kt the irreplaceable
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 2,375
- 4,893
Braza lazima uelewe vita ni biashara, makampuni ya silaha marekani yanatafutiwa tenda kwa mbinu za hali ya juu. Ukraine alianza kuuziwa silaha mda mrefu na marekani, fuatilia hili utakuja kugundua kitu.Ndio maana nikasema kuwa "vita vya panzi, ni furaha kwa kunguru" nikiwa na maana kuwa hii vita ya Ukraine na Russia ni furaha kwa Marekani na nchi za Magharibi. Fikiria aina ya silaha inazotumia Urusi katika vita, idadi ya jeshi lake linalokwenda mapambanoni maana ameshaongeza jeshi baada ya baadhi ya wanajeshi wao kuuwawa, kutekwa, kujeruhiwa nk. Mpaka hii vita ikija kusimama Urusi itakuwa imeshapoteza askari wengi, silaha nyingi na gharama kubwa za vita. Pia hivi vikwazo vilivyowekwa sasa madhara yake ni mara kumi ya yale madhara aliyokuwa ameyafikiria Putin hapo kabla. Kwahiyo nguvu ya jeshi ya Urusi itashuka ukilinganisha na ile nguvu iliyokuwa nayo kabla ya vita (hii ndio point muhimu inayotafutwa na Marekani) Lakini faida nyingine kwa Mmarekani ni kwamba wakati Russia inapanga mipango ya kushinda vita kila dakika bila mafanikio, mmarekani na washirika wake wanatumia muda huo kuendelea kuunda silaha mbali mbali na jeshi lenye nguvu kwa ajili ya adui yeyote akiwemo Urusi ambayo sasa nguvu zake za kijeshi zitakuwa zimepungua kutokana na vita hivyo plus uchumi kuanguka nk.
Sio USA au nchi yotote ata risk nchi yake kwenda kupigana na Urusi physically. Ulaya wanajua madhara ya vita, uingereza ilianguka kutoka kua supe super power kwasababu ya vita.
Ukraine anatumiwa linapokuja suala la mafuta, gesi na kuuza silaha USA hana rafiki, yeye ni masilahi mbele.