LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Ndio maana nikasema kuwa "vita vya panzi, ni furaha kwa kunguru" nikiwa na maana kuwa hii vita ya Ukraine na Russia ni furaha kwa Marekani na nchi za Magharibi. Fikiria aina ya silaha inazotumia Urusi katika vita, idadi ya jeshi lake linalokwenda mapambanoni maana ameshaongeza jeshi baada ya baadhi ya wanajeshi wao kuuwawa, kutekwa, kujeruhiwa nk. Mpaka hii vita ikija kusimama Urusi itakuwa imeshapoteza askari wengi, silaha nyingi na gharama kubwa za vita. Pia hivi vikwazo vilivyowekwa sasa madhara yake ni mara kumi ya yale madhara aliyokuwa ameyafikiria Putin hapo kabla. Kwahiyo nguvu ya jeshi ya Urusi itashuka ukilinganisha na ile nguvu iliyokuwa nayo kabla ya vita (hii ndio point muhimu inayotafutwa na Marekani) Lakini faida nyingine kwa Mmarekani ni kwamba wakati Russia inapanga mipango ya kushinda vita kila dakika bila mafanikio, mmarekani na washirika wake wanatumia muda huo kuendelea kuunda silaha mbali mbali na jeshi lenye nguvu kwa ajili ya adui yeyote akiwemo Urusi ambayo sasa nguvu zake za kijeshi zitakuwa zimepungua kutokana na vita hivyo plus uchumi kuanguka nk.
Braza lazima uelewe vita ni biashara, makampuni ya silaha marekani yanatafutiwa tenda kwa mbinu za hali ya juu. Ukraine alianza kuuziwa silaha mda mrefu na marekani, fuatilia hili utakuja kugundua kitu.

Sio USA au nchi yotote ata risk nchi yake kwenda kupigana na Urusi physically. Ulaya wanajua madhara ya vita, uingereza ilianguka kutoka kua supe super power kwasababu ya vita.
Ukraine anatumiwa linapokuja suala la mafuta, gesi na kuuza silaha USA hana rafiki, yeye ni masilahi mbele.
 
Rais wa Ukraine ni mpumbavu,hivi ni Nchi gani hapa Duniani itataka waingie vitani na Mrusi??,hakuna hakuna hata mmoja yenye uwezo huo na ndio maana mbinu wanatumia ni kuungana Ulaya nzima.
Na tatizo wakiungana Ulaya nzima yaani NATO nzima kwenda kupigana na Russia hiyo inakuwa tena ni WWW3,swali ni kuwa USA+NATO wapo tayari kwa WW3???
 
Dunia kwa sasa yaangalia na hata weye huna budi kujifunza kwamba siku ingine Marekani, NATO na wengine wakitaka kuishambulia nchi yoyote ile ni lazima nao wakumbane na hali wanayokumbana nayo Russia kwa sasa.

Maana hatukuona kule Afghanstani, Iraq, Syria, Siera Leone na kwingine.

Dunia yasubiri kuona New World Order ikizaliwa.
Bado mataifa ya ulaya magharibi na Marekani wanahodhi mashirika makubwa ya habari yenye nguvu za kueneza ushawishi wao kila pembe ya dunia.

Hivyo kwenye propaganda itakuwa vigumu kuwashinda.....hata nchi zao zikifanya uvamizi/jinai zitapambwa zinafanya ukombozi.
 
Tuliambiwa hapa kufikia mida hii Kiev itakuwa majivu,ngoja tuwasubiri waliopo mstari wa mbele kwenye battle field watuletee LIVE hali ilivyo,si unajua JF inawakilishwa vyema kwenye mstari wa mapambano.
Uliambiwa na nani Mkuu??
 
Serous? Yaani ukitembelea forums wanazodiscuss haya mambo huoni wanaolaani? Hata kwenye pages za habari tu huwaoni unataka nikutajie?
Sasa huko kwenye forums wana nguvu gani?

Issues ya Ukraine, UN kalaani, EU wamelaani na kuweka vikwazo, FIFA na UEFA wamewafungia Russia,kuna baadhi ya timu wamekataa kuvaa label za makampuni ya Russia nk,mbona walishindwa kufanya hivyo kwa Iraq,Libya na Afghanistan hawakufanya hivyo?

Au mamilioni ya waliokufa Iraq,Libya na Afghanistan sio watu au hawana thamani?
 
Hypocrisy mixed with stupidity .
Ukraine wakitoa habari kuwa wanajeshi kadhaa wa Urusi samekufa katika shambulio fulan mnasema ni propaganda za media za west ila wakisema wanajeshi wao kadhaa samekufa kwasababu ya shambulio la Urusi hiyo si propaganda.
Ideot at it's best.
Wanajeshi kufa wa Urusi lazima wave,tinachobisha na hizo western media zenu ni kuwa Warusi wanakufa wengi kuliko wa Ukraine huku kila siku wanajeshi wa Urusi wanasonga mbele na Raia wanahama Nchi.
Sasa unajiuliza kama hao wanajeshi wa Ukraine hawafi kwa kiwango hicho inakuwaje wanajeshi wa Urusi kila kukicha wanachukua mini???
 
Mbona hujibu swali langu!? Swali la pili, leo umejamba mara ngapi!?
Usiwe unaongea kama umeibiwa mume na baba yako.

Sikia lugha za kuudhi watu humu tunazo, hatutaki tu uzi uharibike.
Tunaangalia tu hili tundu lako lisivyo na staha tunanyamaza.
Screenshot_20220301-155347_Chrome.jpg
 
Uliongea na Putin ndio akakuambia Mpango ilikuwa ni kuifanya Ukraine majivy within 24 hours au kuna siku aliwahi kutamka katika speech yake.

Usijifanye umesahau.. Kwanza alitaka wajeda wa Ukraine wamkamate rais wao wamkabizi kwenye jeshi lake, then akataka jeshi la Ukraine lijisalimishi mapema kabla ya homa NDUI haijaingia nchini mwao,jeshi likakataa kwasababu wanajua prezidaa wao hana makosa.
Putin na wapambe wake wa kasema Ukraine itakuwa majivu withini 24 hours lakini Mungu si Abdallah leo ni ijumanne bado hata hawajadhibiti ipasavyo miji kadhaa ya Ukraine.
 
Russia hataweza kushinda kwa kutumia Jeshi la ardhini, tena hizo Silaha zikifika ndio atakuwa anashambuliwa nyuma, mbele na kulia... Mataifa ya Ulaya yamesharuhusu Raia wake kwenda Ukraine kupigana vita hapo wataingia hadi wanajeshi wa hizo nchi
Raia wa ulaya waliojiunga na Isis ili kupigana Syria waliitwa magaidi na wasaliti na mataifa yao.

Ila watakaoenda Ukraine kupigana na Urusi watapongezwa na hata msaada wa silaha na malipo watapewa.

Dunia ni tambara bovu....
 
Back
Top Bottom