lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,485
Pro Russia Ina watu ma NGULI Kwerikweri.Siku nikipata muda nitaanzisha uzi wa malengo makuu ya Russia kwenye hii operation. Najua wengi wanajua ni NATO ila hiyo ilikuwa kama entry gate tu ya putin kuingia na kuanza kukamilisha malengo yake mama kwa masilahi ya nchi na watu wake. Kuhusu kujiunga NATO siyo issue sana kwa Urusi issue ni NATO kuweka millitary bases karibu na mipaka yake, hapo hata uwe Mna NATO kwa miaka 20 Moto utawaka.
Ngoja nigusie tu lengo kubwa la hii operation ya Urusi, lengo kuu lililojificha nyuma ya pazia nikuifanya Ulaya hasa "EU" waendelee kumtegemea Urusi katika kuendesha uchumi na maisha yao ya kila siku, Putin anaamini hiyo ndo njia pekee ya Urusi kubaki imara kiuchumi na kiushawishi.
Je Ukraine anahusika je hapo?; Ukraine ndo nchi pekee huko ulaya inayoelekea kufanana na Urusi kwa suala la Rasilimali na bidhaa za kilimo yani reserve ya mafuta, gas, umeme, mazao na n.k, hivo basi putin alivyoona uhusiano wa Ukraine na watumwa wake wa EU unaelekea kukua hadi kuanza kushirikiana mambo mengi, akastuka ili awa wahi mapema kabla hawajaanza kuweka mitambo yao ya ku utilize oil and gas reserves iliyopo mashariki mwa Ukraine, pili anajua vizuri kabisa "EU" hawana ardhi ya kilimo kama aliyo nayo na Ukraine na anae walisha kila siku ni yeye na Ukraine, kwa hiyo ili abakie kama tegemezi kwao nilazima Ukraine awe underdog kwake.
Sasa basi ili hilo lengo likamilike nilazima yeye au vibaraka wake ndo wawe controller wa hayo maeneo mhimu yanayo windwa na westerners kwa lengo la kujiondoa kwenye utegemezi wa Urusi. na njia pekee iliyokuwepo kufanikisha hilo lengo nikuyachukua hayo maeneo kijeshi maana kisiasa tayari Zelensky alikuwa ashaoelewa na westerners, so Urusi iliona kuendelea kutumia siasa nikuendelea kujimaliza wenyewe. Na ndo maana Tangazo la kwanza kabla ya kuingiza vikosi Ukraine, Putin alitangaza kuyatambua majimbo ya DRP na LRP kama states huru maana ndo target yake na ndo kuna rasilimali nyingi mfanano na za Urusi zinazotegemewa sana na Westerners. Unganisha na Dot za kuyathibit maeneo ya Crimea, Zaporizhzhya nuclear power plant, Mariupol, snake island na Odesa(still on fire)
Naomba niishie hapa, details zaidi zitakuwa kwenye Uzi (nikipata muda mzuri one day) ila Russia yupo tayari kutumia hata nukes ili tu Ukraine mashariki iwe chini yake. Inahitajika akili ya utulivu sana kuelewa plans za Kremlin chini ya Putin maana hata EU, G7,NATO na UN wazielewi kabisa ndo maana kila siku wanaishia kuingizwa choo cha kike tu.
Nawasilisha.
Wewe bwana utakua unashusha nondo kutokea Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi.
Uko weeeeel informed.