Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Nusu ya dunia isipokuwa hai itabaki hiyo nusu nyingine. Dunia ina watu bilioni 8 kwa sasa, nusu yake ni bilioni 4. Mwaka 1960 wakati Africa inapata Uhuru dunia yote ilikuwa na watu bilioni 3.
 
Africa haitapata maendeleo kwa Marekani na Ulaya kuanguka kiuchumi au kuangushwa na Urusi bali itazidi kuwa maskini zaidi kwa sababu itakuwa koloni kamili la China. Mtanyonywa rasilimali zote na Wachina, watachukua tenda zote za ujenzi na watawapa mikopo kwa riba na terms wanazozitaka wao kwa sababu watakuwa hawana mshindani tena hapa Africa.

Africa imekuwa maskini kwa sababu raia wake wengi wajinga na viongozi wake wengi ni majanga na hawana maono yoyote ya kiuongozi zaidi ya kubaki madarakani. Marekani ndio imesaidia kumaliza Polio barani hapa bila wao wengi wenu mngekuwa vilema sasa hivi.Mlipopukitika kwa janga la Malaria wao ndio walikuaa wa kwanza kulimaliza na kuwaletea dawa, mkipigana vita na kuuana wenyewe kama mazombi kama ilivyotokea Sudan wao ndio wa kwanza kuja kuwapatanisha na wakichelewa kama ilivyotokea Rwanda mnapiga mayowe kuwalaumu kama walevi wa gongo.
 
View attachment 2242119
⚔️⚔️⚔️Russian soldiers capture Elon Musks Starlink components used by Ukrainian army⚔️⚔️⚔️
Kwa ambao wame like bila kukijua hicho kifaa..

maelezo:
Starlink is a broadband satellite internet network developed by Musk's SpaceX company that aims to beam internet access to customers anywhere in the world (as long as they have a Starlink satellite dish to connect to the satellites
 
Mkuu kama wa Africa tunahitaji another alternative ya development model kwanini US na EU ndo watuambie jinsi ya kuendelea, hapana China sio mnyonyaji kama USA na EU kwahiyo kubadoli kwa world balance of power, huenda tukapata the second chance ya kuanza upya na kusahisha pale tulipo kosea ila US na EU are economic evils in Africa development wakianguka ni furaha kwetu wa Africa
 
Marekani anakusaidia hadi kufundisha mbwa wa kunusa dawa za kulevya msiwe mateja wote. Pia anakupa na msaada wa kutahiri magovi ili kasi ya Ukimwi ipungue. Sehemu nyingine anakujengea na vyoo.

Hizi ndo Fikra za vijana wa Africa ambaye haamini kwenye kujitegemea fwala sana, mwanaume ukishakua unapenda vya bure namashaka na wewe [emoji2380]
 
Hizo ni explosives reactive armour (ERA) blocks ambazo ni milipuko iliyofungwa nje ili kuzuia HEAT (high explosives anti tank) rounds. Kwa makombora ya zamani ya vifaru na RPGs kama RPG 7 vinazuilika na hizo ERA blocks. Ila kwa modern anti tank weapons zinatumia secondary explosives kwahiyo zinapita. Explosive ya kwanza inalipua ERA na ya pili ndio inapenya.

ERA imetengenezwa kiasi kwamba ukiipiga risasi hailipuki, ukiichoma moto haiungui, haiko more sensitive ila inaweza respond haraka na hit from a missile. Na kuna namna imefanywa izuie chain explosion kwamba ikipigwa block moja inalipuka hiyo tu.
Tatizo la ERA ni kwamba hawatakiwi kuwepo infantry pembeni watarukiwa na milipuko, na hiyo block ikishapigwa inabaki nafasi wazi mpaka uje kufanya maintenance.

Nashindwa kuendana na uzi kwa kuwa una comments nyingi sana na sipati updates au notification. Napata notification baada ya 12 hours, ilianza ni after 24 hours.
 
Hicho kifaa ni sawa tu na satellite dish .Kina pokea mawambi ya internet kutoka low Earth orbit satellite za Elon. Cha ajabu kipi hapo?
 
Kama mmeshindwa kuutumia uhuru wenu kujiletea maendeleo ni ujinga wenu. Ila ni afadhali kubwa kuwa maskini huru kuliko na maendeleo chini ya mkoloni, kaburu au dikteta.
uhuru mlio nao toka 1961 umewasaidia nini mpaka sasa? mmeaachieve kitu gani cha maana kama taifa?
 
Minimum ya RUSSIA kwenye hii OP nikuanzia miaka 10s
Jamaa hawakukurupuka na walijipanga nakujiandaa haswaaa
Ila umeandika ukweli mchungu kwakweli maana watu walikua wameaminishwa kwamba US EU na NATO yao wao ndio baba na ndio mama wa DUNIA
Ila kupitia hii OP mzee mzima RUSSIA katuonyesha NYETI za KUKU
RUSSIA sio ZIMBABWE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole na na kutingwa MKUU
Ila ahsante kwa hili darasa HURU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Russia au China hawawezi kuwapa mikopo, misaada, fursa za biashara, masomo, ujuzi, msukumo wa demokrasia na keheshimu haki za binadamu na kazi kama mnavyopata Marekani au Ulaya.

China anachofanya hapa Africa kwa sasa ni aibu kubwa zaidi, bidhaa zake zilizojaa Kariakoo ni earphones, cover za simu, urembo, toothpicks na jeans za kutoboka.Amechukua tenda za ujenzi hadi vibarua wa kubeba zega wanatoka kwake. Kwa hali hii sahauni kuwa na viwanda vya maana kama vile tulivyokuwa navyo muda mfupi baada ya uhuru tukaviua.

Urusi hakuna cha maana inachoipa Africa zaidi ya ngano ya kutengeneza maandazi, AK-47 na mbolea kidogo ya wakulima wa jembe la mkono kuganga umaskini wao ambavyo vyote tunanua kwa pesa zetu.
 
Unajua marekani inasaidia kwa maslahi binafsi na inaongiza kuumiza nchi za kiafrika kwa mikataba ya kinyonyaji? His viongozi unaosema ni vilaza na hawana maono ndio marekani inawataka,Marekani hii ambayo Ilimuua Patrice Lumumba kiongozi aliyekuwa na maono ndio unayotetea humu?
 
Tatizo la Africa sio development models. Muda mfupi baada ya uhuru Tanzania na mataifa mengine mengi walirukia development models za USSR na China ya Mao lakini chumi zao wote waliangukia pua na umaskini kushamiri.

Tatizo la Africa ni kwamba raia wake wengi ni wajinga na viongozi wake wengi hawana maono na maarifa ya kuhakisha utulivu nchi mwao, kuchochea ubunifu na biashara za maana katika nchi na kati ya mataifa yao.

Kwa sababu wameshindwa kufanya haya yote,maendeleo yamedumaa na wanawatumia Marekani na Ulaya kama "bogeyman" wao kwenye propoganda dhaifu.
Madikteta ya Africa yakisababisha mafarakano,vita, njaa na umaskini yanakimbilia kulaumu wazungu.
Inasikitisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…