Wapiganaji wa mwisho wa Ukraine waliojibanza katika eneo la kiwanda cha chuma cha Azovstal cha mji huo sasa wamejisalimisha, maafisa wa Moscow wamesema.
Kwa miezi kadhaa vikosi hivyo vilikuwa vimezingirwa katika jengo hilo kubwa, na kuizuia Urusi kuwa na udhibiti kamili wa mji huo.
Uokoaji wa siku ya Ijumaa unaashiria mwisho wa kuzingirwa na uharibifu zaidi wa mji wa Mariupol ambao sasa umesalia magofu.
Mji huo na kiwanda chake cha chuma sasa "umekombolewa kabisa" baada ya wanajeshi 531 wa Ukraine kuondoka katika eneo hilo, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema.
"Vituo vya chini ya ardhi vya kiwanda hicho, ambako wanamgambo walikuwa wamejificha, viko chini ya udhibiti kamili wa majeshi ya Urusi," iliongeza katika taarifa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema walinzi wa mwisho waliosalia kaika eneo hilo wameruhusiwa kuondoka.
"Leo wapiganaji hao walipokea ishara ya wazi ya amri ya kijeshi kwamba wanaweza kutoka nje na kuokoa maisha yao," aliiambia kituo cha televisheni cha Ukraine mapema Ijumaa.
Kwa wiki kadhaa eneo hilo la Azovstal ilikuwa limezingirwa kabisa.
Vikosi vya Urusi vilizuia misaada yote ya kibinadamu kuingia, na kulishambulia eneo hilo kutoka angani na kuwataka watetezi wake waliobaki kuweka chini silaha zao na kujisalimisha.
Wengi wa wale waliokwama ndani walikuwa raia, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto na wazee. Mapema mwezi huu waliondolewa baadhi kufuatia mazungumzo magumu yaliyoratibiwa na Umoja wa Mataifa na Shirika la Msalaba Mwekundu ambayo yalidumu kwa wiki kadhaa.
Lakini kuendelea kukataa kujisalimisha kwa wapiganaji hao wa Ukraine kulimaanisha Urusi haikuweza kuwa na udhibiti kamili wa mji huo wa bandari ya kimkakati.
Kwa raia wengi wa Ukraine, inawaona wapiganaji hao wa Azovstal waliojisalimisha kuwa mashujaa wa kitaifa ambao walionyesha upinzani wa ukaidi wa nchi dhidi ya Urusi.
Mamia ya wanajeshi waliojificha kwenye mahandaki ya kiwanda hicho ni pamoja na wanamaji, Jeshi la Ulinzi la Taifa (ikiwa ni pamoja na kikosi cha Azov), walinzi wa mipaka, polisi na vitengo vya ulinzi wa eneo.
Walipiga kambi na kupungua kwa vifaa vya chakula na hakuna maji, waliishi kwa wiki katika bunkers chini ya ardhi na mahandaki bila kuona mchana.
Chanzo:BBC
SASA WE PIMBI NJOO UBISHANE NA WANAGHARIBI WENZIO