Sovereignty ukiwa na maana gani?
Nikiwa na maana nchi huru yenye mamlaka ya ke ya kujiamulia mambo yake yenyewe kama vile Finland ilivyoamua kujiunga NATO.
Nchi zilizo na Kambi ya majeshi ya kigeni ni huru?
Ni huru. Ujerumani, Japan, Poland, Qatar, Korea Kusini ni nchi huru na siku wakiona kambi za kijeshi za US hazina faida kwao watawaambia waondoke.
Nchi zilizo kaliwa kimabavu baada ya vita ya pili ni huru?
Africa haikuwa bara lenye nchi mpaka mwaka 1884/85 ulipoketi mkutano wa Berlin na kuzigawa hizi nchi unazoziona leo hii. Hakukuwahi kuwa na serikali za nchi kabla ya vita vya pili vya dunia hivyo swali hili halina mashiko.
Je Urusi ndiyo ya kwanza kuvamia hapa ulimwenguni?
Hapana, sio ya kwanza na haitakuwa ya mwusho.
Libya ilivamiwa? Je kama haikuvamiwa kilichofanyika kilikuwa halali?
Libya haikuvamiwa, majeshi ya NATO yalienda kulinda raia waliokuwa wanauwawa na Gaddafi baada ya azimio la umoja wa mataifa la baraza la Usalama S/RES/1973 kupitishwa kwa wingi wa kura.
Iraq ilivamiwa? Kama sivyo hayo Mataifa yalichukuliwa hatua gani?!
Iraq tangu mwaka 1990 lilikuwa ni 'rogue sate' chini ya dikteta Saddam ilikuwa inavamia jirani zake kama Kuwait, inafadhili makundi ya kigaidi dhidi ya Israel na kufanya genocide kwa Wakurdi, Saddam alikuwa sawa na Amin na alinyongwa na WaIraq wenyewe.
Vipi Syria nae, kwa nini hawakuheshimu sovereignty ya Lile Taifa?
Sovereignty haina maana kiongozi anaweza kuua tu raia wake kwa Impunity ndio maana kuna ICC.
Tanzania ilisapoti waasi kwenye Mataifa ya Kongo, Uganda Burundi, tulifanya sahihi? au tuliingilia sovereignty yao.
Kusapoti waasi dhidi ya mtu kama Mobutu au Amin ni sawa, ila kuusapoti waasi dhidi ya mtu kama Hichilema, Uhuru au Chakwera ambao wamepigiwa kura na wananchi wao sio sawa.
Ukitambua siasa za Kimataifa na geopitics lazima utakiri Urusi ipo sahihi?
Eleza sababu zinazoifanya Urusi kuwa Sahihi kuivamia Ukraine.
Nafikiri mkuu yoda ni mfuasi wa ile Imani isemayo uongo ukiludiwa mara nyingi, basi hugeuka kuwa kweli.
1.Sovereignty ukiwa na maana gani?
Nikiwa na maana nchi huru yenye mamlaka ya ke ya kujiamulia mambo yake yenyewe kama vile Finland ilivyoamua kujiunga NATO.
Jibu
Tukubaliane hapa ni total sovereignty tunayoizungumzia hapa ni Ile ya kweli.
Hivyo utakubaliana nami iwapo itatokea Cuba kuweka makombora ya nyuklia ya kirusi watakuwa sahihi?
Kama si sahihi ,naomba utuelezee kwa nini USA alipiga kelele na kutokutaka siraha za nyuklia toka Urusi zisiwekwe Cuba, wakati ni nchi huru? Kumbuka Cuba missiles crisis.
Kama sivyo kwa nini Marekani anaingilia affair ya nchi nyingine.
Kwa nini Dunia haipigi kelele? na kupiga hii double standard.
2.Nchi zilizo na Kambi ya majeshi ya kigeni ni huru?
Ni huru. Ujerumani, Japan, Poland, Qatar, Korea Kusini ni nchi huru na siku wakiona kambi za kijeshi za US hazina faida kwao watawaambia waondoke.
Jibu
Hapa uliamua kupopoma.
Ni kwa sababu hakuna Taifa lenye majeshi ya kigeni na bado likwa huru.
Hiyo Ujerumani inalazimika kufuata sera za Marekani.
Mfano swala la gesi linaloenelea Sasa ni kuudhoofisha uchumi wake.
Japan nayo, raia wake hufanya Maandamano wakitaka jeshi la Marekani liondoke kwenye ardhi yao.
3.Nchi zilizo kaliwa kimabavu baada ya vita ya pili ni huru?
Africa haikuwa bara lenye nchi mpaka mwaka 1884/85 ulipoketi mkutano wa Berlin na kuzigawa hizi nchi unazoziona leo hii. Hakukuwahi kuwa na serikali za nchi kabla ya vita vya pili vya dunia hivyo swali hili halina mashiko.
Jibu
Dah aisee kumbe tuna watu wa sampuli hii afrika halafu tunataka maendeleo?
Labda huelewi maana ya nchi🥲🥲🥲
Kama hakukuwa na nchi?
Himaya ya Ethiopia ilikuwa nini?
Aksum kingdom ilikuwa ni nini?
Kongo kingdom ilikuwa ni nini?
Hehe kingdom ilikuwa nini?
Kilwa Sultanate
Mwenemutapa
Mirambo kingdom
4.kwa maelezo yako hayo?
Ni kuwa kungekuwa na Taifa lenye nguvu Toka afrika, lingeweza kabisa kuipiga Marekani kisa wanawauwa na kuwanyanyasa watu weusi kule kumbuka Black lives matter.
Je haujaingilia huo unaouita Uhuru?
Kama umeuingilia hauoni maelezo yako yanajicontradict na maana halisi ya sovereignty ulituhubiria?
Double standard
5.Iraq ilivamiwa? Kama sivyo hayo Mataifa yalichukuliwa hatua gani?!
Iraq tangu mwaka 1990 lilikuwa ni 'rogue state.
Jibu
Nani anayeamua Taifa fulani, lenye uhuru wake kamili ni rogue state?
Je Marekani kuendelea kuua watu weusi na kuwafunga kwa sababu za kijinga na mfumo kandamizi wa elimu na lenyewe ni rogue state?
Kuvamia Mataifa mengine under pretext kupelekwa demokrasia, sio ishara linasambaza tabu badala ya amani na maendeleo, haki ipi inayowapa kuishambulia Mataifa mengine wakati wenyewe wanafanya hayo hayo?
6.Sovereignty haina maana kiongozi anaweza kuua tu raia wake kwa Impunity ndio maana kuna ICC.
Jibu: Unafahamu kwamba Marekani sio member wa ICC.
Na mwaka Jana alizuia watu wake kufanyiwa uchunguzi wa makosa ya kivita huko Afghanistan.
Taifa kama hili tutaliamini vipi linaweza kulazimisha haki kwa wengine especially Russia.
7.Kusapoti waasi dhidi ya mtu kama Mobutu au Amin ni sawa, ila kuusapoti waasi dhidi ya mtu kama Hichilema, Uhuru au Chakwera ambao wamepigiwa kura na wananchi wao sio sawa.
Umeiona double standard au kifupi hujielewi unasimamia wapi?!!!
Kwa hiyo unakili Taifa likifanya jambo baya linapaswa livamiwe bila kujalisovereignty yake ndio? au hapana?
Hivyo utawala wa Israel unaoua na kunyanyasa wapalestina ukishambuliwa na Iran itakuwa sahihi, kwa sababu Israel ni rogue state? Jibu ndiyo au hapana.
Ukraine ikivamiwa ni sawa, kwa sababu Wana Neo Nazi? Jibu ndiyo au hapana.
Ulaya ikishambuliwa ni sawa kwa sababu wanatukuza ushoga na ndoa za jinsia Moja?
Jibu ni ndiyo au hapana.
Marekani akipigwa ni sawa kwa sababu aliuwa wahindi wekundu?
Jibu Ndiyo au hapana
Kwa maelezo hayo Mrusi yupo sahihi na hana KOSA, kenge maji[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]