Maana hapa mwingine ambaye hana uwezo kama wa Galip Vrl wa kutazama mambo kwa kina kalibeba hilo kalipeleka kijiwe cha kahawa kuwaambia Putin anataka kuchukua eneo la mashariki awafanye Ulaya kua tegemezi wake ili kustablize Uchumi wake kitu ambacho na mimi naungana na Galip Vrl kusema si kweli.
Yah uko right mkuu, kufunzana na kuelimisha sio kukubalian kwa kila jambo bali kuelekezana kukubaliana kwa mambo yaliyo mengi.

Binafs mahaba sina, ila napenda kutizama vitu au kukaa upande wa vitu vinavyo make sense!

Pale nitakapoambiwa kua
A ni sawa na B,
B ni sawa na C,
C ni sawa na M... Basi nategemea pia kuona A ikiwa sawa na M, Otherwise logically hiyo equation haiko sawa.
 
Back
Top Bottom