Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hapo mkuu mrusi kujifanyia hujuma inakuwa na nguvu kuliko kama angefunga Kwa kusema nimeamua kufunga kwanini ni kwasababu

Akijifanyia hujuma maana yake kampuni za seamens watalazimika kuja kutengeneza sasa kama kuna vikwazo raia wa EU kipindi cha baridi hawata mlalamikia Putin Ila watawalalamikia viongozi wao Kwa kufanya maamuzi ya kujinga na hii itasababisha machafuko Kwa EU na kitu ambacho Putin anakitaka kama Putin akiamua yeye mwenyewe kufunga gas wananchi wa EU watashikamana na viongozi wao Kwa kuwa kitendo cha wao kukosa gas ni Kwa sababu Putin kaamua kufunga bomba la gas na Siyo maamuzi mabaya ya viongozi wao, sasa Putin hataki Kwa namna yeyote aonekane kuwa matatizo wanayopitia raia wa EU chanzo ni viongozi wao na Siyo putin
 
Nimekaona kamekula mweleka 🤣🤣🤣🤣 sasa atahutubia masaa manne huyu?
 
Na ajipange haswa akija kichwa kichwa analimwa ya kichwa tena, na hivi anapenda show off na visifa vya kijinga.
 
Swala kubwa hapa ni burden ya hizo fedha inaangukia wapi. Hizo fedha zinakuwa mzigo kwa wazalishaji wa dunia nzima kuwa dola inatumika kama sarafu ya dunia . Wanaprint wanapeleka World Bank tunakopeshwa tunalipa kwa riba kubwa baada ya.kuzalisha pamba kahawa na mafuta . Wao hawahitajiki kuzalisha kama sisi wanachapisha tu fedha. Kama dunia itawatenga kwa maana ya kuitenga dola basi inflationary rate yao itakuwa ya kutisha sana ukizingatia gharama kubwa za kuendesha majeshi na vyombo vyao vya usalama ambavyo kimsingi vinagharamiwa na sisi raia wote wa dunia.
 
Nimekaona kamekula mweleka 🤣🤣🤣🤣 sasa atahutubia masaa manne huyu?
Awezee wapi wakati inaonesha mwili hauna coordination hapo! Ilipaswa akae kwake apumzishe fuvu hilo huku akiomba toba!

Raia wa US nao sijuw waliwaza nini kiukweli... Biden 80yrs kasoro miezi tu. Yule Speaker Nancy Pelosi 82yrs. Wote na Babu Joe wakiwa wanazungumza unajiuliza ina maana US walikosa viongozi wakaamua kuishikisha mihimili miwili hivi vizee viwili? Majibu unakooooooosa!

Wanasoma ila wanapuyanga live questions waanzaje kutoboa!
 
Thanks 😂😂😂😂sisi maslow learner tuvumilieni yaani nakukusoma kote hapa sikuambilia kitu,kuna uyo alotoa mfano wa covid 19 kwangu ndio nimemuelewa wanatengeneza tatizo alafu linatatuliwa kwa kukopeshwa note zao ambazo zina masharti ya jinsi ya kulipa.
 
Leo si umeona maandamano London mkuu, imetangaza aljazila
 
kuna mambo yanachekesha sana,
ila nimegundua USA wajanja wajanja hivi, lakin IQ ndogo , Russia watulivu ila watu makin sana na high IQ
mwanzo nilikuwa neutral nikiangalia mwenendo lakin Russia jamaa wako makin sana
 
Kawaida tu shangazi ila sina hakika kama na yeye umemuelewa alichokimaanisha.

Fedha zilizotoka kwenye Covid-19 ni just a fraction ya hizo fedha... US kila mwaka ana deficit ya budget ya over trillion of dola. Hiyo deficit inasuluhishwa vipi? Hapo ndipo utakapouona mlango wa kuziingizia hizo fedha kwenye mzunguko.

Mfano we na Baba Yoyoo, mmepanga budget yenu ya 20k, ila makusanyo ya miradi yenu hapa na pale inafikia 11k, hivo 9k hauna... So inabidi ukakope si ndio?

Naam katika mikopo yako ukabahatisha 5k means 4k bado inahitajika right? Sasa zile bill ulizopanga na Baba Yoyoo za 4k unaingia chumbani kuprint.

So kile kipya unacho print unakiingiza kwenye mzunguko... N kwenye demand and Supply maana ake unaongeza Supply.

Demand and Supply iko hivi
1. High Demand with High Supply... The value is maintained constantly...

2. High Demand in Low Supply... The Value is Increasing

3. Low demand in Low supply... Rejea kwenye moja

4. Low demand kwenye high supply, inakua kinyume cha number 2... Thamani inaporomoka

Sasa ukirudi kwenye budget deficit ya US, Over 1 trillion dollar. Ambayo Iko on par na GDP ya 12th au 13th hivi of the world largest economies. Hiyo deficit haifidiwi kwa mkopo tu bali Printers zinahusika.

Kwenye ile Graph niliyokupa, Upande wa kulia inaonesha Jumla ya Fedha zilzio kwenye mzunguko. Upande wa kushoto unaonesha kiasi cha fedha kilichokua printed mwaka husika...

Ngoja niiweke tena...

Cha kutoa kwenye graph ni kama haya
1. Kila mwaka fed wana print fedha (Sio zile za kubadilisha chakavu pekee la hasha, za kuongezwa kwenye mzunguko) kupitia bills!

2. Kua 2020 na 2021 (mind you hapo 2021 kwenye graph haipo) US wamefanya over printing.

Mfano wa ziada, majuzi kati baada ya kuidhinishwa zile B40 dolla, Senator Rand Paul akawa anasema hizo fedha Serikali haina that means wakakope ili wapeleke Ukraine. (hapa china alihusishwa) wengine wakawa wanasema Fed watafanya mambo yao wana print kisha wanasafirisha.

Yote kwa yote issue za fedha ziko complicated sio lazima tuzijue deep kiiivyo. We kitendo cha kujua Putin anafanya nini mie nakupea salute tu 🤩🤩🤩
 
Additional note kuhusu nyakati za Covid ni hivi... Kipindi cha Covid ukichagiza na zile lockdown shughuli nyingi zilisimama hivo uchumi kuyumba.

Katika jitihada za kuimarisha uchumi huo hapa, feds waliongeza dola karib trillion karib 3 ndani ya miezi kadhaa.

Mwishoni mwa mwezi February 2020 US Feds balance sheet ilikuwa inasoma dollars trillion 4, mwezi June. Ikiwa ni miezi mi3 mbele US Feds balance sheet ikawa inasoma over 7 trillions dolla. Hizo fedha zote zimekuwa pumped in 😂

Hapo ni 4 hadi 7 miezi mi3 kati, Sasa again ikawaje zikatoka tena 7 hadi over 20, story nyingine tena hiyo...

That's why baadhi ya Pro-Russia wanasema uchumi wa US wa mchongo!
 

POINT
 

Ndomana hii mikopo nchi nyingi za Africa haziendelei ni mikopo inayofanya tuzidi kuwa maskini
 
🤩🤩🤩🤩🤩🤩 Thanks again wengine tujue kununua,chench,muamala na ya kutolea vingine tuwaachie nyie maalumni😂😂😂🙌🙌.
 
wayahuni hao hao ndio waliompa mrussi Siri za Manhattan project
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…